Elections 2010 CCM ina rekodi ya utekelezaji 2005 - 2010



PUNDAMILIA JF NI BODI YA GREAT THINKERS NA SIO WATU WA BLAH BLAH TUU,
NI AIBU KWA VIONGOZI WA CCM KUJISIFA KWA UANDIKISHAJI WA WATOTO WASHULENI NA KATIKA VYUO ILIHALI ELIMU INYOTOLEWA HUKO SI YA KURIDHISHA HATA KIDOGO.
KILA MTANZANIA ANAKUMBUKA KUWA SERIKALI YA CCM ILITUMIA RASLIMALI NYINGI KUTAYARISHA MPANGO YA KUPUNGUZA NA KUONDOA UMASKINI TANZANIA UJULIKANAO KAMA MKUKUTA NA BAADYE MALENGO NA SHABAHA ZAKE VIKAINGIZWA KATIKA ILANI YA CCM YA 2005 HADI 2010.
HIVYO TUNAPOTAKA KUPIMA UTEKELEZAJI WA SERIKALI YA CCM, TUNAFANYA HIVYO KWA KULINGANISHA RASLIMALI ZILZOKUWA CHINI YA USIMAMIZI WA SERIKALI YA CCM NA KIWANGO CHA MAFANIKIO KILICHOPATIKANA KATIKA MALENGO AMBAYO SERIKALI HIYO ILKUWA IMEJIWEKEA YENYEWE.
UTAKUBALIANA NA MIMI KUWA UJENZI WA MADARASA ULIFANIKISHWA KWA KIWANGO KIKUBWA NA RASLI MALI ZILIZOCHANGWA NA KUSIMAMIWA NA WANANCHI WENYEWE KUJENGA MADARASA YA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI ZA KATA. HATA HIVYO ULIKUWEPO UFISADI MWINGI KUTOKA KWA WENYEVITI NA WATENDAJI WA MITAA, VIJIJI NA KATA IKIASHIRIA MAPUNGUFU MAKUBWA YA SERIKALI YA CCM KATIKA NYANJA YA USIMAMIZI WA RASLI MALI ZA TAIFA
Table 1 Summary of broad clusters, broad outcomes and goals of the National Strategy for Growth and Reduction
of Poverty
The operational targets (see Table 2) established in the NSGRP address early childhood development,
increased enrolment, and opportunities for children with disabilities, improved learning environment
and access to and quality of education, adult education, and improvement and expansion of vocational
and higher education.
A. Early Childhood
o Increase in the number of young children prepared for school and life
B. Primary Enrolment
o Increased gross and net enrolment of boys and girls, including children with disabilities in primary schools from
90.5% in 2004 to 99% in 2010
o Increased proportion of orphans and other vulnerable children enrolled, attending and completing primary
education from 2% in 2000 to 30% in 2010
C. Secondary Enrolment
o Increased percentage of girls and boys with disabilities and OVCs who qualify for secondary education enrol and
complete secondary schools by 2010
o At least 50% of boys and girls aged 14 -17 years are enrolled in ordinary level secondary schools by 2010
o At least 60% of girls and boys pass Standard VI I examinations by 2010
o At least 25% of boys and girls are enrolled in advance level secondary schools by 2010
D. Primary Achievement & Quality
o Achieving an average daily attendance in primary schools of at least 85%
o At least 95% of cohort complete standard IV
o At least 90% of cohort completes standard VII.
E. Secondary Achievement & Quality
o At least 70% of girls and boys pass at Division I -III in Form IV examinations.
o Improved learning environment for all children in all schools, with all education institutions safe, violence free,
child friendly and gender sensitive
o Access to and quality of education in GoT and Non -Government schools regulated.
o 90% of primary and secondary schools have adequate, competent and skilled teachers by 2010.
o Primary and secondary education is of a high quality and promotes the acquisition of critical knowledge, real
skills and progressive values.
F. Higher & Technical Education
o Increased enrolment in higher and technical education in Universities and in Technical Colleges to 30,000 full
time students, 10,000 part time, and 15,000 distance learners by 2008.
o Improved knowledge on entrepreneurship skills amongst youth
5
G. HIV/AIDS
o Effective HIV and AIDS education and life skills programmes offered in all primary, secondary schools and
teachers colleges.
H. Adult & Non-Formal Education, & Culture
o At least 80% of adults, especially women in rural areas, are literate.
o Reduced number of illiterate adults from 3.8 million (2004/05) to 1.5 million (2007/08).
o Reduced numbers of young people involved in COBET from 234,000 in 2004/5 to 70,566 in 2007/08
o Expanded and improved public participation in cultural activities.
o Increased numbers of students/youth who are service orientated.

