Elections 2010 CCM inajiandaa kuwa wapinzani au kuingia msituni?

akashube

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2009
Posts
401
Reaction score
23
Ukifuatilia kwa undani kampeni za wagombea wa udiwani, ubunge na urais kupitia chama cha ma.....CCM utagundua yafuatayo:

1. Wanazungumzia barabara, umeme, kilimo, ajira, maji na amani na utulivu. CCM inadai kuwa wameleta maendeleo nchini kwa kuleta maendeleo katika mambo haya.

SWALI: Je ni kweli mpaka leo hii haya bado yanaendelea kuwa matatizo. Je hatukutakiwa kuwa tumekwisha malizana na haya....na pengine tuzungumzie sasa viwanda, elimu bora, uchumi imara, teknolojia na sayansi, uimara wa Taifa katika masuala ya kimataifa. JE NI NANI ALIYETUDUMAZA KAMA SIO CCM?

2. Wanazungumzia kuwa wapinzani wakichaguliwa nchi itaingia katika vita.

SWALI: Je ni nani atakayeleta vita hivyo? au ni kutisha wananchi kuwa CHADEMA au CUF au chama kingine cha upinzani kikishika madaraka CCM wataingia msituni?

3. Wanazungumzia wamejenga barabara kwa kuwa hakukuwa na barabara.

SWALI: Hakukuwa na barabara chini ya serikali ya chama gani? na ni barabara gani mpya za maana na za kiwango cha wakati tulionao zilizojengwa na CCM?

4. Wanadai CCM imetimiza ilichoahidi.

SWALI: Je ukiahidi chini ya kiwango ukatimiza....umetimiza ahadi au umetimiza uhuni. Ok nifafanue kidogo... unapoahidi kufeli kwenye mtihani wako na ukafeli unakuwa umetimiza ahadi au umetimiza uhuni....tumeelewana sasa? haya swali hilo

5. Wanadai kuwa vyama vya upinzani vinatoa ahadi ambazo hazitekelezeki.

SWALI: Je ni ahadi zisizotekelezeka au ni ahadi zisizotekelezeka kwa CCM.... bali zinazotekelezeka ikiwa chama tawala kimeamua kweli kufanya kazi iliyowapeleka madarakani..?? ......Hivi sera ya elimu bure kwa kila mtanzania kwa elimu ya lazima ya hadi kidato cha sita; sera ya CHADEMA ni kweli CCM inaona haitekelezeki?

SWALI: Hivi uongo huu wa wazi wazi wa CCM ni kwa sababu wanahisi wamefanikiwa kuwafanya watanzania wasiwe na uelewa wa mambo kwa kuwa wamewanyima elimu kwa makusudi. Hapa naweza kuuandika msemo wa kweli kabisa 'ujinga wa watanzania ndio mafanikio ya CCM'

KWA KUJINADI KWA NAMNA HII CCM JE INAJIANDAA KUWA CHAMA CHA UPINZANI, KUIBA KURA AU KUINGIA MSITUNI?
 
Kuingia msituni tu ndo nia yao, waingie tu watapigana na wake zao sh#$%^&zy kabisa
 


Madaraka matamu. Kuyaachia hivi hivi ngumu. Usalama wa taifa tunasikia wameanza kazi maalumu kwa amri ya bwana mkubwa. Mimi naendelea kumwomba Mungu mambo yawe shwari kwa nchi yetu.
 
Kuingia msituni tu ndo nia yao, waingie tu watapigana na wake zao sh#$%^&zy kabisa

Mpaka sasa wanasema wapinzania wawe tayari kukubali matokeo......bado nina maswali mengi kwa CCM ikiwemo la kukubali matokeo....JE CCM KWELI WAKO TAYARI KUKUBALI MATOKEO TAREHE 31 OCTOBER 2010??????
 
Mi naona hata suala la barabara kikwete ameendeleza ahadi zile zile za mwaka elfu mbili na tano. kwa kumbukumbu zangu ilani ya sasa ya chama cha mapinduzi ni ile ile ya miaka mitano iliyopita ambayo haikutekelezwa na sasa wanatuadaa tena.

kadi yangu ya kupiga kura ninayo. sitamkosea Mungu kwa kuchagua tena CCM. Kura yangu sasa nimeamua nimpe Dokta Slaa na CHADEMA.
 
Originally Posted by akashube

unapoahidi kufeli kwenye mtihani wako na ukafeli unakuwa umetimiza ahadi au umetimiza uhuni


Hii ni nukuu ya leo


Haswaa mkuu hii naomba kwa ruhusa ya wahusika niiweke kwenye kumbukumbu. Inaonyesha CCM waliahidi kufeli na wamefeli haswa na sasa wameahidi kufeli zaidi kwa kasi zaidi, hari zaidi na nguvu zaidi.
 
