CCM inakuwaje Askari wetu wa Uhifadhi wanakosa nguo na vifaa vya uhakika hadi kufikia kuvaa kama vikosi vya Waasi/ Askari wa DRC?

Soma uzi basi na uuelewe
kwani umeona sijasoma? Haya basi ngoja nitoe maoni. Inawezekana menejimenti ya hiyo taasisi ni mbovu na mkuu wao hana akili nzuri kiasi cha kutokuona mavazi ya askari wake yakoje
 
Mitumba ipo, wakanunue ile mitumba wanayokataza raia wasivae. Ipo ya kichina, kimarekani, kivietnam, nchi za kiarabu wakaokoteze huko kama wanashindwa kupata proper uniform. Kuvaa gambuti za shambani ni nzito na huchanika haraka
 
Mitumba ipo, wakanunue ile mitumba wanayokataza raia wasivae. Ipo ya kichina, kimarekani, kivietnam, nchi za kiarabu wakaokoteze huko kama wanashindwa kupata proper uniform. Kuvaa gambuti za shambani ni nzito na huchanika haraka
Kweli kabisa zile buti za kijeshi nzuri kama wanazovaa majeshi ya uarabuni zimejaa Kariakoo kama uchafu. So it seems zinaweA kupatikana za kutosha tu kwa ajili ya hawa askari wetu wakiamua kuwa nadhifu.

Sijui kwa nini wanawaza kuiba hela tu bila kuwahali hata kivifaa na mavazi askari wetu.
 

kwa habari ya uvaaji na mavazi kila mtu anayo namna yake anayopenda yeye na ndiyo maana hata mavazi yooote duniani hayawezi fanana na hata uniforms sehemu za kazi hazifanani kutoka idara hadi idara nyingine kama zinavyotoutiana idara zenyewe na hata mavazi yake yanatofautiana.
na kitengo hiki unachoona kwamba hakijavaa kwa namna ya kukufurahisha ww kinaye anayependezwa na uvaaji wao na zaidi ya hapo wanayo pia idara yenye kuhusika na kusimamia unadhifu pamoja na nidhamu.
ama wewe utuambie walipaswa kuvaa nini cha namna gani na wakati gani?.
na usisahau kwamba kazi yao inahitajika sana utaalamu wa kupambana na hao wanyama kuanzia namna ya uvaaji na hata kutembea kwao na silaha gani zinatakiwa kutokana na aina ya mnyama/wanyama wanao-deal nao kwa wakati huo hii ni kuanzia mavazi na hata silaha zipi zinahitajika kuhusika.
ila kama wewe unafahamu namna yao hao askari wanyama pori namna uvaaji na namna ya kutenda kwao kazi basi niseme ni vizuri umewashauri nikiamini kwamba watakuwa wamekusikia na watayafanyia kazi mkuu!
 
Pesa zote wanapeleka kulipa wasanii na machawa ili wawapigie promo wabaki madarakani, na kulipana maposho na per diem na kuagiza ma V8 na kula kwa urefu wa kamba zao, hawana muda na hao maaskari
 
Umetoka kijijini lini kwenda mjini? Na una elimu gani?
 
Ndo hapo sasa. Hela zote wanazipiga kina Doto Magari na Wasanii!

Zingine zinaenda kulipia magori ya Simba na Yanga.

Kweli CCM laana.
Dotto magari na magori ya simba na yanga kwa uwandishi huu hatuna imani kama unajua lolote ktk tasnia ya uongozi
 
Ndo wavae mabuti ya wakulima?

Huko kuishi vizuri kwa nini wasitumie hizo hela kuwanunulia protective gears sahihi na nzuri?

We angalia askari wa Congo hapa wana tofauti gani na hawa wetu?
View attachment 3246112
Wanazo ila wanapenda gun boots kwa issue za maji na matope Kenya ni semi arid areas so kuko kame kuliko kwetu
 
Wanavaa vibaya. Wanaweza pewa uniform mpya lakini wanaamua kuvaa za zamani ili zikichafuka porini isiwe nongwa. Mpya zinavaliwa kukiwa na ugeni mzito.
Umeshawajibu hata yy kwake anakunywa chai kikombe kilichobenyuka ila wakija wageni hasa wakazini set mpya ya vyombo inatolewa
 
Kwa hiyo ni sawa askari wetu kuvaa mabuti ya wakulima we kilaza wa kijani?
Hizo buti za wakulima (Gambuti) zinavaliwa na majeshi yote au watu wote hasa sehemu zenye matope na madimbwi ya maji

Kuvaa hivyo haimaanishi hawana buti nzuri

Gambuti zinapendwa kwa sababu ya kustahimili matope na maji

Mkoani kigoma hasa kasulu Gambuti ni sale rasmi ya shule siku za mvua

Mashirika kama
Word vision
Good neighbors
Medical team
IRC
Wanavaa Gambuti pia wanapokuwa field
 
Simiyu kuna mvua?
 
Acha kuongea ujinga wewe. South America kwenye mvua na matope umewahi ona majeshi yao yakivaa gumboots?
 
CCM ni janga pesa wanakula wachache sana Katika nchi hii ,Ata magereza sare zao wanaweka viraka tu..
 
Umetoka kijijini lini kwenda mjini? Na una elimu gani?
asante sana kwa maswali yako haya.lakini kabla sijakujibu ningeomba kufahamu ili niweze kukujibu vizuri.je maswali yako haya yanahusiana vipi na mada iliyoko mezani? na kama hayana uhusiano wa moja kwa moja na mada tunayojadili basi tujikite kwenye mada ili tuweze kueleweshana na kufikia muafaka mzuri.
 
Kazi kweli kweli...
 
Halafu kwanini wasiwe wanawachukua vipimo ndo wanawashonea nguo zinazowatosha badala ya kuwavalisha ma over size hayo au mabuga hayo........!
Hiyo mbinu ya kijeshi PORINI hutakiw kupendeza unatakiwa ufanane na JANGIRI UNAWAJUWA MAJANGIRI WW AU unazani JANGIRI anayeenda kuimba pembe za farunna meno ya Tembo anafanana na panya road wa mikoa yenu
 
Inaonekana unasumbuliwa na ushamba pamoja na kukosa exposure
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…