CCM imvue Uanachama na kumfukuza kabisa Chamani Askofu Gwajima haraka sana bila kuchelewa

Ikifanya hivi, ccm itakuwa imeondoka kwenye misingi yake ya kutetea wanyonge na kupinga maovu.Gwajima pamoja na mapungufu yake yote kwa hili ameonyesha uzalendo kwa nchi na chama
Gwajima hana uzalendo wa aina yoyote ile
 
Ndugu zangu Watanzania,

Lazima tukubali ukweli ya Kuwa Askofu Gwajima siyo mwana CCM na hajawahi kuwa mwana CCM kiuhalisia. Askofu Gwajima siyo Mwenzetu na hajawahi kuwa mwenzetu hata siku moja. Hajawahi kuwa na uchungu wala kuwa na maombi mema au mazuri kwa CCM.

Askofu Gwajima na Humphrey Polepole ni wale wale waliopitia na kupitishwa katika njia ile ile inayowafanya wasiwe na uchungu na CCM wala kujali chochote kile kuhusu CCM wala kuguswa na lolote lile kuhusu CCM. Askofu Gwajima yeye hata CCM ikifa leo kwake ni furaha na shangwe kubwa sana.kwa sababu hana upendo wala Mapenzi na CCM.

Huyu ni aina ya wale ambao walizolewa tu ,kuvalishwa sare zetu na kupewa zawadi ya Ubunge . Haijui CCM wala historia ya CCM wala Thamani ya CCM. Hana uchungu wa jasho ,Damu na machozi ya wanachama wenzetu waliomwaga Wakipigania ,kutesekea na kukitetea chama hiki ili kiendelee kusalia madarakani na kuimarika siku hadi siku. Hajui hata kuna watu walikesha maporini kulala sakafuni kwa ajili ya kueneza itikadi na sera za chama.

Ndio Maana yupo Tayari kutoboa Mtumbwi ili Maji yajae ndani na hatimae kuzamisha mtumbwi wa CCM na kuwaangamiza wote waliomo. Hana analojua kuhusu CCM zaidi ya maslahi yake binafsi ya posho , marupurupu na kiinua mgongo cha Ubunge wake. Amekuta kila kitu kimetengenezwa,kuandaliwa na yeye kupewa tu Ubunge wa Bwelele .ndio maana hana uchungu kwa CCM,ndio maana yupo kazini muda wote kuihujumu CCM na kutaka kuivunja vunja na kuipasua vipande vipande.

Ndio sababu hana adabu wala heshima wala staha kwa viongozi wetu . Ndio sababu anaweza kuongea na kutamka neno lolote lile kuwachafua ,kuwatweza na kuwavunjia heshima viongozi wetu. Hajui maadili ya chama chetu wala miiko yake wala taratibu zetu wala miongozo ya chama chetu wala kanuni zetu. Yeye ni kukurupuka na kuropoka tu atakavyo. Kwanini? Kwa sababu huyu siyo wa kwetu na wala siyo mwenzetu. Huyu ni mamluki tu aliye na kazi maalumu ya kuibomoa CCM yetu.

Anasema atabakia ndani ya CCM kusudi aendelee kutumia mwamvuli wa CCM kuichafua ,kuivuruga na kuipasua atakavyo na kwa kadri ya maagizo apewayo na wanaomtumia na kumtuma. Sasa itakuwa ni Uwendawazimu na ukichaa mkubwa sana kuendelea kumuacha na kumkumbatia mtu wa aina hii ndani ya CCM yetu. kuendelea kumwaga petroli chini huku akiwa na kijinga cha moto mkononi Mwake kwa ajili ya kukiangamiza chama kwa kuripua moto.

Narudia kusema ya kuwa huyu mtu siyo mwana CCM bali alizolewa tu na kuvalishwa valishwa nguo ili afanane na sisi kwa nje lakini ndani ya moyo wake hajawahi kuwa mwana CCM na wala hajawahi kuipenda CCM. Yeye dua yake ni kuona CCM inakufa na kuangamia na kupotea kabisa katika uso wa Dunia na historia ya Taifa letu. Sasa wana CCM wenzangu ni lazima tufahamu ya kuwa ni bora Joka kubwa lililo nje ya nyumba kuliko nyoka aliye uvunguni Mwa kitanda maana huyo wakati wowote atajikunjua na kung'ata wote walio ndani ,atagonga wote na kuacha Simanzi tu ndani ya nyumba na kisha kutorokea Gizani.