BADALA YA VIONGOZI NA WAPIGA DEBE WA CCM KUJISIFIA MAFANIKIO YALIYOPATIOKANA KUTOKANA NA WANANCHI KUFANIKIWA KUSIMAMIA RASLI MALI ZAO WENYEWE. CCM INATAKIWA KUTUELEZA KUWA IMEFANYA NINI NA RASLIMALI ZILIZOLKUWA CHINI YAKE IKIWEMO KODI ZINAZOKUSANYWA, FEDHA ZITOKANAZO NA MADINI, MBUGA ZA WANYAMA, VIVUTIO VYA UTALII, MISAADA, MAUZO YA NJE N.K IKILINGANISHWA NA MALENGO YALIYOKO KATIKA MKUKUTA NA SI VINGINEVYO

KAMA TUNAVYOONA HAPO JUU, KATIKA MALENGO YA MKUKUTA NA ILANI YA CCM YA 2005, SERIKALI YA CCM ILIAHIDI KUWA KUFIKIA 2010, 70% YA WASICHANA NA WAVULANA WA SEKONDARI WANAFAULU MITIHANI KWA KIWANGO CHA DIVISHENI I HADI III- MATOKEO YAKE ILI KUFICHA AIBU YA UKOSEFU WA WAALIMU NA VIFAA VYA KUFUNDISHIA- BILA AIBU WALA SONI VIONGOZI WA SERIKALI YA CCM WAKAFUTA MITIHANI YA MAJARIBIO YA KIDATO CHA PILI; KWA NIA YA 0KUFICHA UDHAIFU WA SEKONDARI ZA KATA IKILINGANISHWA NA SHULE BINAFSI. JE KUFUTA MITIHANI YA MAJARIBIO NDIO KUTOA ELIMU BORA?

HIVI HUKO VIONGOZI WA CCM WANAPOPELEKA WATOTO WAO KUSOMA KATIKA SHULE ZA MSINGI, SEKONDARI ZA BINAFSI, VYUO NA KATIKA NCHI ZA KENYA, UGANDA, AFRIKA KUSINI, MALAYSIA, INDIA N.K HAKUNA MITIHANI YA MAJARIBIO?

KAMA MITIHANI YA MAJARIBIO IPO, NI KWANINI SERIKALI YA CCM INAWACHEZEA WATOTO WA KITANZANIA? NDIO MAANA TUNATAKA IONDOKE MADARAKANI ILI KUWANUSURU WATOTO WA WAKULIMA NA WAFANYAKAZI WA TANAZANIA KIELIMU.

-ILIAHIDI KUFIKIA 2010, MAZINGIRA YA KUSOMEA KATIKA SEKONDARI ZOTE YATABORESHWA KIUSALAMA-NI WASICHANA WANGAPI WANAJAZWA MIMBA KUTOKANA NA SERIKALI KUSHINDWA KUWAWEKEA MABWENI NA KUWAPATIA MAHITAJI MUHIMU YA KIELIMU NA MAZINGIRA MAZURI YA KUSOMEA? NANI ANAPASWA KUBEBA LAWAMA KWA KUHARIBIKIWA MAISHA WATOTO WA KIKE?

