CCM inaenda kuondolewa na watumishi wa Umma, Wahitimu wa Vyuo, Wakulima na wafanyabiashara

CCM inaenda kuondolewa na watumishi wa Umma, Wahitimu wa Vyuo, Wakulima na wafanyabiashara

Trust None

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2018
Posts
1,260
Reaction score
4,419
Watumishi wa umma hawajapata nyongeza ya mishahara kwa miaka mitano, kupanda madaraja na vyeo ni ndoto, uhamisho wa kubadilishana ni hadithi

Wahitimu wengi sana wa vyuo hawana ajira tangu 2015 mpaka sasa, ajira ya moja kwa moja ilikoma Mei 01, 2015 enzi za Jakaya. Wakulima wanadhulumiwa mazao yao, hawalipwi kwa wakati hadi wengine huitwa kangomba.

Wafanyabiashara wanalia na kodi kubwa, wengine waliamua kuhamishia biashara zao nchi za nje. Kuna wengine wanaagiza mizigo kupitia bandari ya Dar kuwa inaenda tuseme Uganda, lakini ilivuka mpaka tu inapiga U-Turn kurudi Tz, hapa ndipo tulipofika. Kodi ya bandari kwa mizigo ya nchi za nje ni ndogo sana ukilinganisha na mizigo inayobaki nchini.

Oktoba 28, 2020 wakati mwafaka wa maamzi mwafaka
 
Tunajenga nchi,vumilia kidogo,mambo mazuri hayataki haraka,hata Guangzhou unayoiona leo haikuwa rahisi kwa wananchi wa China,kirahisi hivyo unavyofikiria...
 
Nimenunua ndege, nimejenga stiglers gorge, nimejenga flyovers, nimejenga standard gauge!!! Miaka mitano amefanya siasa peke yake huku akihubiri mambo yale yale! lakini mpaka leo anapendwa kwa kuwalazimisha tu watu. Sidhani kama ana mvuto kwa wananchi walio wengi.

Labda wale wasanii 100 watumike kuwavutia wananchi kwa ajili tu ya burudani. Kinyume na hapo walio wengi watafurika kwa Tundu Lissu ili walau wakapate matumaini ya maisha bora.
 
Wafanyakazi waliotumbuliwa na waliokumbwa na vyeti fake vya form 4 wakati huo wanavyeti vya taaluma ambavyo siyo fake nao kura zitaenda upinzani
 
Wafanyakazi waliotumbuliwa na waliokumbwa na vyeti fake vya form 4 wakati huo wanavyeti vya taaluma ambavyo siyo fake nao kura zitaenda upinzani
Nimemuona Jiwe akitorokea Rwanda kabla ya hitimisho la uchaguzi. Hawezi kuhimili vishindo vya Antiphas Lissu. Pace make itaishiwa chaji na itakufa kabisa
 
Sema we jamaa tabili zako huwa zinakuwa kweli
 
Huo ndo ukweli mchungu........

Uchumi wa kati fekeroooo.....
 
Back
Top Bottom