Uchaguzi 2020 CCM itashinda 2020 kwa 99%

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2014
Posts
24,501
Reaction score
28,711
Nianze kwa kutoa pole kwa viongozi wa upinzani na wanachama, kiukweli inaumiza sana, nchi haina demokrasia tena, hakuna tume huru hakuna ahueni kwa wagombea wa upinzani, mpaka sasa kwenye chaguz ndogo za udiwani, tayari CCM kwakushirikiana na tume ya uchaguzi ishafanya rafu amabapo karibu Madiwan 30 wa ccm washapita bila kupingwa wanasubiri kuapishwa, .Madiwani wa chadema na upinzan hasa, wanachofanyiwa hakiridhishi kwasisi wapenda haki, diwani wa chadema anaambiwa aandike neno ZINJANTHROPUS akishindwa tu anaambiwa Hajui kusoma wala kuandika, hivo hana vigezi, wa CCM anapitishwa bila kupingwa,

Kama mnakumbuka JIWE alishawahi kusema Haiwezekani Awachague wakurugenzi, wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa halafu wampitishe mgombea wa upinzani,

Na kwa uoga walionao viongozi, wateule wa bwana JIWE, sioni ni mkurugenzi gani, atawafanyia fair upinzani, anagalau wapite maana ikitokea Upinzani umepita kwenye eneo lako Itabidi uwajibishwe au kibarua kiote nyasi, kwa staili hii Naona Upinzani ukifa kibudu kama Viongozi na wanachama hawatachukua hatua madhubuti,

Kwasasa imekuwa kama maigizo, Chadema wamekuwa wakisusia uchaguz mpaka Kasoro zirekebishwe, lakin MA CCM hayarekebishi hata neno moja,

Chadema wanarud tena na kuanza kufanya uchaguzi, hawachukui hatua zozote, Tumeona yaliyotokea Siha, kinondoni, MA CCM yapo tayari damu imwagike ila wapinzani wasipate kitu.

Hii yote ni trela ya uchaguz wa 2020,

Naiona rafu kubwa ikichezwa hasa kwa wabunge nguzo za upinzani, naiona CCM ikijitangazia ushindi wa 99% hadi 100%

Tumeshaona Zitto akiandaliwa kisaikolojia atafute kazi nyingine, tumeona Msigwa akiwa njia panda na kuanza kujipelekapeleka ccm labda watamuhurumia, .

MBOWE KAMA MWENYEKITI CHUKUA HATUA MADHUBUTI, UPINZANI UNAULIWA MIKONONI MWAKO, MASHINJI UMEJIFICHA WAPI?
 
Hakuna chenye mwanzo duniani kikakosa kuwa na mwisho.......

CCM kutawala milele ni kukufuru uumbsji.........
 

I agree with your comments. Lakn nafkri ni shida kwa upinzani pia. kuna sehemu upinzani wanaonesha ulegevu kiasi fulani. Kwa mfano haingii aakilini kwa Tz kuwaweka wakurugenzi wa H/ mashauri/ miji / Mjiji kuwa ni wakala wa NEC kwa sababu ya kuonesha sura mbili na kuonesha loyalty kwa aliyemteua. Igizeni mfano wa zanzibar ambako wasimamizi wa uchagzui huomba kusimamia kwenye uchaguzi na sio kuwatumia wakurugenzi wa miji na H/ mashauri.
Inapendeza zaidi kama wasimamizi wakawa ni watu huru na ikiwezekana wasiwe watumishi wa serikali ili kuepuka vitimbi kama hivi tunavyoshudia wakifanyiwa wapinzani ktk uchaguzi wa madiwani.

Hapa wapinzani lazima wajitahidi kupaza sauti ili NEC iweke utaratibu maridhawa wakusimamia uchagzui na waache mara moja kuwatumia watendaji wa H/ mashauri. Kauli za mkuu wa kaya alizozitoa zinania ya kuwatisha watendaji wa H/ mashauri ili waendelee kubinya upinzani.
 
Huu utawala umejaa dhuluma. Naamini ipo siku watajutia matendo yao.
Sikubaliani na wewe kwa kulaumu utawala, mimi nawalaumu Watanzania. Ukimkuta mtu amechagua kwa hiari yake kuishi ndani ya nyumba chafu, hatakiwi kuanza kuwalaumu nzi, viroboto, kunguni na chawa...ajifunze tu kuishi nao kwani uchafu ndio mitaji yao.

Jenerali Ulimwengu alitupa usia...ukichagua hovyo usianze kulalamika hovyo unapotendewa hovyo. Ukilikoroga kwa kuchagua hovyo uwe tayari kulinywa hata likiwa chungu kiasi gani...kwetu Watanzania hizi tunazoziona kama dhulma ni rash rasha tu, za vuli ziko njiani kwani vichaa tunazidi kuwapa marungu makubwa zaidi kila siku!
 
Ikitawala milele hiv wewe unapata faida gani tueleze????
 
Mkuu, hivi tulichagua au kuna waliotuchagulia?
 
Mbowe atachukua hatua gani? Kumbuka bunge,mahakama,police,jeshi,magereza na tume ya uchaguzi vipo chini yao ndio maana wanafanya lolote walitakalo......demokrasia itakuwepo endapo magufuli atawaonea huruma wapinzani kinyume na hapo tusitegemee fair play

Ni bora tungekaa pembeni kwenye chaguzi hizi za kilofa
 
Na fair haipo
 
Ngoja tusubiri yajayo maana hata Mimi nimepanga kupiga kura
 
Mkuu huko Zanzibar akina JECHA walipindua matokeo ya uraisi juu-chini sembuse huu wa madiwani na wabunge?? Kwa kifupi huwezi kuwalaumu wapinzani huku kila muhimili upo chini ya ccm.
Katiba yenyewe ni magumashi usitegemee democracy nchi hii
 
Mkuu huko Zanzibar akina JECHA walipindua matokeo ya uraisi juu-chini sembuse huu wa madiwani na wabunge?? Kwa kifupi huwezi kuwalaumu wapinzani huku kila muhimili upo chini ya ccm.
Katiba yenyewe ni magumashi usitegemee democracy nchi hii
Hhaaaaa kweli walipindua juu chini
 
Kwani inashindana kinamna gani mpaka useme itashinda?
 
ushinda utakuwa zaidi ya 150%. kumbuka uchaguzu uliopita walio andikishwa kupiga kura walikuwa zaidi ya nusu ya raia wa taifa hili, lenye watoto zaidi ya nuru ya watu wote.
 
Natabiri...2020 Chadema inakufa kifo cha mende jike.
 
Iwaonee huruma watanzania sio wapinzani.
 
Yanayoendelea ni mipango endelevu yaliyoasisiwa na chama tawala, Kukubali vyama vingi 1992 ilikuwa ni cosmetics tu. Huwezi kuwa na vyama vingi na kuacha kurekebisha katiba ili kuruhusu chaguzi za kidemokrasia na mifumo ya kidemokrasia. Tofauti tu ni utawala ulipo madarakani basi. Katiba inaruhusu yote yanayotokea kwani kiongozi Mkuu wa inchi anaapa kuilinda katiba lakini vifungu kadhaa mbele kwenye katiba hiyo hiyo kinamruhusu kufanya vinginevyo. Katiba ndio chachu ya mabadiliko bila hilo basi inabidi nguvu mbadala zitumike ila sio nzuri wala rasmi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…