-ILIAHIDI KUFIKIA 2010, UBORA WA ELIMU KATIKA SHULE ZA SERIKALI NA MASHIRIKA MENGINE UTASIMAMIWA VIZURI-JE HILO LINAFANYIKA KWA WANAFUZI 600 KUWEKEWA WAALIMU 3 TU?

-ILIAHIDI KUFIKIA 2010, 90% YA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI ZITAKUWA NA WAALIMU WENYE TAALAMU NA UJUZI WA KUTOSHA KUFUNDISHA-JE HILO LIMEFANYIKA.

ILIAHIDI KUWA ELIMU ITAKAYOITOLEWA KATI SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI ITAKUWA NI YA KIWANGO CHA JUU NA INAYOKUZA UFAHAMU WA KUWEZA KUJIENDELEZA- JE ELIMU INAYOTOLEWA KATIKA VODA FASTA IKO HIVYO.

KAMA SERIKALI YA CCM IMESHINDWA KUTIMIZA HATA 50% YA MALENGO YA MKUKUTA ILIYOJIPANGIA YENYEWE KUFIKIA 2010 KATIKA SEKTA HII MOJA, UNAFIKIRI KATIKA SEKTA ZINGINE HALI IKOJE?

NDIO MAANA VIONGOZI WA CCM WANAJIVUNIA UANDIKISHAJI WATOTO MASHULENI NA VYUONI TU KWA KUWA HUKO WANANCHI WENYEWE AU WAMILIKI WA SHULE NA VYUO WALISIMAMIA RASLI MALI ZILIZOHUSIKA KULETA MAFANBIKIO YA UJENZI WA MADARASA, SHULE NA VYUO

TUPENI MAJIBU YA RASLIMALI ZILIZOKUWA CHINI YA SERIKALI YA CCM KUPITIA KODI MBALI MBALI, MADINI, VITUTIO VYA UTALII, MAUZO YA NJE, MISAADA N.K SIO KULETA BLAH BLAH TUPU.

TUNATAKA CCM IONDOKE MADARAKANI ILI VIPAUMBELE VYA TAIFA HILI VIPANGWE UPYA KWA MUJIBU WA MAHITAJI YENYE TIJA.

UBORA WA ELIMU UTATOKA WAPI KATIKA HALI YA WALIMU KULIPWA MISHAHARA DUNI, HIVI SASA MWALIMU WA SEKONDARI ANALIPWA SHILINGI 250,000/= KWA MWEZI ILIHALI MBUNGE AMBAYE HANA TIJA YOYOTE KWA TAIFA HILI ANALIPWA MILIONI 7,5 KWA MWEZI.HII NI KWA MUJIBU WA TAKWIMU KUTOKA KWA SPIKA SAMUEL SITTA (MSHAHARA NA MARUPURUPU). KWA MANTIKI HII SERIKALI YA CCM INAMLIPA MBUNGE MMOJA MISHAHARA YA WAALIMU 30, SASA ELIMU BORA ITATOKA WAPI KATIKA MAZINGIRA YA AINA HII?.

ENDAPO MISHAHARA NA MARUPURUPU YA WABUNGE VITAPUNGUZWA KUFIKIA MILIONI 2,500,000/= (SAWA NA MISHAHARA YA WAALIMU 10) KIASI CHA SHILINGI MILIONI 5 x MIEZI 12 x WABUNGE 323=BILIONI 19,380,000,000 ZITAOKOLEWA KILA MWAKA.

IKIWA POSHO ZA VIKAO NAZO ZITAPUNGUZWA KWA 50%; KWA SIKU 90 KATIKA MWAKA,SHS 50,000 x 90 x 323 =BILIONI 1,453,500,000 ZITAWEZA KUOKOLEWA. UKIZIDISHA NA 19,380,000,000 ZA HAPO JUU UTAPATA NI BILIONI 20,833,500,000 ZITAWEZA KUOKOLEWA KWA MWAKA KUTOKA KWA WABUNGE WASIO NATIJA YOYOTE KWA TAIFA HILI, SANA SANA KUCHAPA USINGIZI BUNGENI .