Askofu Gwajima Tayari ni adui yetu ambaye tunapaswa kumtupa nje haraka sana iwezekanavyo pasipo kuchelewa. Ni vyema afanye chochote kile awezacho kupambana na sisi na kwa usaidizi wa mtu au kikundi chochote kile lakini akiwa nje ya chama chetu na huku sote tukijua huyu ni adui yetu. Kuliko ajifanye ni mwenzetu huku akitoboa mtumbwi wetu halafu tuendelee kukaa tu kimya kwa kusema mbona ni mwenzetu na tupo naye chomboni.

Bila kuchelewa wala kuwa na subira Gwajima atolewe haraka sana chamani ili huko ndiko sasa aanze vita yake sasa. Ni bora kupambana na akina heche au kupeana mikono na akina heche unayejua kabisa ni mpinzani wako kuliko kuacha glasi ya maji mezani alipokaa gwajima kwa kusema ni mwenzako. Utakuwa ni huna akili kabisa ukifanya hivyo na kuamini hivyo na kutokuchukua tahadhari.

Kuendelea kumuacha chamani itajenga picha na taswira mbaya sana,itakuwa mfano mbaya sana kwa wanachama wengine juu ya usimamizi wa maadili ya chama,italeta na kuchochea uasi ndani ya chama chetu na inaweza kuleta majaribio ya Mapinduzi na kuondoa kabisa amani ,utulivu ,umoja na mshikamano ndani ya CCM.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Uko sahihi.Askofu ana chuki binafsi na utawala wa sasa.Ni mchonganishi na ana hasira ya kukosa kukusanya sadaka
 
Unaweza kosoa uongozi wa sasa kwa jambo moja tu?
 
Ujinga hauvumiliwi. Chama kinachoweza kuvumilia ujinga jinga hakiwezi kudumu.
Demokrasia ni pamoja na kuvumilia ujinga wa wajinga hata kama wewe ni muelevu. Ukimuita fulani mjinga kwa mtazamo wako, na wengine wanakuona mjinga kwa mitazamo yao. Ili tubalance maisha tujifunze kuvumiliana, hakuna mkamilifu katika ulimwengu wa demokrasia wala ulimwengu wa kiroho
 
Nimekieleza.
Changamoto ni kusema ukweli hata gwajiboy , na polepole wakikaa kimya bado watatokea wengine wa kuongea mimi nafikiri kama wanachoongea kama ni uongo basi kamati zitoke na kujibu au kuelezea kwa fact hiyo ndo njia sahihi unaweza kuwa ndani ya chama miaka 1000 na usiwe na uchungu ukawa wewe kila kitu hewala hewala na mtu anaweza kuingia leo tu akaona udhaifu na akaongea ukweli shida ndo inakuja kwanini huyu kaja juzi tu anaanza kuongea ukweli yeye anaongea kwa kuwa nyie wazoefu mliona na mnajua ukweli lakini mmechegua kukaa kimya je ipi ni solution kutoka na kuongea fact pasipo kuchanganya na mambo mengine binafsi ya mtu watanzania ni wasikivu wanasikiliza na kuchambua yupi yupo sahihi yupi anasema uongo
 
Kwa hiyo una uchungu na CCM kuliko wmaslahi ya wakulima na wafanyakazi ambao ndiyo Ile jembe na nyundo siyo?
Ndugu zangu Watanzania,

Lazima tukubali ukweli ya Kuwa Askofu Gwajima siyo mwana CCM na hajawahi kuwa mwana CCM kiuhalisia. Askofu Gwajima siyo Mwenzetu na hajawahi kuwa mwenzetu hata siku moja. Hajawahi kuwa na uchungu wala kuwa na maombi mema au mazuri kwa CCM.

Askofu Gwajima na Humphrey Polepole ni wale wale waliopitia na kupitishwa katika njia ile ile inayowafanya wasiwe na uchungu na CCM wala kujali chochote kile kuhusu CCM wala kuguswa na lolote lile kuhusu CCM. Askofu Gwajima yeye hata CCM ikifa leo kwake ni furaha na shangwe kubwa sana.kwa sababu hana upendo wala Mapenzi na CCM.

Huyu ni aina ya wale ambao walizolewa tu ,kuvalishwa sare zetu na kupewa zawadi ya Ubunge . Haijui CCM wala historia ya CCM wala Thamani ya CCM. Hana uchungu wa jasho ,Damu na machozi ya wanachama wenzetu waliomwaga Wakipigania ,kutesekea na kukitetea chama hiki ili kiendelee kusalia madarakani na kuimarika siku hadi siku. Hajui hata kuna watu walikesha maporini kulala sakafuni kwa ajili ya kueneza itikadi na sera za chama.

