Utangulizi.
Ukoloni unatambulika kama sera ya taifa moja kulikalia kimabavu taifa linguine na kusimamia shughuli za kisiasa kwa kupitia walowezi, huku likipora rasilimali na/au kuwafanyia wananchi wa nchi wenyeji unyonyaji wa kiuchumi.
Japokuwa ukoloni umekuwepo enzi na enzi, ukoloni tunaousoma kwenye vitabu ni ule ulioshamiri kuanzia karne ya kumi na tano, uliochochewa kwa kiasi kikubwa na kiu ya kutafuta vito vya thamani, madini na malighafi zilizohitajika viwandani huko Ulaya.
Sababu mbalimbali zinatajwa kama vichocheo vya ukoloni, lakini zifuatazo zinaorodheshwa na wanahistoria kama sababu kuu za ukoloni.
(a) Sababu za kisiasa.
Wafalme wa nchi za Ulaya walikuwa wakikabiliwa na kizazi kilichoelimika Zaidi na chenye kuhoji uhalali wa kuendelea kutawaliwa kwa mfumo wa kifalme.
Wafalme walitumia mbinu za kuwahamishia kwa lazima wanaharakati, wahalifu na wapinzani kwenye makoloni yao.
(b) Sababu za kiuchumi.
Kutokana na ongezeko la watu na ufinyu wa rasilimali, raia wengi walihamasika kuhamia kwenye makoloni wakiamini kuwa wangepata fursa za kuendelea kwa haraka.
(c) Sababu za kidini.
Waprotestanti wengi walikimbilia kwenye makoloni hawa “New World” Amerika Kaskazini baada ya kunyimwa uhuru wa kuabudu walivyotaka.
Baadhi ya makanisa yaiona fursa ya kueneza dini kwa watu wa mataifa kupitia mwanya huu wa ukoloni.
Serikali za wazungu ziliamua kuitumia njia ya kuwatuma wapelelezi maeneo mbalimbali ya dunia wakati mwingine wakiambatana na makanisa ili kupata uelewa wa maeneo ya kujitwalia kama makoloni mapya.
Mbinu zilizotumika kuendeleza ukoloni.
Mbinu mbalimbali zilitumika na wakoloni ili kuendelea kuyashikilia makoloni yao hata pale ilipokuwa wazi kuwa muda wa kuziachia hizo nchi zijitawale ulikuwa umefika.
Hapa nitaainisha mbinu hizi kwa ufupi kisha nitaelezea mfanano wa mbinu hizi na zile zinazotumiwa na serikali za CCM hasa awamu hii ya tano.
(i) Matumizi ya mabavu kupitia vyombo vya dola.
Watawala wa kikoloni walipoona upinzani unazidi, walikimbilia matumizi ya mabavu na vyombo vya dola kuwasakama wote waliokuwa wanatoa sauti tofauti kwa raia.
Walianzisha kampeni za vitisho, mauaji ya wanaharakati na raia, kuwasweka magerezani wapinzani wa ukoloni, na kadhalika.
(ii) Matumizi ya propaganda.
Propaganda inatafsiriwa kama juhudu za makusudi za serikali zinazolenga kuathiri tabia, mitazamo na mienendo ya watu au makundi ya watu (mfano, makabila, vikundi vya dini, nk), kwa matarajio kuwa makundi hayo yatabadili mienendo, tabia au mienendo dhidi ya serikali.
Propaganda hizi zilienezwa hasa na vyombo vya habari (magazeti na redio) na kupenyezwa kwenye mifumo ya utawala walioutumia (mfano kuwatumia viongozi wenyeji kueneza propaganda).
Propaganda za kikoloni zililenga kuwaaminisha watu, hasa raia wa kawaida kuwa mfumo wa ukoloni ndio mfumo pekee unaowafaa, na kinyume na huo ni machafuko na mauaji.
(iii) Kuwagawa watu kimakundi na ubaguzi.
Tawala za kikoloni zilitumia njia ya kuwatofautisha watu kimakundi. Mfano, kuwatambua watu kwa misingi ya randi au asili zao, kisha kuwapa haki kwa misingi ya ubaguzi.
Mfano, mzungu anakuwa juu ya wote kama mtawala asiyehojiwa popote. Akiwa na haki zote za kumiliki, kupora, kuua, kubaka, na kutawala chochote anachokutana nacho bila kuhojiwa na yeyote isipokuwa kwa watawala wa serikali inayomiliki koloni husika.
