akashube
JF-Expert Member
- Dec 24, 2009
- 401
- 23
Ukifuatilia kwa undani kampeni za wagombea wa udiwani, ubunge na urais kupitia chama cha ma.....CCM utagundua yafuatayo:
1. Wanazungumzia barabara, umeme, kilimo, ajira, maji na amani na utulivu. CCM inadai kuwa wameleta maendeleo nchini kwa kuleta maendeleo katika mambo haya.
SWALI: Je ni kweli mpaka leo hii haya bado yanaendelea kuwa matatizo. Je hatukutakiwa kuwa tumekwisha malizana na haya....na pengine tuzungumzie sasa viwanda, elimu bora, uchumi imara, teknolojia na sayansi, uimara wa Taifa katika masuala ya kimataifa. JE NI NANI ALIYETUDUMAZA KAMA SIO CCM?
2. Wanazungumzia kuwa wapinzani wakichaguliwa nchi itaingia katika vita.
SWALI: Je ni nani atakayeleta vita hivyo? au ni kutisha wananchi kuwa CHADEMA au CUF au chama kingine cha upinzani kikishika madaraka CCM wataingia msituni?
3. Wanazungumzia wamejenga barabara kwa kuwa hakukuwa na barabara.
SWALI: Hakukuwa na barabara chini ya serikali ya chama gani? na ni barabara gani mpya za maana na za kiwango cha wakati tulionao zilizojengwa na CCM?
4. Wanadai CCM imetimiza ilichoahidi.
SWALI: Je ukiahidi chini ya kiwango ukatimiza....umetimiza ahadi au umetimiza uhuni. Ok nifafanue kidogo... unapoahidi kufeli kwenye mtihani wako na ukafeli unakuwa umetimiza ahadi au umetimiza uhuni....tumeelewana sasa? haya swali hilo
5. Wanadai kuwa vyama vya upinzani vinatoa ahadi ambazo hazitekelezeki.
SWALI: Je ni ahadi zisizotekelezeka au ni ahadi zisizotekelezeka kwa CCM.... bali zinazotekelezeka ikiwa chama tawala kimeamua kweli kufanya kazi iliyowapeleka madarakani..?? ......Hivi sera ya elimu bure kwa kila mtanzania kwa elimu ya lazima ya hadi kidato cha sita; sera ya CHADEMA ni kweli CCM inaona haitekelezeki?
SWALI: Hivi uongo huu wa wazi wazi wa CCM ni kwa sababu wanahisi wamefanikiwa kuwafanya watanzania wasiwe na uelewa wa mambo kwa kuwa wamewanyima elimu kwa makusudi. Hapa naweza kuuandika msemo wa kweli kabisa 'ujinga wa watanzania ndio mafanikio ya CCM'
KWA KUJINADI KWA NAMNA HII CCM JE INAJIANDAA KUWA CHAMA CHA UPINZANI, KUIBA KURA AU KUINGIA MSITUNI?