Binafsi nimekuwa nikishangazwa na kelele za ukabila na udini unaopandikizwa na CCM kwa CHADEMA bila ya kufahamu lengo lao, sasa ndiyo naanza kupata picha.
Kwa jinsi inavyoelekea CCM wanaweza hata kuanzisha kampeni dhidi ya kundi fulani la wananchi kama wanavyowa demonize watu wa eneo fulani kwamba eti hawastahili kupata nafasi katika uongozi wa nchi hii!
Sijui ni wapi walikoichukua falsafa hii ambayo ni kinyume kabisa na ya mwasisi wao Hayati Nyerere.
Namaliza kwa kusema kama mmoja alivyochangia humu, Time will Tell.