Kundi lingine la wahamiaji hasa waasia waliokuwa na haki kiasi za kumiliki kiasi cha ardhi, kufanya biashara nk.
Kundi la mwisho ni la watawaliwa ambao walichukuliwa kama wanyama wa porini, wasiokuwa na hakiyoyote, isipokuwa kutumiwa kwa manufaa ya watawala.
Mfanano wa mbinu zinazotumiwa na CCM na mbinu za kikoloni.
Kwa muda sasa tumeshuhudia serikali za CCM zikiendelea kupoteza uungwaji mkono kwa wananchi.
Sababu kuu ikiwa ni kutoonekana maendeleo ya kweli na mabadiliko ya maisha ya watu hasa wanapojilinganisha na mataifa mengine, hata yale yasiyokuwa na rasilimali tulizonazo.
Kwa muda mrefu, bado watu wanasumbuka na mambo madogomadogo ya kukosa huduma za maji masafi, kukosekana kwa elimu duni mpaka inafikia kuwa mtu akisomea nje ya nchi anatukuzwa kuliko aliyesomea hapa hapa nyumbani, uduni na ukosefu wa ajira, serikali kuingilia na kuwabana wananchi wa kawaida kama vile kuchukua kwa bei chee mazao yao ya kilimo, kutoza kodi kubwa kwa wafanyakazi, kutoza kodi kubwa zisizo na uhalisia kwa wafanyabiashara na kadhalika.
Kukataliwa huku, kumezisukuma serikali za CCM hasa awamu hii ya tano kukimbilia mbinu za kikoloni kuendelea kutawala.
Tutizame tena mbinu hizi nilizoziainisha hapo awali na namna zinazofanana na zile za wakoloni.

Serikali za chama cha mapinduzi kadiri upinzani unazidi kuimarika, tunashuhudia serikali na chama cha mapinduzi walikimbilia matumizi makubwa ya mabavu na vyombo vya dola hasa polisi na pale inapoonekana hatari, kuliingiza jeshi.
Vyombo hivi ni wazi kuwa vinatumika kuwasakama wote wanaotoa sauti tofauti na serikali kwa wananchi.
Wameanzisha kampeni za vitisho, utekaji, mauaji ya wanaharakati na raia, kuwasweka magerezani viongozi wa vyama vya upinzani, kuzuia mikutano halali na sasa wamefikia kuzifanya shughuli zote za siasa za vyama vingine isipokuwa CCM kuwa haramu.
Tunashuhudia polisi na vyombo vya usalama kufanya kazi mithili ya tawi la kijeshi la chama cha mapinduzi (green-guard).
(ii) Matumizi ya propaganda.
Kama tulivyoona hapo awali, propaganda ni juhudu za makusudi za serikali zinazolenga kuathiri mitazamo, mienendo, na tabia za watu dhidi ya serikali.
Sote tunashuhudia matumizi ya propaganda kwa makundiya watu mbalimbali. Tulianza kuona propaganda dhidi ya vyama vya upinzani, baadhi ya makabila hasa ya kaskazini, propaganda dhidi ya waliokuwa wanataka haki za kitaifa kwa Zanzibar, nk.
Serikali za CCM imeviteka vyombo vya habari na magazeti, kisha kuendesha vitisho kwa vyombo vilivyo huru, visivyofungamana na serikali au chama cha mapinduzi.
Tumeshuhudia wanahabari kuandamwa hasa pale wanapotoa maoni tofauti. Baadhi ya wanahabari wamekamatwa na kupewa kesi za uhujumu uchumi, wengine wamepokea vitisho, na wengine wamepotezwa kabisa.
Propaganda za awamu hii zimekuwa mbaya kuzidi zile za kikoloni. Propaganda hizi kama zilivyokuwa za kikoloni, zinalenga kuwaaminisha wananchi kuwa ni chama cha mapinduzi pekee ndicho chenye haki ya kutawala, na kinyume na huo ni vita, machafuko na mauaji.
Kila mara Rais anapoongea demokrasia na utawala bora huishia kuwaasa wananchi waendelee kuichagua CCM ili amani iendelee kudumishwa.

Kaka ilivyokuwa kwa tawala za kikoloni, serikali za CCM nazo zimeichukua mbinu hii ya kuwagawa wananchi kimakundi.
Mfano, serikali na chama cha mapinduzi wanafanya juhudi kubwa kupandikiza ubaguzi wa kiitikadi, kivyama, na wakati mwingine hata kiimani.
