CCM ina tatizo la kuwa-brand watu wasio na uwezo.

Unajua kwanini wenye uwezo hawapewi nafasi na hata wakijitokeza wanapigwa vita? Si rahis ku control mtu mwenye akili, ila ni rahisi kum control chawa,mnafki.

Wanachotaka wao ni watu rahisi ku control na si efficient
Kweli kabisa
 
Dawa ni Katiba Mpya.

Tunahitaji Katiba Mpya haraka!
Kwa hio Katiba Mpya ndio itawaondosha hao kupe? HUONI kinachoendelea Kenya? Pamoja na Katiba hali ni Ile ile hakuna afadhari sana sana kumezuka janga lingine la Gen Z
 
Nimelia sana kwa hio nini kifanyike?

Kwasasa nikutoa elimu mtaani ulipo watu waelewe nchi yao inavyooperate na kuacha kujikita kwenye ubishani wa Simba,Yanga, mara Diamond sijui Mobeto huku Taifa lao likiliwa na wao kuachiwa chain ya umasikini.

Watu wengi wakielimika na kujua hasa nchi yao inavyoendeshwa na kuwa serious kufuatilia muenendo wa Taifa lao itasaidia kujenga kizazi chenye hasira kitakacholeta mabadiriko haraka na kuwawajibisha wajinga wote.

Vyama vya siasa kama viko serious kweli Kwa sasa viachane na harakati ya kushika dola kupitia uchaguzi bali vijikite kutoa elimu na kuitisha makongambano mara kwa mara mubashara ili kuinua hisia za jamii na watu kuelewa nini maana ya wao kuwa watanzania na kunufaika na keki ya Taifa kama wengine wanavyojinufaisha.
 
Mkuu una akili kushinda hata muasisi wa icho chama chao, Big Brain 🧠

Kwa utashi wao ulivokua mdogo wataishia tu kusonya baada ya kusoma ili bandiko kisha kuendelea na ngonjera zao za kuimba na kusifu.

sikujua kama watu wenye akili kama zako bado wanaexist humu jukwaani, nilijua wamebakia vichwa panzi tu kama Lucas Mwashambwa na Tlaatlaah
 
Leo hii watoto wote wa viongozi hawasomi public school bali wako private school tena zile 1st class na nyingine zinatumia mtaala wa Cambridge na Lugha ya kufundishia na kuwasiliana ni kiingereza.

Viongozi hawa hawa wanakwambia mfumo huu wa elimu tunaoutumia uko vizuri kabisa na Lugha yetu adhimu ya kiswahili lazima tuienzi kwa kuiifanya kama Lugha ya kusomea/kufundishia matokeo yake tunawaacha nyuma mamilioni ya Watanzania kwenye soko la Dunia la ajira na fursa zilizopo duniani.
 
Kwa hio Katiba Mpya ndio itawaondosha hao kupe? HUONI kinachoendelea Kenya? Pamoja na Katiba hali ni Ile ile hakuna afadhari sana sana kumezuka janga lingine la Gen Z
Hapana. Shida ya Tanzania ni Katiba Bora.

Matatizo ya Kenya na Tanzania yana utofauti mkubwa sana. Sie kwa matatizo yetu ya kupata watu wasio wa uwezo na maarifa sahihi katika nafasi za juu ya maamuzi yanayoamua mustakabali wa maendeleo ya Taifa letu na Wananchi wake, dawa yake ni Katiba Mpya iliyo Bora tu.
 
Nimeipenda hii
 
Ebu tuelezee unataka hio Katiba Mpya & Bora iweje iweje japo kwa ufupi
 
Ebu tuelezee unataka hio Katiba Mpya & Bora iweje iweje japo kwa ufupi
Katiba inayoweka nguvu kwa mifumo na sio Wanasiasa. Katiba inayosema ni kosa la Jinai kwa kiongozi yeyote kuivunja na inayoweka utaratibu mzuri wa kuwajibishwa kwake endapo ataivunja.

Katiba inayotamka nafasi za uteuzi wa Rais zitathibitishwa na Bunge. Nafasi hizo ni pamoja na nafasi za Mawaziri na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama.

