GE2025 CCM isimpe Mgombea huyu Jimbo la Sikonge, sababu ni hizi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Kayugumis

Senior Member
Joined
Jun 6, 2022
Posts
160
Reaction score
172

Wakati vuguvugu la mchujo wa wagombea ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) likizidi kupamba moto, mgombea ubunge wa Jimbo la Sikonge, amejikuta katika hali ngumu baada ya kufichuliwa kwa tuhuma nzito kuhusu mienendo yake, zilizotolewa na watu wa karibu.

Akizungumza na mwandishi wetu, mmoja wa watu wa karibu wa Mgombea huyo ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe—alisema kuwa moja ya makosa makubwa ambayo wananchi wa Sikonge wanaweza kufanya ni kumpitisha kuwa mbunge, kwani hana sifa wala maadili yanayostahili kiongozi wa umma.

“Huyu jamaa msimuone tu anavyotabasamu; sisi tuliomzoea tunamjua vizuri. Nimeamua kusema ukweli kwa sababu dhamira yangu hainiruhusu kunyamaza. ana tabia nyingi zisizofaa, ikiwemo kuchukua wake za watu bila haya, eti kwa sababu ana pesa! Amewaumiza watu wengi sana. Na suala la utapeli bado lipo—hilo halijawahi kuisha,” alieleza.

Aliongeza kuwa kipindi akiwa mbunge aliwahi kumtapeli mamilioni ya fedha mfanyabiashara mmoja, lakini kutokana na ushawishi wake wa kisiasa wakati huo, suala hilo lilifunikwa kimyakimya. “Sasa amerudi tena kwa gia mpya kutaka ubunge. Nawahurumia wananchi watakaomchagua. Tunaomba CCM isimpe nafasi watu wa aina hii kugombea uongozi,” alisema.

Mwanasiasa huyo aliwahi kukumbwa na kashfa ya kutuhumiwa kutapeli zaidi ya shilingi milioni 100—sakata ambalo liliwasilishwa hadi Ofisi ya Bunge jijini Dodoma na pia kufikishwa kwa Waziri Mkuu.

Katika tuhuma hizo, anadai kuwa mwaka 2008, alimshawishi kuingia ubia wa biashara ya kuagiza na kuuza pikipiki aina ya Dayun, pamoja na matairi na mipira ya ndani kutoka China, kupitia kampuni ya Oceanic Distributors Ltd, ambayo inaelezwa kumilikiwa na mbunge huyo.

Mgombea huyo alikiri kuwepo kwa madai hayo, lakini alisisitiza kuwa deni hilo linaihusu kampuni yake binafsi na si yeye kama mtu.
 
Unazijua Sheria walizojipitishia hapo juzi??, ni kwamba watamleta yule wanayemtaka wao yaani anayemtaka mwenyekiti ndiye atakayepitishwa hata kama wajumbe hawakumpitisha....kwahiyo kazi ya wajumbe imeporwa rasmi....mjumbe hana mamlaka ya kuchagua mtu wanayemuhitaji....bali mwenyekiti taifa ndiye atawaletea jina ili mumpitishe 😄😄
 
Duh mnachapiwa wake zenu
😄

Ova
 
😄
Acha waendele kuchapiwa tu

Ova
 
Huu ujinga tumeulea mpaka umekuwa kama kitu cha kawaida na sio kosa tena, na hili la mwenyekiti kujipa mamlaka kuchagua anayemtaka na si box la kura kuamua tunaongeza ugonjwa mwingine
 
Unazishauri Ngedere Zimkatae Na Kumtenga Ngedere Mwenzao Kwenye Msafara Wa Kwenda Kula Karanga Shamba La Bibi.
Kilio Chenu Labda Muungane Na NRNE.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…