KWA KUWA WAKUU WA MIKOA NA WILAYA NAO PIA HAWANA MCHANGO WOWOTE KWA UCHUMI NA MMAENDELEO YA TANZANIA. WAKURUGENZI, MAMEYA NA MADIWANI WA HALMSHAURI ZA MIJI NA WILAYA WANATOSHA KABISA KUSIMAMIA MAENDELEO KATIKA MAENEO YAO KAMA ILIVYOTOKEA NCHINI KENYA BAADA YA KUPITISHWA KWA KATIBA MPYA.

NAFASI HIZO HUTUMIKA KAMA VYEO VYA HISANI KWA MAKADA WA CCM WASIOTAKA KUJITUMA KATIKA KILIMO AU UJASIRIMALI. IKIWA WAKUU WA MIKOA 26 NA WA WILYA 127 WATAONDOLEWA KIASI CHA FEDHA KITAKACHOKOLEWA NI TAKRIBANI MILIONI 5 (MISHAHARA NA MARUPURUPU KWA MWEZI) MILIONI 5 x MIEZI 12 x WILAYA 153= BILIONI 9,180,000,000/= KWA MWAKA.

FEDHA ZINAZOWEZA KUOKOLEWA KATIKA VYANZO HIVI VIWILI NI BILIONI 30,013,500,000/= ZINATOSHA KUWALIPA MISHAHARA WAALIMU 120,054 WAPYA ILI KUBORESHA ELIMU HAPA NCHINI.

KIASI HICHO PIA NI 12% YA SHILINGI BILIONI 260 JAKAYA KIKWETE ANAZOAHIDI KATIKA KAMPENNI HIZI ZA 2010 KUZIPATA KUTOKA KWA WAMAREKANI KWA AJILI YA KUJENGA NYUMBA ZA WAALIMU KATIKA SHULE ZETU KANA KWAMBA WATANZANIA HATUNA VYANZO VYETU VYA NDANI?.
 
View attachment 14345

I can't wai to move to Kigoma (the New Dubai). Kigoma katika picha 2015!!!!




KIGOMA by 2015!!!! Mwenzenu nisha tafuta kashamba huko, nyie bado mnahangaikia ya Bagamoyo na Mkuranga??

CCM ina rekodi ya utekelezaji!!! Ahadi ya kuifanya Kigoma Dubai ya TZ si utani!!! Kama huamini subiri 2015!!
 


Hongera kwa kuwa na 'courage kama ya mwendawazimu! ama ya kifisadi. Hivi hii barabara ya Tunduma Sumbawanga ndio ile inayogharimiwa na MCC? Nayo imo kwenye ilani ya CCM?
Just wanted to know Pundamilia
 


Haya tulikwisha yazoea, mwaka 2005, JK aliahidi kuifanya Mwanza California ya Africa. Leo ni 2010 hata mipango ya michakato ya kubadili mwanza ni ndoto!!!

Hakuna jipya CCM, period.
 

mkuu hakuna cha kujivunia katika ujenzi wa barabara nilizowekea rangi nyekundu. Badala ya serikali kuimarisha mfumo wa reli ili iweze kuvuta mizigo mingi kwa mara moja imewekeza fedha watanzania walizokusanya kama road tool fund katika ujenzi wa barabara. Kipaumbele hiki kilikuwa na kasoro kubwa, ccm ilichozingatia na maslahi ya viongozi na wabia wao wa kibiashara ya usafirishaji wanaomiliki wanamiliki maelfu ya malori ya mizigo ya kusafirisha bidhaa kwenda mikoani na nje ya nchi.