Ndio Maana yupo Tayari kutoboa Mtumbwi ili Maji yajae ndani na hatimae kuzamisha mtumbwi wa CCM na kuwaangamiza wote waliomo. Hana analojua kuhusu CCM zaidi ya maslahi yake binafsi ya posho , marupurupu na kiinua mgongo cha Ubunge wake. Amekuta kila kitu kimetengenezwa,kuandaliwa na yeye kupewa tu Ubunge wa Bwelele .ndio maana hana uchungu kwa CCM,ndio maana yupo kazini muda wote kuihujumu CCM na kutaka kuivunja vunja na kuipasua vipande vipande.

Ndio sababu hana adabu wala heshima wala staha kwa viongozi wetu . Ndio sababu anaweza kuongea na kutamka neno lolote lile kuwachafua ,kuwatweza na kuwavunjia heshima viongozi wetu. Hajui maadili ya chama chetu wala miiko yake wala taratibu zetu wala miongozo ya chama chetu wala kanuni zetu. Yeye ni kukurupuka na kuropoka tu atakavyo. Kwanini? Kwa sababu huyu siyo wa kwetu na wala siyo mwenzetu. Huyu ni mamluki tu aliye na kazi maalumu ya kuibomoa CCM yetu.

Anasema atabakia ndani ya CCM kusudi aendelee kutumia mwamvuli wa CCM kuichafua ,kuivuruga na kuipasua atakavyo na kwa kadri ya maagizo apewayo na wanaomtumia na kumtuma. Sasa itakuwa ni Uwendawazimu na ukichaa mkubwa sana kuendelea kumuacha na kumkumbatia mtu wa aina hii ndani ya CCM yetu. kuendelea kumwaga petroli chini huku akiwa na kijinga cha moto mkononi Mwake kwa ajili ya kukiangamiza chama kwa kuripua moto.

Narudia kusema ya kuwa huyu mtu siyo mwana CCM bali alizolewa tu na kuvalishwa valishwa nguo ili afanane na sisi kwa nje lakini ndani ya moyo wake hajawahi kuwa mwana CCM na wala hajawahi kuipenda CCM. Yeye dua yake ni kuona CCM inakufa na kuangamia na kupotea kabisa katika uso wa Dunia na historia ya Taifa letu. Sasa wana CCM wenzangu ni lazima tufahamu ya kuwa ni bora Joka kubwa lililo nje ya nyumba kuliko nyoka aliye uvunguni Mwa kitanda maana huyo wakati wowote atajikunjua na kung'ata wote walio ndani ,atagonga wote na kuacha Simanzi tu ndani ya nyumba na kisha kutorokea Gizani.

Askofu Gwajima Tayari ni adui yetu ambaye tunapaswa kumtupa nje haraka sana iwezekanavyo pasipo kuchelewa. Ni vyema afanye chochote kile awezacho kupambana na sisi na kwa usaidizi wa mtu au kikundi chochote kile lakini akiwa nje ya chama chetu na huku sote tukijua huyu ni adui yetu. Kuliko ajifanye ni mwenzetu huku akitoboa mtumbwi wetu halafu tuendelee kukaa tu kimya kwa kusema mbona ni mwenzetu na tupo naye chomboni.

Bila kuchelewa wala kuwa na subira Gwajima atolewe haraka sana chamani ili huko ndiko sasa aanze vita yake sasa. Ni bora kupambana na akina heche au kupeana mikono na akina heche unayejua kabisa ni mpinzani wako kuliko kuacha glasi ya maji mezani alipokaa gwajima kwa kusema ni mwenzako. Utakuwa ni huna akili kabisa ukifanya hivyo na kuamini hivyo na kutokuchukua tahadhari.

Kuendelea kumuacha chamani itajenga picha na taswira mbaya sana,itakuwa mfano mbaya sana kwa wanachama wengine juu ya usimamizi wa maadili ya chama,italeta na kuchochea uasi ndani ya chama chetu na inaweza kuleta majaribio ya Mapinduzi na kuondoa kabisa amani ,utulivu ,umoja na mshikamano ndani ya CCM.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Kwa hiyo una uchungu na CCM kuliko wmaslahi ya wakulima na wafanyakazi ambao ndiyo Ile jembe na nyundo siyo?
Wakulima na wafanyakazi wanakula matunda tu kwa sasa. Rais Samia ameongeza bajeti ya kilimo mpaka trillioni 1.2 huku wafanya kazi wakiongezwa mishahara
 
Pole sana, amesema Tanzania kwanza, vyama na mambo mengine vinafuata. Mbona rahisi sana kuelewa?
 
Back
Top Bottom