CCM ina tatizo la kuwa-brand watu wasio na uwezo.

Mbaya zaidi ndio imekua kama Role Model ya taasisi nyingine hata zisizokua za kiserikali kufanya teuzi za watu wa aina na kariba ya sifa kama ulizoziandika humu.
 
Mafikunyungu ni mengi serikalini hasa wakuu wa Idara nyeti. N
Vye0 vinapatikana kwa ndumba,ushirikina,majungu nk na siyo uwezo binafsi. Wenye uwezo hawaamini macho yao anapopewa ukuu wa Mkoa form four failure hasa Mikoa nyeti na ya Kimkakati!!.
 
Hapo kwa Jokate umekosea mazima...huyo binti kichwani zina-charge sana, kwa andiko lako hili ni rahisi kabisa kung'amua kwamba IQ ya Jokate imekuzidi by far.
Ila Yuko CCM, hapo ndio IQ yake inapokua ndogo
 
Ndani ya mfumo wa CCM na hata serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamejazana viongozi/watendaji wasio na uwezo na hii inatokana na kutokuwepo vetting system inayoeleweka.
Very true Mkuu.
Na ndio maana kauli za viongozi wengi wa ccm hujaa ulimbukeni ujinga na dhararu kwa walio chini yao.
 
Hii shida haipo CCM bali hadi Serikalini.

Wenye uwezo na akili hawapewi nafasi. Wenye upeo mkubwa na mawazo yenye kuifanya hii nchi kuwa bora hawapewi nafasi. Wanaopewa nafasi ni chawa, watu wasio na uwezo kwa sababu ya kujipendekeza.

Tanzania ina watu wengi sana wenye upeo, maarifa na akili za kuifanya nchi yetu kuwa nchi bora zaidi kimaisha na kiuchumi hapa Afrika ila kamwe huwezi ona wakipewa nafasi zaidi ya wajinga wajinga tu!
 
Simply sifa ya uchawa ndo sifa mama
 
Kwenye Mawizara niliwahi sikia wale watumishi ambao huwa wana uwezo wa kuandika maandiko, mipango mizuri kwa maendeleo ya kweli huwa wanapigwa vita sana na hata siku moja huwezi waona wakiwa wanapendekezwa kushika nafasi za juu za uongozi kwenye Mawizara na Maofisi ya Serikali.

Siku ya mwisho huwa wanastaafu wakiwa watu wa kawaida na wanaondoka Serikalini na mawazo yao mazuri. Wengine wanakufa wakiwa na vitu vyao vizuri kichwani.

Serikalini huko watu wanasoma Masters na PHD ili wapande vyeo. Wakati watu wenye uwezo wanaachwa kabisa.

Mbaya zaidi wengine wanapewa vyeo eti kwa sababu hawezi wabishia au kuwashauri kwa kujiamini wakubwa wake, ni chawa, undugu, kujuana n.k.

Hii nchi kwa kweli inahitaji Factory setting ili tuanze upya kwa sehemu kubwa. Na hili ni rahisi tukianzia kwenye Katiba Mpya tu.
 
Uko sahihi...ila Hilo neno kajitu ,linadhalilisha...litoe please..utaambiwa unadhalilisha Kwa maumbile yake!
 
Ili upate uteuzi ccm lazima uwe mbumbumbu ama ukubali kuishi kimbumbumbu hata kama ni msomi.
The problem of Africans, those with ideas have no power, and those with power have no ideas.
 
Kwenye taasisi na idara zote kabisa za Serikali na hata katikΓ  baadhi ya Makampuni binafsi hali iko hivyo. Mtumishi au Mfanyakazi yoyote yule ambaye atabainika kuwa yuko smart Sana kichwani, ni mbunifu au mwenye mawazo na fikra chanya zenye uwezo wa kuleta tija au mabadiliko mahala pa kazi, basi huyo ajiandae kupigwa Vita kubwa Sana kutoka kwa Wafanyakazi wenzake ambao ni vilaza au mbumbumbu. Atafanyiwa kila aina ya fitina, chuki, hujuma na kila aina ya uovu ili ashindwe kazi. Afrika ni mahali pagumu Sana kwa kuishi kwa Watu wenye akili timamu sawa sawa kabisa kichwani mwao, ni pagumu haswa.
 
CCM huwa hawaangalii Merit wao wachoangalia ni mkata kiuno mzuri wa Chama na mwenye uwezo wa kuongea kama Chrehani
 
Kwa mtu mwenye uchungu na mzalendo akisoma hili andiko na kufananisha na yanayoendelea basi anaweza kulia.
 
Mungu Mbariki Rais wetu Dr Samia Suluhu Hassan na serikali ya Tanzania.
Huu ni Msiba mzito yaan nimesoma hadi nimemaliza nikajihisi km nimefiwa na Ndugu yangu wa karibu sana
 
Kwa namna unavyoona post za kuwabrand sijui Mwigulu, January, Makonda, Polepole mara Doto Biteko kuwa Marais wa JMT ndo unaamini kuwa kuna shida kubwa sana huko chama cha Mapinduzi na endapo tuaipopata Katiba Mpya haraka hii nchi itaelekea shimoni.

Kuna watu wanaaandika mambo mazuri ya kuisaidia hii nchi ila huwezi wasikia popote unawasikia wajinga wajinga wanaojua kupiga mdomo kila siku.
 
Chadema inayoongozwa na mwenyekiti asiekuwa na walau kadegree kamoja ndio mwenye uwezo?
Acha majungu kwenye vitu serious watu tupo msibani usilete utani wa ngumi utasababisha kutokee msiba mwingine
 
Hapo kwenye vimada inakwenda mbali mpaka watoto na ndugu wa vimada pia.

Kuna watu ni Waziri, makatibu, MaRC nk kwasababu tu baba yake/mama yake alikuwa kwenye utumishi.
Hatupimi tena uwezo bali tunaangalia connection yako mbaya zaidi hili mpaka kwenye taasisi nyeti kabisa ambazo akili, uwezo na uelewa kinapaswa kuwa kipaumbele number Moja.

Watu hawa na ajira hizi ndio zimetufikisha hapa, maana watu wako busy kutengeneza utajiri binafsi na wavizazi vyao na sio kufikiria Leo na kesho ya Tanzania na Watanzania.
Watu hawa wamefanya siasa kuwa ajira inayolipa sana na utumishi wa umma kuwa ni ajira inayolipa sana kwa wizi na usanii na sio tena professional jobs nk, matokeo yake vijana wote wanawaza kuwa wanasiasa na watumishi waumma ili wawe matajiri na sio kutumikia wananchi.

Leo hii mfanyakazi wa kawaidak TRA, TPA nk anakuwa milionea bila kufanya biashara yeyote, mtumishi wa umma anawezaje kuwa millionea na si mfanyabiashara au experts wa field fulani kwenye sekta binafsi?
 
Nimelia sana kwa hio nini kifanyike?
 
Unajua kwanini wenye uwezo hawapewi nafasi na hata wakijitokeza wanapigwa vita? Si rahis ku control mtu mwenye akili, ila ni rahisi kum control chawa,mnafki.

Wanachotaka wao ni watu rahisi ku control na si efficient
 
Daaaah! umeongea kwa hisia kali sana. Na huo ndiyo ukweli.πŸ‘πŸ‘πŸ‘
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…