hivyo kabla barabara hizi kuwaletea watanzania maendeleo endelevu, maelfu ya malori yanayotumia barabara hizo tena katika mazingira ya ccm kushindwa kudhibiti rushwa iliyotapakaa na kuruhusu malori yanayozidisha uzito kuendelea na safari, barabara zote hizi zitaharibiwa na malori ya vigogo wa ccm na kuturudisha watanzania wote tulikotoka. Mingi ya mizigo inayosafirishwa katika barabara hizi ilipaswa kuvutwa na mabehewa ya treni hadi vituo fulani fulani na idadi ndogo ya malori kutumika kubeba mizigo hiyo katia ya reli na wananchi na wananchi na reli zilzipo. unakumbuka kampuni ya kenatco ya kenya ilivyovunja barabara zetu miaka ya sabini au unaleta ushabiki tuu?

hapo ndio tunafikia katika ufisadi mkwingie mkubwa wa viongozi wa ccm kuua shirika la reli la tanzania, mwaka 2005 kikwete aliposhaki madaraka alikuta mchakato wa kubinafsisha trc ukiwa katika hatua za juu kabisa. Alisimamisha machakato huo, na kutuletea wahindi wa trl na rites. Hii ni hujuma

ujenzi wa barabara nilizoweka rangi ya bluu ni ufisadi mtupu kwa kuwa eneo hilo tayari likuwa na barabara za lami za kutosha lakiniu kwa ufisadi wa mramba akajenga barabara ingine ya lami huko.

ujenzi wa barabara niliyoweka rangi ya njano ni yaani barabara ya kilwa ni wa kiwango cha chini kiasi kwamba hata kiwete alikiri kuwa serikali yake imeshindwa kusimamaia raslimalki zilizotumika kwa barabara hiyo alipokuwa kwenye kampeni huko temeke.

kimsingi bado haujajibu hoja za msingi kuwa ni kiwango gani cha raslimali kinatumika katika miradi hii na nini inakuwa matokeo yake.

kama raslimali za taifa zinatumika vizuri mbana idadi ya maghorofa na magari ya kifahari ya viongozi wa ccm na watendaji wa serikali ya ccm vinaongezeka kwa kasi kubwa wakati hali za wananchi wanyonge zinazidi kuwa tete?

hata mwalimu nyerere aliwahi kuuuliza mali hizi mnapata wapi?
 

washabiki wa ccm wakati ninyi mnahangaika na ahadi hewa na kigoma kuwa dubai ya afrika na kutupatia takwimu kibao za kutulaghai. Uhalisia wa mamabo hapa nchini, leo tar 28/9 radio clouds wametangaza kuna mtoto wa kike miaka 12 kapotea yuko kituo cha polisi magomeni, ana wiki tu tokea awasili hapa jijini kutokea chimbereng'ende, nachingwea, baada ya mama yake kamuaichisha shule ya msingi na kumtoa aje kutumikishwa hapa mjini baada ya kushindwa kumlipia michango ya shule, kumnunulia sare za shule na kumpatia riziki. Habari kama hizi hutangazwa anagalau mara tau au nne kwa mwezi, sasa hiyo maisha bora yako wapi?
 

At least that is some proof of practicality, the others are still in the drawing board NO ONE KNOWS their solutions can be feasible or NOT. It is a 50% / 50% chance. Are we ready to give it a try?. 5 years lost can be disastrous for a poor country like ours cause there is still a chance to loose!!. All that said TZ still needs strong opposition to achieve higher than that.
 
Kutoka mwaka 2005 hadi 2009,jumla ya zahanati 464,vituo vya afya 98 na nyumba za waganga 394 zilijengwa. Zahanati 1,037 vituo vya afya 285 na hospitali 112 zimekarabatiwa.

