Elections 2010 CCM ina rekodi ya utekelezaji 2005 - 2010

Recruitment ya troops wapya imeanza kusuasua, sasa wameaamua ku-deploy reserves na retirees!!! lol

Steve Dii
Let's go man, substitute anatakiwa awe bora zaidi ya aliyetangulia. Hata hivyo ni vema tukakutana na kujadili hatima ya nchi yetu kama wazalendo. inafurahisha kuona kuwa we discuss kwa kuheshimiana na contructively.
 
Masikini wameongezeka kwa kasi zaidi, mishahara na marupurupu ya viongozi wa serikali imeongezeka kwa ari zaidi, mfumuko wa bei umekuwa kwa nguvu zaidi

tempo_user1
Inawezekana una hoja nzuri lakini unasahau kuwa bila ya evidence kwa maana ya takwimu hoja yako inakuwa ni kishabiki tu, haina nguvu. Thibitisha madai yako ili tuwe na upana mkubwa wa kujadili.

Kwa mfano lete takwimu mbadala kwa kukata hia zangu hapo juu.
 
Hakuna taifa lililowahi kuendelea duniani kwa kuwekeza zaidi katika masuala ya jamii badala ya yale ya kiuchumi...
 
Hakuna taifa lililowahi kuendelea duniani kwa kuwekeza zaidi katika masuala ya jamii badala ya yale ya kiuchumi...

Safari you are making a great mistake in your analysis.

Hebu tuangalie undani wa South Korea (investment in education was the main force behind their success).The problem with many opposition members today in Tanzania is:

They want us not to accept the fact that economic growth (which has been greatly achieved in the past 15 years) is a prerequisite to economic development (the stage that we are moving in). This is where the whole argument is.
 

Wenye uwezo wa kufikiri kama wewe ndo mnaipeleka nchi pabaya. CCM inapaswa kueleza kipindi chote ilipo kuwa madarakani imefanya nini na si kutoa ahadi. wanaopaswa kutoa ahadi ni wale ambao hawajaingia madarakani. Ukiona mnang'ang'ania ahadi, ujue mambo yamewashinda!!!!!!
 

Nyange,
Hata kama basi ulitakakutoa mtazamo hasi dhidi ya CCM, basi ungesoma nilichokiandika na ukaelewa.

Hivi ni kweli umeshindwa kuelewa kuwa swali lako majibu yake ndiyo hayo niliyoweka hapo mwanzo.

Inasikitisha kuwa unavaa ushabiki huku ukiwa haupo makini.

Soma vizuri tena maelezo yangu na utatambua kuwa kiu yako ya maendeleo tayari ilikwisha kidhiwa na CCM katika miaka 5 iliyopita.
 
Rekodi ya Utendaji na Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM

1. Ujenzi wa barabara zilizoahidiwa mwaka 2005 umekamilka zikiwemo, Manyoni -Dodoma, Manyoni -Singida, na Mkurang -kibiti
2. Tumejenga vivuko vya uhakika kigamboni, MV Misungwi, MV Pangani, MV Kome
3. Tumejenga kiwanja cha ndege kipya cha Mbeya (Songwe) na tumeendelea kuimarisha viwanja vitano vya ndege (JNIA, Arusha, Mwanza, Kigoma na Mafia)
4. Tumejenga madaraja makubwa nchini kama lile la Mpiji, mchakato umeanza wa daraja la kigamboni Dar es salaam, Daraja la Kilombero mkoani Morogoro, usanifu wa daraja jipya la Ruvu na ujenzi wa daraja la umoja baina ya Tanzania na Msumbiji.
5. Tuliahidi kuanza ujenzi wa barabara mpya kwa kiwango cha lami kama ifuatavyo:
Barabara ya Tunduma –Sumbawanga ujenzi umeanza
Marangu-Tarakea-Songao ujenzi umekamilika
Minjigu-Babati-Singida – ujenzi unaendelea
Mbeya-Chunya-Makongolosi – ujenzi unaendelea
Arusha-Namanga – ujenzi unaendelea
Tanga-Horohoro –ujenzi unaendelea
Ukarabati za Barabara za Kilwa, Sam Nujoma na Nelson Mandela ama umekamilika ama unakaribia kukamilika