Wacha waende tutawasindikiza kama wanahitaji nauli tutawachangia halahala wasibakie msituni milele wakipigana na nyani badala ya binadamu.
Waache kututisha bana.
 
Hivi kweli maisha ya msituni CCM watayaweza? Umweke Kepteni Komba na TOT yake na kile kitambi ataweza kweli kukimbia na AK-47?
 
Hivi kweli maisha ya msituni CCM watayaweza? Umweke Kepteni Komba na TOT yake na kile kitambi ataweza kweli kukimbia na AK-47?

Hata mimi najiuliza.....na hasa ukizingatia kuwa msituni hakuna khanga, pilau wala takrima.

msituni hakuna mambo ya 'oyeeeeee', na kisha msitu hauna usafiri wa bure.
 
mimi niko bara la asia, niko kakurezato na ni msituni mno, ninamudu kwa sababu nimefuzu mafunzo ya ninjutsu. mafunzo haya yamenigharimu dola za kimarekani milioni saba na elfu hamsini na tisa na mia mbili na sita. na sasa mimi ni grandmaster mwenye dani sita za ninjutsu yaani kama degree za chuo kikuu za martial arts sita.

Msituni sio suala la mchezo. CCM na serikali yetu tulihakikisha tunaweka kambi za jeshi kila msitu, hivyo hatuwezi kukimbilia msituni kwa kuwa msitu haupo tena. Hata hivyo tutashinda tu kwa kuwa wananchi wana imani kubwa na sisi.

Mimi ni mwana CCM halisi na hata hivyo sifahamiki kabisa CCM kwa kuwa nimekuwa nje kwa muda mrefu na ninapambana kivyanguvyangu. Nina mpango wa kusafiri kuja nchini kuanzia tarehe 6 mwezi wa 10 mwaka huu ili kusaidia CCM ishinde.

Ninasoma sana makala za hapa jamvini lakini huwa najibu chache ambazo nahisi zinaandikwa na watu wasioelewa maana ya amani na utulivu.

CCM ni chama pekee bora Tanzania, hata japo sijakaa nyumbani kitambo lakini nafuatilia mambo kwa ukaribu.
 


we kada wa CCM chama cha mapepo ebu jibu maswali ya msingi.....acha kupoteza dira ya mada hii.
 
Huko msituni kuna UPUPU unakuwasha. Sema kama uataka kukunwa. Au Umekwama nauli nini unahitaji msaada wa CCM?!. Unabana Pua mbele za wanaume unatuambia nimetumia 7ml$. Mijitu ya CCm imekaa kifisadi kweli. Kwa shughuli gani huko Asia unayofanya za kukupati hizo pesa au ndo nyie wazee wa kuuza vocha za tig(o).:becky:
 
Doler milion saba za uninja? Sisi si wajunga kama wewe . Nani kakupa hizo hela na kwa madhumini gani. Eti uninja ..nyambaf.
 
Ponti yako ni hipi sasa,kwamba CCM hawawezi kwenda msituni sababu kila msitu una kambi ya jeshi?,Au hawana haja ya kwenda msituni sababu kila msitu una kambi ya jeshi na majeshi yote ni yao?.Au unataka kutuambia umeinvest zaidi ya bilioni saba(za kitanzania) kujifunza huo uninja wako na una dani 6,hayo mafunzo yako yatawasaidia vipi watanzania wanaoishi chini ya dola moja?
 
Madaraka matamu. Kuyaachia hivi hivi ngumu. Usalama wa taifa tunasikia wameanza kazi maalumu kwa amri ya bwana mkubwa. Mimi naendelea kumwomba Mungu mambo yawe shwari kwa nchi yetu.
Kumomba Mungu ni sawa. Lakini Mungu hutenda kupitia mikono na matendo ya binaadamu. Zile enzi za Mungu kutenganisha Bahari ya Shamu ili Waiziraeli wapite ziliishaisha. Kwa hiyo usiombe peke yake hakikisha kuwa unatoa mchango wako. Piga Kura, Linda Kura, Toa Elimu.
 
we kada wa CCM chama cha mapepo ebu jibu maswali ya msingi.....acha kupoteza dira ya mada hii.
Hawana uwezo wa kujibu maswali ya msingi, huoni hata midahalo wanaikimbia! Wanadhani bado tupo kwenye kipindi cha "zidumu fikra za mwenyekiti". Hivi sasa watu wako makini kila kauli inayotolewa na CCM inajadiliwa na kuhojiwa.
Hivi sasa watu wanakaba hadi mate, wakitema tunafukia, wanabaki kutapata!!!!
 
Nguvu ya wapigakura ndiyo kiboko ya yoteeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…