Wananchi ni sisi wamoja, na jambo pekee linalopaswa kuletwa na wanasiasa ni mustakabali wa taifa letu, namna bora na mfumo bora wa kutuletea maendeleo nk.
Lakini cha kushangaza CCM na serikali huja na hoja kuwa ni chama hiki au kile, ni kabila hili au lile, badala ya kuongelea ubora wa elimu au huduma za jamii, au ajira.
Mgawanyo huu pia huhamishwa na kuwatupia lawama hata watu wa nje huko na kuwaita mabeberu kuwa ndio wahusika wanaokwamisha serikali isiweze kuboresha huduma, hata kusambaza maji.
(iv) Kupora mamlaka ya maamuzi kwa wananchi.
Mara baada ya uchaguzi ambao wengi bado wanaamini aliyesimamishwa na muungano wa upinzani alishinda, CCM na serikali imejikita kuwapora wananchi haki yao ya kuamua waongozwe na nani. Ilianzia kule Zanzibar, ambapo kura za urais wa muungano zilionekana hazina dosari, lakini zile za urais wa Zanzibar pekee ndizo ziliharibika na kilazimisha uchaguzi wa Zanzibar pekee kurudiwa.
Kuanzia hapo, serikali na CCM ilikosa imani na wananchi. Iliamua kuwapora hata ile haki ya kuchagua waongozwe na nani.
Serikali na CCM huamua kabisa mtu wanayemtaka, kisha huwahadaa wananchi kwa kuitisha uchaguzi feki, ambao matokeo hutengenezwa kinyume kabisa na karatasi za kura.
Wananchi walipoona hakuna maana ya uchaguzi, mwaka huu 2019, waligomea hata kujiandikisha kupiga kura.
Serikali ikajilazimisha kuongeza muda ili kurekebisha pale walipokosea na kutengeneza waandikishaji feki kwa mamilioni.
Walipoona vyama vikishiriki hawana uhakika kama wananchi hawatawachagua, wakawaengua mapema kabisa kisha kujitangazia uchaguzi feki wa kupitisha majina ya CCM.
Hiki ni kiwango ambacho hata hatukukisikia kwa wakoloni. Hata mwalimu Nyerere, pale alipokosekana mpinzani, aliitisha kura za ndiyo au hapana. Lakini awamu hii imeamia kuondoa hata ile sauti ya kusema ndiyo au hapana.
Serikali ya awamu hii inawachukulia wananchi mithili ya wanyama wa porini wasiokuwa na uwezo wa kutambua chochote.
Imekosa imani kwa wananchi, inajihami, inapora, inaua, inateka, na ni wazi kuwa ipo tayari kuendeleza vitendo hivi vya kinyama kwa wananchi.
Hitimisho
Ni dhahiri kwamba mambo mengi yanayoendelea kufanywa na serikali ya chama cha mapinduzi ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli, imechukua kwa kiasi kikubwa na katika maeneo mengine kuzidisha mbinu zilizotumiwa na wakoloni kuendelea kutawala.
Mbinu hizi zimeonekana kuwa ndizo muafaka baada ya serikali na chama cha mapinduzi kukosa uungwaji mkono wa raia “Popular Mandate” maeneo mengi ya nchi.
Ni wajibu wetu kama wananchi halali wa nchi hii, tunaotarajia kuwa na historia ya kudumu kwa nchi hii, kuendelea na mapambano na vita ya kuirejesha nchi katika utawala wa haki na ustaarabu.
Mbinu hizi za kikoloni ni lazima zipingwe kwa nguvu ileile iliyotumika kuuondoa ukoloni nchini. Tuzidi kupasa sauti zetu dhidi ya mbinu za kikoloni zilizochukuliwa na serikali na chama cha mapinduzi.
Tuwaunge mkono wanaoongea kwa ajili yetu, na tuwape nishani ya ushujaa wale wote wanaojitoa mhanga kusema, tukijua kuwa hatma ya taifa letu lenye maendeleo, demokrasia na haki ipo mikononi mwetu.
Sote hatutamani siku chuki itakapojaa
miongoni mwetu kwa ghilba za chama cha mapinduzi na serikali tuanze kuuana. Sote tunaitamani nchi yetu, yenye maendeleo, demokrasia, uhuru, amani na mshikamano.
Wote wanaoamini kuwa wataigawa nchi hii kwa mbinu za kikoloni watashindwa, na wataondoshwa kama walivyoondoshwa wakoloni.
“No force shall prevail against our resolve, if we so desire to have a prosperous nation”
Nawatakia jumapili njema.