Tetesi: CCM inawabebembeleza iliowafukuza!!

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
21,470
Reaction score
40,593
Habari toka ndani ya CCM zinaeleza kwamba baadhi ya wanachama wa chama hicho waliofukuzwa, wameelekezwa kuandika barua za "kuomba msamaha" ili chama hicho "kiwasamehe" na kuwarudisha tena CCM.

Taarifa hizo zinadai kwamba zoezi hilo linafanyika kwa baadhi ya wanachama hao kuelekezwa kuandika barua na nini cha kuandika kwenye barua hizo na kisha hujadiliwa na kamati ambayo Mwenyekiti wake ni Mzee Philip Mangula na kufikishwa kwa Mwenyekiti wa CCM Taifa na kisha wanachama hao "kusamehemewa" kupitia kikao cha Halmashauri Kuu.

CCM kwa maigizo, mnampiku hata Mzee Majuto!!
 
Sio CCM hii, labda Ile ya 2015 kurudi nyuma, CCM mpya chama kwanza, mtu baadae
Wewe una uhusiano hata na kiongozi yeyote yule aliye karibu na Mzee wa Mangula umuulize kama Jumatano ya wiki hii hawajapokea Barua toka kwa waliofukuzwa?

Halafu hii kaulil mbiu yenu ya chama kwanza mtu baadaye si mnayo miaka yote, leo imekuwaje mpya?
 
Mkuu kaa kimya tu, wale madiwani waliohama kule Hai kwa Mbowe, barua zao za kujiuzulu zilikuwa na maudhui sawa ila wakajichanganya kwenye majina. Wakati ule ndio ilikuwa hii project ya nunua wapinzani pazia la usajili limefunguliwa. Sasa hivi hii inayoitwa ccm mpya sterling ni babayenu naye anacheza siasa za kishamba ile mbaya. Bora hata hiyo ccm ya kabla ya 2015 wagombea wa uchaguzi wa ubunge walikuwa wanapatikana kwa ushindani, na sio hii mpya wahamiaji wanakuja na kupewa nafasi, waliofia chama wanabaki kupamba majukwaa ya kuwapokelea akina Msando na kina Kafulila, na kuishia kupeleka viongozi kwa waganga kuvuta nyota ya cdm iende ccm.
 
kweli kabisa siasa za kishamba chakubanga na bichwa washamba kwelikweli
 
Habari toka ndani ya CCM zinaeleza kwamba baadhi ya wanachama wa chama hicho waliofukuzwa, wameelekezwa kuandika barua za "kuomba msamaha" ili chama hicho "kiwasamehe" na kuwarudisha tena CCM.

Taarifa hizo zinadai kwamba zoezi hilo linafanyika kwa baadhi ya wanachama hao kuelekezwa kuandika barua na nini cha kuandika kwenye barua hizo na kisha hujadiliwa na kamati ambayo Mwenyekiti wake ni Mzee Philip Mangula na kufikishwa kwa Mwenyekiti wa CCM Taifa na kisha wanachama hao "kusamehemewa" kupitia kikao cha Halmashauri Kuu.

CCM kwa maigizo, mnampiku hata Mzee Majuto!!
Sofia simba tayari bado Madabida na Stela Msambatavangu,
kumbe zile zilikuwa drama tu
 
Sio CCM hii, labda Ile ya 2015 kurudi nyuma, CCM mpya chama kwanza, mtu baadae

Ni kweli wanafanya hivyo, kwasababu, CCM inamuhitaji sana Sofia Simba Kuliko Sofia Simba anavyoihitaji CCM. CCM haiwezi kuikaribia CHADEMA NA CUF Dar bila Sofia Simba. Halikadhalika kwa LOWASA, Nchimbi na na na....

Kwa mantiki hiyo sasa hivi Mwenyekiti anaambiwa kuwa alifanya kosa kubwa kuwafukuza wanachama wakongwe wenye mvuto. Ameombwa hata kutojenga uhasama na wafanyabiashara.

Mzee kaanza kusikiliza ushauri.

Ila safari hii hata kama akimrudisha Lowasa CCM NYUMBANI KWAKE NI KABURINI. Ni polisi na Jeshi ndio wenye uwezo wa kuibakisha CCM madarakani sio nguvu za wananchi.
 
Wewe una uhusiano hata na kiongozi yeyote yule aliye karibu na Mzee wa Mangula umuulize kama Jumatano ya wiki hii hawajapokea Barua toka kwa waliofukuzwa?

Halafu hii kaulil mbiu yenu ya chama kwanza mtu baadaye si mnayo miaka yote, leo imekuwaje mpya?
Kumbe kupokea barua ndo tatizo, acha uvivu wa kufikiri , kama wameanfika barua wanayo haki ya kusikilizwa so kama imekuumiza ukaamua kutunga habari basi hilo ni tatizo lako binafsi, usiwagawie wenzako hapa
Eti wamebwmbelezwa waandike barua,nao wakakubali?
 
Sio ccm hii anayoiyongoza Rais magufuli ccm ya sasaiv ikoimara sana na hatuwabembelezi wanakuja wenyewe baada ya kuona kaz nzuri inayofanywa na Rais
 
Back
Top Bottom