CCM inapoteza Msingi Mkuu wa Dira yake na nguvu yake

CCM inapoteza Msingi Mkuu wa Dira yake na nguvu yake

Pang Fung Mi

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2022
Posts
6,653
Reaction score
13,919
Shalom,

Ni ajabu sana siku hizi huwezi kusikia kauli kama serikali ya CCM, utekelezaji wa ilani ya CCM, serikali imeleta.

Utasikia kauli za kipumbavu kwamba Rais amefanya, Rais ameleta upumbavu mtupu.

Rais ni mwajiriwa, mtumishi, mwakilishi wa CCM, pesa yoyote ile sio yake ni ya nchi, ni ya serikali.

CCM inakosa umaarufu, badala yake Rais anatamkwa utadhani ameingia madarakani kama mgombea binafsi ni aibu sana.

Ni hayo tu.

Wadiz
 
Ni sahihi pesa Hizo ni kodi zetu, kodi za mama zetu na babu zetu na bibi zetu na Kaka zetu. Wamezigeuza kama za kwao
 
Mama Samia mimi namkubali, kwa vile amesahihisha mengi mabaya ya mtangulizi wake.

Lakini hili la kusema mama Samia katoa fedha kufadhili hiki au kile , ni kama ujinga fulani kwa yule anayesema hivyo.

Hela yote inatokana na kodi za wananchi, na ndio wanaotoa fedha zote kupitia kodi zao.

Ukina kiongozi anasema mama Samia katoa hiki/kile ujue mbumbumbu huyu uchawa unamsumbua, hata awe kiongozi wa ngazi yoyote.
 
Ndio hayo tu namshukuru mama kwa kuweza kutype kwa amani mpaka muda huu!
 
Mimi naunga mkono mambo mengi aliyofanya MAGU lkn Kwa hili la rais kafanya miongoni mwa mambo ambayo hayakuwa sawa na Kwa nguvu zake za utawala angelizuia lingekufa kabisa,rip mzalendo MAGU.
 
Ujinga huo uliasisiwa na dola the state has a pale walipoihakikishia ccm itatawala milele kwa katiba mbovu kabisa!!wamejipa kazi kubwa Sana kama watataka kubadili Hali iliyopo coz wamejifunga kisheria na kikatiba!Rais na mwenyekiti wa CCM hawezi wajibishwa Kwa Sheria hizi Wala katiba hii bali kwa ugonjwa ama kifo!!Dola imejiingiza kwenye mtego mkubwa Sana Haina namna zaidi ya Damu ya muhusika kama muhusika ataenda kinyume na matakwa yao!!!

Huo ndio ukweli mchungu sana ambao Dola inauishi!!!

Ccm ingekua inapumzishwa kushika Dola kama America walau ingepata muda wa kujitathmini na kuwajibika kwa wananchi!lakini kwa kiburi hiki na uchawa huu ni njia Moja TU inaweza kutumia sio nyingine ni kiwaua makada tu !kuanzia mwenyekiti Hadi wastaafu wenye influence na ufisadi nchini

So sad!!
 
Back
Top Bottom