Kujenga/ kuongozeka zahani pekee hatusaidii chochote, ungesema na wauguzi/ madaktari/manesi nk wangapi wamesomesha ndo ingeleta maana. Haya ndo yale yale unajenga shule bila kuwa na mkakati wa kuongeza walimu. CCM kuweni makini kabla hamjafanya jambo muwe mnaweka mikakati ya kujua ni vipi mtaitekeleza,



 
Unajua twakimu ehhe? Pesa za EPA ni kiasi gani? Pesa za Richmond, pesa Kikwete aliyotumia katika safari zake nje ya nchi? Toa upumbavu, toa ccm!
 

MWANANCHI
Serikali inachangia wanafunzi kutojua kusoma na kuhesabu
Monday, 27 September 2010 20:45

Na Fredy Azzah
WIKI iliyopita,Tanzania ilipewa tuzo ya kimataifa, kwa kutekeleza vizuri malengo ya elimu ambayo ni sehemu ya Malengo ya Maendeleo ya Milenia ya (MDGs), yanayotakiwa kukamilika mwaka 2015.Tuzo hiyo ilipokewa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwenye sherehe ya tuzo ya utekelezaji wa malengo ya milenia 2010, iliyofanyika nchini Marekani.



Akipokea tuzo hiyo, Pinda alisema imeipa moyo Tanzania iongeze bidii ili ifanikiwe katika malengo yote ya milenia ifikapo mwaka 2015.

kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa na vyombo vya habari kuhusu tuzo hiyo, Tanzania imefanya vizuri katika lengo la elimu kwa kuhakikisha watoto wote wanaandikishwa shuleni na kufikia asilimia 95 mpaka sasa.

Hata hivyo, wakati serikali ikiwa imefanikiwa katika kuandikisha wanafunzi wengi katika shule za msingi, utafiti uliofanywa na asasi ya kiraia iitwayo Twaweza, umeonyesha kuwepo kwa kasoro kubwa katika mchakato wa ujifunzaji kwa wanafunzi wengi wa elimu ya msingi..

Utafiti huo uliopewa jina la 'Are Our Children Learning', ulibainisha zaidi kwamba, si tu wahitimu wengi hawawezi kufikiri, kujitegemea, kujiamini, kuchambua mambo, kuuliza na kuwa wadadisi, lakini pia baadhi yao wanapigwa chenga na stadi za msingi za kusoma na kuhesabu.

Ripoti ya matokeo ya utafiti huo iliyosomwa kwa wanahabari inaonyesha kuwa nusu ya wanafunzi wanaomaliza shule ya msingi hawawezi kusoma lugha ya Kiingereza.

Si Kiingereza tu, ripoti hiyo iliyoshirikisha wanafunzi zaidi ya 40,000 katika wilaya 38 nchi nzima inabainisha kuwa wanafunzi wengi wanakosa stadi za msingi za kusoma katika lugha ya Kiswahili ambayo kwa wengi ni lugha maarufu wanayoitumia kila siku.

Matokeo haya yanatupa picha halisi kuwa licha ya nchi kufanikiwa katika uandikishaji mkubwa wa wanafunzi shuleni, bado kuna kazi kubwa ya kuhakikisha elimu inayotolewa inakidhi viwango vinavyokubalika katika dunia ya sasa.
Hakutakuwa na maana kujisifu kwa takwimu za wanafunzi wanaoandikishwa darasa la kwanza, huku tukijua kabisa hakuna wanachokipata shuleni.

Mzazi yeyote anapompeleka mwanaye shule, anataraji kuwa atapata elimu iliyo bora kwa ajili ya ustawi binafsi na maendeleo ya taifa.

Kinyume na matarajio hayo, wanafunzi hawa ambao serikali inaringia takwimu za wingi wao, ndiyo hao hao wanaomaliza miaka saba darasani wakitoka kapa kichwani.

Serikali lazima itambue kuwa, matokeo ya kuwajaza wanafunzi shuleni bila ya kujiandaa kuwasaidia kitaaluma ni jambo la hatari kwa mustakbali wa nchi hii iliyo bado change kimaendeleo. Ni vigumu kuendelea kwa kuwa na taifa la watu ambao hata stadi za msingi za katika maisha kama kusoma na kuhesabu zinawapiga chenga.

