Mkuu kaa kimya tu, wale madiwani waliohama kule Hai kwa Mbowe, barua zao za kujiuzulu zilikuwa na maudhui sawa ila wakajichanganya kwenye majina. Wakati ule ndio ilikuwa hii project ya nunua wapinzani pazia la usajili limefunguliwa. Sasa hivi hii inayoitwa ccm mpya sterling ni babayenu naye anacheza siasa za kishamba ile mbaya. Bora hata hiyo ccm ya kabla ya 2015 wagombea wa uchaguzi wa ubunge walikuwa wanapatikana kwa ushindani, na sio hii mpya wahamiaji wanakuja na kupewa nafasi, waliofia chama wanabaki kupamba majukwaa ya kuwapokelea akina Msando na kina Kafulila, na kuishia kupeleka viongozi kwa waganga kuvuta nyota ya cdm iende ccm.