Ndani ya mfumo wa CCM na hata serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamejazana viongozi/watendaji wasio na uwezo na hii inatokana na kutokuwepo vetting system inayoeleweka.
Huwezi kujenga taifa Bora kama hauna vetting system.sisi hata vetting system hatujui maana yake.
Sifa pekee ya kupata nafasi ya uongozi ndani ya CCM ni kuwa na mtu mmoja au watu kadhaa wenye access kwa Rais na mamlaka zingine za uteuzi.huyu au hao watu wakikusemea basi game is over.
Sifa nyingine inaweza kuwa fitna,majungu na kujipendekeza na nyingine yenye nguvu ni kuwa mtoto wa au kimada wa wastaafu.
Unakuwaje na taifa lenye utitiri wa viongozi wasio waadilifu kiasi hiki? Wapiga dili kila Kona, viongozi wanaosaka umaarufu, washamba, waliojaa elements za ukabila na udini, wazembe, wenye kiburi na wasio na maono
Ubunifu uko wapi? Mbona hakuna mipango yenye akili kubwa ya muda mrefu?
Viongozi wetu wengi siyo analytical yaani hawana uwezo wa kuchambua mambo na hawana maarifa wala ujuzi katika kutatua matatizo ya wananchi
Nina uhakika kuwa CCM inaongozwa na watu wasio na uwezo, wenye uwezo wako nje ya mfumo.
si miaka ya hivi karibuni CCM ilimteua Kulwa Milonge kuwa katibu wa CCM mkoa wa Morogoro? Mtu ambaye baadaye ilibainika hajui kusoma na kuandika. Yeye alikuwa mcheza ndombolo pale VIJANA JAZZ BAND. Siku hizi ameshushwa kuwa katibu wa Wilaya.
Sasa huko wilayani anafanya nini?
Leo hii Jokate Mwegelo ndiyo mtendaji wa UVCCM taifa?Hivi hii inawezekana?
Lakini watazame watendaji wa CCM wilaya na Mikoa.wengi wao hawajui kabisa wanachokifanya na ndiyo maana CCM inaendelea kuongoza nchi kutokana na nguvu kubwa inayotumiwa na vyombo vya ulinzi na usalama na masuala mengine ya kimataifa, CCM kama chama haina uwezo tena wa kushinda uchaguzi bila kutegemea vyombo hivyo kwani mfumo wake ni wa hovyo ambao watu wajinga wamepewa madaraka makubwa.
CCM hawana database maalumu ya makada wao,mfano huyu ni nani hasa?yuko wapi? Anafanya nini,amesomea nini? Ana kipaji gani na kadhalika.Hii ingekisaidia Chama hicho katika vetting system.
Hata ndani ya mfumo wa serikali hakuna mfumo maalumu ambao ni independent na imara unaofanya Kazi kwa weledi na kwa kufikiria maslahi mapana ya taifa.
Rais Dr Samia Suluhu Hassan anapata shida anapofanya uteuzi kwani hakuna mfumo unaomwezesha kuwatambua watu ipasavyo na badala yake anaona majina yaleyale kila siku na hivyo kusababisha tatizo lingine la Leadership recycling.
Hivi unajua Petro Magoti juzijuzi tu ndiyo ametolewa ikulu? Hivi Petro Magoti anaweza kumshauri kitu gani Rais? Petro Magoti ana sifa ya kufanya kazi ikulu?
Sisemi haya kwasababu ni mlemavu lahasha, nasema kwa kuwa najua hana uwezo na ndiyo maana kitu pekee alichokuwa anafanya Ikulu ni kuwagombanisha wenzake.
Na kwasababu wanaoteua hawajui wanachokifanya Magoti leo hii ni DC wa Kisarawe.mimi nisingemteua nafasi hiyo.
Ningeweza kumteua nafasi ya Katibu Tawala wa Wilaya( DAS)ili akamsaidie DC kwenye masuala ya kijamii kwasababu hawezi pilikapilika za U-DC. na siyo Administrator mzuri.
Kwenye vetting system lazima muwe na uwezo wa kutenganisha nafasi za kisiasa na za utendaji.
Nataja majina machache tu kama mfano na majungu siyo sehemu yangu ya maisha
Ifike mahali tubadilike, tupunguze uswahili ili tuweze kujenga taifa bora.
Tazama viongozi wetu wengi wanapohutubia, hawahutubii Kwa hisia kali, kuzungumza kwa hisia ni muhimu sana kwani kunaonyesha "unaguswa"
Tuamke.
Tanzania inatakiwa kuwa nchi muhimu Afrika na Dunia Kwa ujumla lakini hatuwezi kufika huko kama mfumo wetu wa uongozi umejaa watu wasio na sifa za uongozi.
Mungu Ibariki Afrika
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Mbariki Rais wetu Dr Samia Suluhu Hassan na serikali ya Tanzania.
Amen