MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 21,387
- 44,030
Kutokana na wanaCHADEMA kuwa mstari wa mbele kupinga na kukosoa mambo mbalimbali yanayoendelea wakati huu wa uchaguzi ninashauri chama chetu CCM kiwape hawa ndugu zetu nafasi maalum ya kupendekeza wagombea wanaowataka. Imefika sehemu viongozi waandamizi wa CHADEMA wamejiunga na Polepole kusema hawamtaki mgombea urais wa CCM Dr Samia Suluhu kama vile akiwekwa mwanaCCM mwingine itawasaidia kupiga hatua kisiasa.
Tunajua kila mtanzania wakiwemo wanaCHADEMA, anatambua bila CCM imara nchi itayumba ila pia jaribuni kuheshimu maamuzi ya mkutano mkuu wa CCM. Mgombea urais tayari kashapatikana na hakuna namna ya kuurudia mchakato hivyo CHADEMA wajitahidi kabla ya 2030 kupendekeza mwanaCCM wanayedhani atakuwa Rais bora kwa nchi. Kwa sasa watanzania tunaenda na Mama Samia.
Najua CHADEMA pia mnafurahia uongozi wa mama ila mnayumbishwa na watu kama Polepole, Mange Kimambi, Maria, Dayon Monsoh na James Delicious. Kuweni na msimamo mumuunge mama mkono kwa kumpigia kura.