CCM inaenda kuondolewa na watumishi wa Umma, Wahitimu wa Vyuo, Wakulima na wafanyabiashara

CCM inaenda kuondolewa na watumishi wa Umma, Wahitimu wa Vyuo, Wakulima na wafanyabiashara

Hivi ni nani huwa anaamua watumishi wa umma wapate walau nyongeza za mshahara, mapunjo, madaraja hela za rikizo na stahiki nyingine??
Wamesahaurika sana eti
 
Mwaka huu sioni popote Magufuli anaweza tokea. Nasema sioni popote. Ameumiza sana watu, ametesa sana watu. Watu wamepoteza Kazi na ajira kwa chuki zake na sekta binafsi. Mwaka huu njia ni nyeupe sana kwa Lissu
 
Yawezekana hata huna takwimu sahihi juu ya unachikiongea,haya watumishi wa umma ni hawazidi Millioni moja,wafanyabiashara nao hawazidi Millioni mbili,wahitimu wa vyuo pamoja na wale ambao bado wako vyuoni hawazidi Millioni mbili,sasa ukijumlisha unapata watu Millioni tano,kwenye hao watumishi wa umma niondoe mimi na Mke wangu,màana hatuwezi kumpa kura lissu kijana mpuuzi,

Pia tambua waliojiandisha ni watu Millioni 22 sasa wewe una watu Millioni NNE +,huu urais unaoongelea wa huyu lissu wako anaupata wapi!
 
kwani uchaguzi uliopita mshidi alipata kura ngapi.....? tuanzie hapo kisha turudi kwenye hiyo milioni nne unayoikisia, japo pia sidhani kama mwaka huu muitikio utakuwa mkubwa , ukirejea yaliyofanyika kwenye uchaguzi wa serikali za mtaa.
 
Mnasemaga hivi hivi halafu baada ya oktoba 28 2020 mtakuja hapa kulalamika mmeonewa mara mmeibiwa kura
 
Mabwana wale hua hawategemei kura kushinda.
 
Hivi ni nani huwa anaamua watumishi wa umma wapate walau nyongeza za mshahara, mapunjo, madaraja hela za rikizo na stahiki nyingine??
Wamesahaurika sana eti
Ni Yule yule ambae ikija mambo ya miradi ya barabara,madaraja,viwanja vya ndege,reli anasemaga tuna mapesa mengi sana lkn ikija kwny annual increaments,kuajiri,kulipa wastaafu anakua hana pesa.

Ajabu sana.
 
Watu unaowaongelea kwanza ni proportion ndogo sana ya Watanzania.Na hata hao unaowaongelea, wafanyakazi, wahitimu, wafanyabiashara na wakulima ambao hawajalipwa wengi ni waelewa,wanaona uhalisia wa mambo anayofanya Maguguli.Wanaona kwamba hili ni kipindi cha mpito tu,anafukia mashimo.

Mkuu tuna ongea nao,we hear what they are saying,so yours is wishful thinking.
 
Watu unaowaongelea kwanza ni proportion ndogo sana ya Watanzania.Na hata hao unaowaongelea,wafanyakazi,wahitimu,wafanyabiashara na wakulima ambao hawajalipwa wengi ni waelewa,wanaona uhalisia wa mambo anayofanya Maguguli.Wanaona kwamba hili ni kipindi cha mpito tu,anafukia mashimo.Mkuu tuna ongea nao,we hear what they are saying,so yours is wishful thinking.
Hahah aisee
 
Labda kwenye udiwani na ubunge. Lakini ngazi ya urais CCM lazima ishinde tu tutake tusitake hebu tuache kuota ndoto za mchana.

Tukubali ukweli tu hata kama mchungu kama shubili, pamoja na madhaifu yote uliyotaja ngazi ya urais CCM itashinda.
 
Utadhani Chadema ni chama kipya, yani ndio siasa zimenoga.
 
Jiwe alifikiri miaka mitano mingi Sana haitofika ,hiyo sasa sijui atasema nini zaidi ya kuiba kura ,vilevile aliowabomolea nyumba zao aliwalia helal zao za tetemeko la Kagera wote wanamsubiri ,sijui ataponea wapi?
 
Back
Top Bottom