Yafuatayo ni machache kati ya mengi ambayo CCM na serikali yake iliahidi 2005 kwa wananchi na imetimiza.
AHADI: KUENDELEA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA
Ujenzi wa miradi 15 ya barabara kwa kiwango cha lami yenye jumla ya urefu wa
Km. 1,398.6 imekamilishwa katika kipindi cha 2005 - 2010 huku ujenzi ambao
unaendelea ukiwa ni wa miradi 29 ya barabara zenye jumla ya Km. 2,536.4- Mkuu naomba tutofautishe barabara za Mkapa v/s za JK, kwani kwa Mkapa rekodi yake wote humu ndani tunaikubali tofautisha na JK. Hapa sitaenda mbali kwani nafanyia kazi hili.
AHADI: KUONGEZA BAJETI YA KILIMO NA KUKUZA SEKTA YA VIWANDA
Bajeti ya sekta ya kilimo imeongezeka kutoka asilimia 4.5 mwaka 2005
hadi asilimia 7.9 mwaka 2010 huku ukuaji wa sekta ya viwanda ukiongezeka kutoka asilimia 8.4 mwaka 2005 hadi asilimia 9.9 mwaka 2008.- Mkuu unaweza kunisaidia kulinganisha/kuoanisha ukuaji wa viwanda kwa miaka hii mitano na volume za export tulizouza na effect iliyokuja katika uchumu; maana figure ulizotoa si haba. Natumaini wote humu ndani tutafurahi kukiwa na uhusiano wa mambo haya isje ikawa tuna figure zisizo na uwiano katika ukuaji wa uchumi wetu.
Idadi ya wakulima wanaopata mbolea ya ruzuku imeongezeka kutoka wakulima 750,000 mwaka 2005/2006 hadi 2,076,710 mwaka 2009/2010 huku bajeti ya ruzuku ya pembejeo ikiongezeka kutoka bilioni 7.5 hadi bilioni 101.4 katika kipindi hicho cha miaka mitano.- Vipi kuhusu controls kuhakikisha ruzuku tuliyotoa katika mbolea imefika kwa walengwa? Wote humu ndani tutakumbuka jinsi ambavyo vocha za takribani bilioni 26 zilivyopotea Rukwa, zikamuingiza matatani mkuu wa mkoa aliyekataa kujiuzuru, ati anasubiri muungwana ndo aamue. Ukweli ni kuwa hizi figure zote ni za kisiasa; hazina msaada wowote kwa wakulima, naamini utakubaliana na mimi kuwa zile vocha chanzo cha kupotea ni bei kubwa mkulima anayotakiwa kulipa; matokeo yake walalnguzi wanazinunua na kuziuza malawi na DRC, to name few!!!
Idadi ya wataalamu wa ugani walioajiriwa katika halmashauri imeongezeka kutoka wataalamu 3,379 mwaka 2007/2008 hadi 4,439 mwaka 2009/2010.- No comment
AHADI: KUKUZA NA KUBORESHA SEKTA YA ELIMU
Wanafunzi wanaojiunga na vyuo vikuu vilivyopo nchini Tanzania waliongezeka kutoka 55,296 mwaka 2005/2006 hadi 118,000mwaka 2009/2010.- Mkuu nakubaliana na figures, lakini vipi uhalisia; hizi figures zimepandishwa kisiasa, hata hao wa UDOM, najua una habari kuwa mwaka huu imebidi UDOM ichukue wananfunzi wachache maana miundombinu chuoni bado haijakamilika, kuna tatizo kubwa la sewerage handling!!! Chuo kimeanza kazi wakati bado muda!!! Ukweli ni kuwa mlianza mapema ili tu kutuletea idadi isiyo kwani mnajua ni rahisis kuwahadaa waTZ
Idadi ya vyuo vikuu imeongezeka kutoka vyuo vikuu 23 mwaka 2005 hadi kufikia vyuo 31 mwaka 2010.
Kuweza kujenga chuo kikuu cha Dodoma chenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 40,000 kwa mwaka na kwa sasa kina wanafunzi 17,282- Rubbish chuo bado hakiko sawa, achilia mbali walimu, UDOM inahaha hadi leo kutafuta walimu, hakukuwa na mkakati wa kujiandaa kutoa walimu watakaofundisha huko, as a result wakati kinaanza kikakumbwa na kashfa ya kuajiri walimu wenye degree feki!!!
Wanafunzi wanaomaliza elimu ya msingi na kuendelea na elimu ya sekondari wameongezeka kutoka 493,636 hadi 999,070 huku idadi ya wanafunzi wanaogharamiwa na serikali toka familia zenye kipato duni ikiongezeka toka 16,345 hadi 58,843. Ongezeko hili ni kati ya mwaka 2005 hadi mwaka 2009.- Imekaa kisiasa zaidi mkuu; imebainika zaidi ya nusu ya wanafunzi wanaomaliza elimu ya msingi hawawezi kuandika na kusoma vizuri, sasa hii idadi itatupeleka wapi? Nyinyi mnapima mafanikio yenu kwa idadi tu!!! Ubora kwenu mwiko!!! Hii nayo haina maana mkuu, tunataka kama ni wanafunzi wa shule za msingi watoke wakiwa na uwezo!! Sekondari ndo usiseme!! Wanafunzi wetu wa kata bure kabisa, shule hizo ni sawa na hakuna kabisa wote tunajua, need i say more!!!
]