Kwa Nafasi za Watendaji wa Mashirika na Taasisi za Umma hawa wapatikane kwa njia ya Ushindani na Wawajibike kwenye bodi zao tu!

Wakuu wa Mikoa na Wilaya wapatikana kwa kuchaguliwa na Wananchi husika.

Taasisi za Kikatiba( Vyombo tendaji) zilindwe na Katiba. Wanasiasa wasiziingilie kwa namna yeyote ile. Na endapo wakiziingilia uwekwe utaratibu wa kuwajibishwa na Katiba hiyo hiyo.

Tukienda hivi tutapata watu wenye uwezo katika nafasi za juu za maamuzi.
 
Magoti hakua mshauri wa raisi, magoti alikua msaidizi tu
Unasema alifaa kuwa DAS na sio mkuu wa wilaya sababu sio administrator mzuri, Sasa hujui DAS ndio administrator? Hiyo "A" kwenye DAS maana yake ni administrative

Pia umemuunderrate sana Jokate, sijui unamlinganisha na nani, au Kamala Harris?
 
Magoti hastahili hata kuwa DAS.

Ndo hivyo kutokana na ubovu wa Katiba yetu tunapata watu wa hovyo kwa sababu tu za huruma, uchawa, kujuana, undugu n.k

Jokate pia hana upeo mkubwa wowote. She is overrated huko CCM.

Ukitaka kujua mtu ana uwezo au upeo wowote angalia hawa Viongozi wanapokuja humu JF wanapopigwa maswali ya maana wanavyokimbia na kushindwa kujibu!

Mie humu JF saivi nimekuwa nikiwauliza chawa wanaokuja humu kujisifia na kujionesha maswali ya kupima uwezo na upeo wao kama wanaweza kweli kushika nafasi wanazozitamani ila hadi sasa nakuhakikishia kwa asilimia 100 hakuna hata mmoja aliyenishawishi kuwa na uwezo na maarifa wa kushika nafasi wanazozitamani
 
Hii ni kawaida, hata ww unaoona wanacaa mm naweza kusema kama haya ambayo umesema
 
Dawa ni Katiba Mpya.

Tunahitaji Katiba Mpya haraka!
Siyo Katiba Mpya tu, bali ni Katiba Mpya iliyo nzuri itakayotokana na Maoni, mawazo na fikra za wananchi walio wengi zaidi katika nchi hii ya Tanzania.

Watu wale wale waovu waliotunga Katiba hii mbaya iliyopo hivi sasa wanaweza wakatunga Katiba Mpya ya kwao ambayo inaweza kuwa mbaya zaidi pengine kuliko hata hii iliyopo, tatizo linaweza kubaki hivi hivi licha ya kwamba imetungwa Katiba Mpya.
 
Na hii ndo hoja yangu hasa. Katiba Mpya ambayo ni Katiba Bora
 
Think tanks wanaotakiwa pale sifa ya kwanza na muhimu kabisa ni lazima awe Chawa kwanza !πŸ˜³πŸ™Œ
 
Mafikunyungu ni mengi serikalini hasa wakuu wa Idara nyeti. N
Vye0 vinapatikana kwa ndumba,ushirikina,majungu nk na siyo uwezo binafsi. Wenye uwezo hawaamini macho yao anapopewa ukuu wa Mkoa form four failure hasa Mikoa nyeti na ya Kimkakati!!.
Iko vile !
Tunalipa fadhila Mkuu πŸ˜³πŸ™„ !
 
Nakupitia uko kwasababu yakuonekana kila siku kwenye tv kuandikwa kwenye magazeti na social media mbalimbali ndiko rais wa Nchi anakotokea. Mm najiuliza kuna watu wengi wazuri na wasomi wenye maono either kwenye private sector ata baadhi ya mashirika ya Umma lkn kwa vile awajawai kuingia kwenye siasa inakuwa ningumu kupata hzo nafasi matokeo yake ndo hv. ifike muda mgombea binafsi aluhusiwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…