Bila shaka utafiti huu uliwashirikisha watoto wanaosoma katika shule za serikali ambazo nyingi hupokea watoto maskini. Hawa ndiyo watakaoendelea kuburuzwa na wenzao wanaosoma katika shule za wazazi wenye uwezo.

Kwa mtazamo wangu zipo sababu kadhaa zinazochangia hali hii katika shule za serikali ikiwemo uhaba wa walimu na vifaa vya kufundishia na kujifunzia. Na pale penye walimu kuna tatizo la walimu kutokuwa mahiri katika masomo wanayofundisha.

Lakini kubwa zaidi ni kuendelea kukumbatia mfumo mbovu wa elimu ambao nao kwa kiwango kikubwa umeathiriwa na maamuzi ya kisiasa yasiyo na tija katika elimu. Sote tunajua namna wanasiasa walivyoharibu mfumo wa elimu kwa kupiga marufuku mitihani ya darasa la nne na kidato cha pili.

Mtihani wa darasa la nne, ulikuwa kigezo kizuri cha kupima uelewa wa mtoto kama kweli ameelewa ipasavyo yale aliyofundishwa kuanzia darasa la kwanza hadi la tatu ikiwa ni pamoja na stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu.

Lakini ili iweze kupata takwimu za juu kwa lengo la kuwafurahisha wale wanaotufadhili, serikali ikaamua kuruhusu hata wale wanafunzi wanaoshindwa katika mitihani ili wajaze tu idadi ya wanafunzi wanaomaliza shule.

Mtihani wa darasa la nne ungekuwa chujio muhimu la kubaini wanafunzi wenye uwezo na wasio na uwezo kitaaluma. Tusingekuwa na taarifa ya wanafunzi wanaomaliza elimu ya msingi kama mtihani huu ungekuwepo.

Hali hii inajitokeza pia upande wa sekondari.Tumepiga marufuku mtihani wa kidato cha pili kwa lengo lile lile la kuongeza idadi ya takwimu za wanaomaliza elimu ya sekondari. Kwa wanaofuatilia matokeo ya mitihani ya taifa wanakumbuka matokeo mabaya ya wanafunzi wa kidato cha nne mwaka 2009.

Kwa nini wanafunzi waliopata daraja sifuri walikuwa wengi? Jibu ni rahisi, wengi ni wale waliokuwa hawajitumi shuleni kwa kuwa waliamini hakuna mtihani wa kuwapima hadi wanafika kidato cha nne.

Sitetei utaratibu wa kuwachuja wanafunzi kama inavyofanyika katika baadhi ya shule binafsi ambazo hatimaye hufanya vizuri katika mitihani ya mwisho, ninachokisema kufuta mitihani ya darasa na nne na kidato cha pili kumewapa mwanya wanafunzi kuzembea zaidi kimasomo wakiamini hakuna wa kuwazuia kumaliza shule.

Siasa imeharibu elimu na nina kila sababu ya kuwalaumu wanasiasa wanaoendesha serikali yetu kwa sasa. Serikali ilaumiwe kwa haya yanayojiri sasa shuleni.
O754224336
 
Mimi nadhani wasomi wengi wanakwepa ukweli mkubwa ktk majibu mazito yanayotakiwa hasa ktk swali kubwa la Kitaifa. Kwa Nini Tanzania bado ni maskini?..

Tukiweza kujibu swali hili nadhani ndipo tunaweza pima mafanikio yoyote yale kulingana na kila hatua tunayopiga kwani hata gari lililokwama ktk tope magurudumu yake kuzunguka na mkafikiri mna kwenda kumbe kwa kila jitihada hizo ndio kwanza mnazidi kujichimbia zaidi. Kwa kutambua wapi tumekwama na sababu zake nadhani itaturahisishia zaidi kutoka ktk lindi hili la Umaskini badala ya kuorodhesha mambo kibao ambayo kusema kweli hayana tija kwetu sote uwe CCM, Chadema,TLP au CUF..

