Uchaguzi 2020 CCM isitarajie mno mteremko 2020

Uchaguzi 2020 CCM isitarajie mno mteremko 2020

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Bahati nzuri au mbaya flyovers, ujenzi wa barabara pana, ndege, na meli havijafika huku kwetu Nanjilinji hivyo sio rahisi watu kupiga kura kwa kushawishiwa na vitu Kama hivyo. Wao bado wanasubiri atakaewapelekea maji ya kunywa, barabara, masoko ya mazao yao, na pesa mifukoni mwao.

Wale waliokuwa nyuma ya Lowassa na kunyonga mikono yao wakati wa peeopooos sidhani Kama walirudi CCM pia wakati Lowassa na baadhi ya wabunge na madiwani waliporudi CCM kwa sababu tata hivi majuzi.

Kama Kuna mtu anasema kuwa upinzani hakuna sasa anaweza kuwa anamdanganya mheshimiwa.

Wako watu Tanzania hawaitaki CCM hata Kama mgombea wake atakuwa malaika, na wako ambao watauchagua upinzani hata Kama mgombea wake Ni shetani na kinyume chake.

Kuna watu wanaoamini kuwa bila upinzani wenye nguvu hata CCM haitatimiza ahadi zake kwa wananchi.

Kinachohitajika Ni free and fair election 2020
 
Back
Top Bottom