Malengo kwa kipindi cha 2010 - 2015

  1. Kwa kushirikiana na Halmashauri za Wilaya na Miji, kukamilisha kazi ya upimaji wa mipaka ya vijiji vipya na kupanga mpango wa matumizi bora ya ardhi. Vile vile kuwahamasisha wananchi kuchangia upimaji wa mashamba yao na kuwapatia hatimiliki za kimila, pamoja na kujenga masjala za ardhi katika ngazi za Wilaya na Vijiji.
  2. Kutekeleza Mpango wa Taifa wa Matumizi ya Ardhi wenye program 12 ambazo ni programu ya kuimarisha TUME, Kilimo, Mifugo, Uvuvi, Misitu, Wanyamapori, Madini, Nishati, Miundombinu, Rasilimali maji, Utalii na Uwanda/Uoto Asili kwa lengo la kukamilisha kazi ya upangaji wa matumizi bora ya ardhi nchini.
  3. Kushirikisha Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi (NHBRA) katika kufanya tafiti mbali mbali za vifaa vya ujenzi wa nyumba bora kwa teknolojia rahisi na gharama nafuu na kufikisha matokeo ya utafiti huo kwa wananchi.
  4. Kuhakikisha kuwa jumla ya nyumba 15,000 (kwa wastani nyumba 3,000 kila mwaka) zinajengwa na Shirika la Taifa la Nyumba (NHC) kwa kushirikiana na sekta binafsi.
  5. Kuboresha mazingira ya upatikanaji wa mikopo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba kwa masharti nafuu, kuwahamasisha wananchi kuzielewa Sheria ili wazitumie kupata mikopo ya muda mrefu kwa ajili ya kujenga au kununua nyumba na kuhamasisha mabenki na vyombo vingine vya fedha kutoa mikopo ya ujenzi wa nyumba ya muda mrefu na yenye riba nafuu.
  6. Kuandaa na kusimamia utekelezaji wa programu ya Taifa ya Kurasimisha Makaazi nchini. Programu hii itakuwa dira ya kuboresha makaazi na kukabiliana na tatizo la ujenzi holela nchini. Aidha, Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine itaendeleza kasi ya Urasimishaji wa ardhi na nyumba katika Majiji na Hamashauri za Miji na Wilaya na kutoa leseni za makazi.
  7. Kutekeleza mradi kabambe wa kuweka kituo cha kupokea picha za Satellite (Satellite Imagery Receiving Station) kitakachorahisisha upimaji wa ardhi yote nchini na pia kitarahisisha utayarishaji wa ramani kwa ajili ya matumizi mbalimbali.
 
Tunaomba na takwimu ya fedha zilizoibiwa kwa kipindi cha miaka 15 iliyopita.fedha zilizopotea kutokana na mikataba mibovu nchi iliyoingia.kiasi gani kimepotea kutokana matamuzi mabaya serikali kuu na halmashauri zetu.
 
Tunaomba na takwimu ya fedha zilizoibiwa kwa kipindi cha miaka 15 iliyopita.fedha zilizopotea kutokana na mikataba mibovu nchi iliyoingia.kiasi gani kimepotea kutokana matamuzi mabaya serikali kuu na halmashauri zetu.

Muonamambo,

Ahsante sana kwa swali lako.


Kwa vile hii thread inaongelea utekelezaji wa yale yaliyoahidiwa CCM na pia kuonesha dira yake ya mwelekeo wa 2010 - 2015.

Ninakushauri hizo takwimu za fedha ngapi zilizoibiwa kaulize kutoka jeshi la Polisi au kwa DPP (mwendesha mashtaka wa serikali) kwani huko ndiyo mahali pake.
Na kama unataka kujua matumizi mabaya ya fedha za serikali na halmashauri zake ninakushauri utafute ripoti Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) uisome na kama huelewi wasiliana nao.


Nadhani nimekuelekeza vizuri jinsi ya kupata taarifa unazoziuliza.
 
AHADI: KUENDELEA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA











Ujenzi wa miradi 15 ya barabara kwa kiwango cha lami yenye jumla ya urefu wa
Km. 1,398.6 imekamilishwa katika kipindi cha 2005 - 2010 huku ujenzi ambao
unaendelea ukiwa ni wa miradi 29 ya barabara zenye jumla ya Km. 2,536.4



 
kaka kama ulivyosema kuwa utasema kweli daima fitina kwako mwiko. pia naamini kwamba takwimu ulizoorodhesha hapo juu umefanya jitihadg kuzipata ili kufikisha lengo lako kwamba ccm imefanya vyema. basi ni vyema utupatie pia takwimu ya fedha zilizoibiwa kutokana na utawala mbovu,mikataba mibovu.sera mbovu na matumizi yasio na maslahi kama safari za nje za jk.magari ya kifahali na mengineo bila kusahau zile zilizopotea kwenye halmashauri zetu?.jibu swali kaka kama fitina kwako mwiko.
 

Vipi kuhusu Ufisadi??

Mbona unazunguka mbuyu?

Hizo porojo tulishaziskia sana.
 