Mimi nimesema toka mwaka 2005 wakati wa Mkapa na nitarudia kusema tena kwamba Tanzania haitaweza ondokana na Umaskini pasipo kukomesha UFISADI..Ni ufisadi ndio umetukwamisha hapa tulipo na sii kwamba Mkapa au Kikwete hawakufanya kitu bali Udhaifu wao ktk kusimamia shieria ndio umesababisha matokeo ya Tanzania hii tulokuwa nayo.

Kikwete kajaribu mbinu nyingi lakini imetugharimu mara tano ya nguvu na fedha zilizotakiwa kutumika hata ktk madogo yaliyofanyika ambayo sii mafanikio isipokuwa ni aibu kubwa ktk utawala bora. Kama ilivyotugharibu kujenga Benki kuu kulipa gharama ya mara 5 (500%) ya gharama halisi ilotakiwa ndivyo mikakati yote nchini imekuwa ikitekelezwa hivyo.

Tusitake kusifia pakacha lililotupu au lilojaa nusu likivuja kwa gharama ilotumika ya ujazo. Nafikiri watu wengi hapa kijiweni wanakwepa sana ukweli huu na mara zote wanashindwa kuuzungumzia hali bado wamegubikwa na maswali magumu kuhusiana na Umaskini wetu. Dhahiri wote wanakubali kwamba umaskini wetu ni wa kujitakia lakini wakati huo huo tunakataa ukweli ulio wazi kabisa kwamba UFISADI ndio sababu kubwa.

Hivyo kuwepo kwa record ya Utekelezaji hakuna maana kwamba ni mafanikio ikiwa utekelezaji huo hauna kipimo cha Accountability, quality, durability, na sustainability kwani ukitazama hata hizo barabara zilizojengwa ni asilimi 20 tu ya fedha za misaada tulopewa ndio imetumika kujenga barabara hizo, fedha nyingine zimeingia mifukoni mwa watu binafsi kwa njia isiyokuwa halali. Mashule, Kilimo na Zahanati kote huko fedha zilizokuwa allocated kwa ajili ya kufanikisha sehemu hizo ni asilimia ndogo sana imetumika hivyo kupata vitu hafifu sana ukilinganisha na fedha ilotakiwa kutumika.

Barabara zetu zote zimejengwa pasipo mifereji ya maji taka ya kisasa, na zote hazina muda mrefu wa kudumu kwani hata zile zinazosifika tayari zimekwisha anza kuharibika. Hakuna barabara yoyote ilojengwa miaka hii ambayo unaweza kuilinganisha na hata barabara ya Pugu au Magomeni (Kajima) kwa Uimara wake. Hivyo kupewa wazalendo wasiokuwa na uzalendo tender za ujenzi wa barabara imekuwa muhali kwetu, naa sababu kubwa ni Ufisadi unaotumika.

Hatuwezi jaza pakacha linalovuja, lenye mirija kila kona hata siku moja, na kama kuna uwezekano huo naomba mwanaJF yeyote anieleze uwezekano huo!. Hata Dr.Slaa akiingia Ikulu pasipo kuthibiti Ufisadi atakuwa amefanya zero kama nilivyosema wakati wa JK akiingia madarakani..huu niu ukweli pekee ambao Watanzania kwa dharau zetu tumeshindwa kabisa kuukubali kwa sababu za kimaskini vile vile (Ujinga na Ulimbukeni) Na hakika Kikwete kajaribu sana kufanya mengi yenye nia njema kwa Taifa (kupaka rangi mpya juu ya ile ya zamani) lakini UDHAIFU wake ktk kuthibiti Ufisadi na kutafuta njia za mkato ndio sababu kubwa ya Watanzania kutaka mabadiliko ya Uongozi uliopo..
 
Ndiyo ina record ya kutumia record za record za Mkapa...za kikwete zi wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…