Uzuri wa rekodi, siyo lazima iwe nzuri... hivyo pundamilia nakupongeza sana kwa kuleta hiyo rekodi ambayo kwangu naiona ni mbaya hasa ukizingati yafuatayo
Miundombinu iliyoboreshwa niile iliyokua kwenye mpango before na ukuaji wake hauendani na ukuaji wa mahitaji
Kwenye kilimo naona mmenufaisha zaidi akina manji na wenzake kiasi cha kutoa agizo la power tiller hata kwenye milima na mabonde kama lushoto
Kwenye elimu mmesaidia sana kuongeza shule za kata na hivyo kufanya baadhi ya makabila kudumaa kielimu mojakwamoja --- kata nyingi za vijijini hazina walimu hivyo basi hakuna kitakachotoka: garbage in, garbage out!!
kwenye afya sisi ndio wa mwisho kwa ubora wa huduma ya mama na mtoto na tunaongoza (EAF) kwa vifo vya akina mama na watoto, hatuna maabara, hatuna good supply system na tunaongoza kwa kukosa wataalam
Kwenye maji sisemi sana maana nilimuona rais wangu mpendwa akimtwisha ndoo bibi wa watu
Kwenye JINSIA NAUNGA MKONO
 

Wote (lakini sina uhakika) tunaelewa kuwa maendeleo au mafanikio upimwa kwa kuzingatia malengo. Mfano, Millennium Development goals waliweka lengo, mfano, kupunguza umaskini kwa nusu kuanzia mwaka 2000 mpaka 2015. Malengo yao yamekuwa na muda, yanapimika, specific, na realistic. Ningependa kuona hayo mafanikio uliyoweka hapo juu yawe na malengo yake, halafu utuonyeshe mafanikio ili tuweze kuyapima. Je, mfano malengo ya miradi ya barabara ilikuwa 15 au 29 au 15+29? Au ndio tunakwenda bila hata kupanga?

Je, tukitumia 'barometer' nyingine ambayo ni Millennium Development Goals (MDGs), CCM imefanya nini kwani hata nusu ya malengo kuanzia mwaka 2000 hayajafikiwa? Je, kufikia 2015 tutafikia malengo hayo?
 
Pundamilia07,
JK na CCM kwa ujumla imepoteza imani toka kwa mwananchi kwa kushindwa kushughulikia kero muhimu za wananchi kwa muda ambao amekuwa Ikulu, pia tabia ya kutosema ukweli ndicho hasa chanzo cha wananchi wengi tutomuamini tena huyu kiongozi wetu na CCM kwa ujumla. Ningependa kupata majibu yafuatayo toka kwake kama mgombea URAIS kupitia CHAMA TAWALA:-
a) Kagoda ni nani? Nani aliasisi wizi wa pesa pale BOT? Kwa nini mpaka sasa hajafikiswa
katika vyombo vya sheria?

b) Richmond ni nani? Na ni kina nani walibariki mkataba huu wa ulaghai? kwa nini hajakamatwa na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria mpaka sasa? Niambie nani alihusika na uchotaji wa pesa za serikali toka makampuni ya Melemeta, Mwananchi Gold?

c) Nani hasa alihusika na kusign mkataba wa kununua RADA ya taifa? kwa nini hajakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria?

d) Nani alishiriki kuuwa mashirika yetu ya Umma kwa kuingia mikataba mibovu? ATC, RELI n.k na kwa nini Kwa nini Chama hakijachukua hatua kupitia mikataba yote ya madini na mali asili za nchi yetu kwani mikataba hii imeonekana na uwalakini mwingi tu?

e) Je unaridhika kwamba kauli mbiu ya KILIMO KWANZA kimekidhi haja kwa wananchi kuelekea mapinduzi ya kilimo cha kisasa?

f) Je Priorities za Chama chenu ni zipi? ELIMU bado duni , AFYA mbovu na MAKAZI ya mwananchi yanatisha.

g) Je unaridhika na matumizi ya fedha zetu za umma? serikali yetu inatumia ipasavyo? Je bajeti ya serikali kila mwaka inamfikia mlengwa au inaishia huko huko juu kwa wenyewe?

h) CCM haina sera nzuri ya ardhi na ndiyo maana wafugaji na wananchi walio karibu na migodi wanavyo nyanyaswa

i) Chama hakina Sera nzuri juu ya walemavu kwa ujumla, wazee (Senior citizens) watoto na kina mama wajawazito.

j) Nini hasa chanzo za umasikini wa watanzania? Madini tuyao kibao, Mali asili na utalii kwa wingi, nini tatizo hapa?


Haya ndiyo baadhi ya mambo wanataka kusikia majibu yake na ni action gani Mkuu wetu alichukua kipindi cha utawala wake hapo IKULU.
 

Acid hapo umesema kweli kwasababu wengine ni mafundi wa kuchakachua mambo. kila kinachofanyika wenzetu wanatuambia ni utekelezaji wa ilani. Vitu vingine vilianza hata kabla ya awamu husika lakini wanadai wametekeleza. Kitu cha ajabu ni kuwa utekelezaji wa ufisadi walioutekeleza wanaukana kuwa siyo wa kwao. Watuambie mfumuko wa bei ulikuwaje?
 


Nimehajribu kukujibu mkuu Pundamilia kama inavyoonekana in red. Ukweli ni kwamba hakuna jipya, mmekosa ubunifu katika kendesha serikali si mbaya mkaona na wenzenu watafanya nini, step down fellas!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…