Uchaguzi 2020 CCM itashinda 2020 kwa 99%

Uchaguzi 2020 CCM itashinda 2020 kwa 99%

Natabiri...2020 Chadema inakufa kifo cha mende jike.
Sio jambo la kufurahia kwani inaposhindikana kwenye ballot box what next inabidi tuwemakini pia na hilo. Ni heri ayasemae hadharani kuliko kuishia underground. Vyama vilelewe vipaki hudharani. haya ni maoni tu.
 
Sio jambo la kufurahia kwani inaposhindikana kwenye ballot box what next inabidi tuwemakini pia na hilo. Ni heri ayasemae hadharani kuliko kuishia underground. Vyama vilelewe vipaki hudharani. haya ni maoni tu.
Ukweli mchungu tatizo Chadema siku hizi hata hoja za maana hawana wanasubiri mpaka Rais aongee ili na wao wapate cha kuongea.

Hali tete.
 
yaani tume ya kwako, uchaguzi unaandaa mwenyewe unashindwaje uchaguzi?
 
Huu utawala umejaa dhuluma. Naamini ipo siku watajutia matendo yao.
Tume itandelea kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sherif na si vinginevyo. kama una hoja yenye mashiko juu ya Tume nakushauri uchukue hatua kuliko kuendelea kubwabwaja maneno
 
Sikubaliani na wewe kwa kulaumu utawala, mimi nawalaumu Watanzania. Ukimkuta mtu amechagua kwa hiari yake kuishi ndani ya nyumba chafu, hatakiwi kuanza kuwalaumu nzi, viroboto, kunguni na chawa...ajifunze tu kuishi nao kwani uchafu ndio mitaji yao.

Jenerali Ulimwengu alitupa usia...ukichagua hovyo usianze kulalamika hovyo unapotendewa hovyo. Ukilikoroga kwa kuchagua hovyo uwe tayari kulinywa hata likiwa chungu kiasi gani...kwetu Watanzania hizi tunazoziona kama dhulma ni rash rasha tu, za vuli ziko njiani kwani vichaa tunazidi kuwapa marungu makubwa zaidi kila siku!
Mkuu Mag3 ni kwa vile kuna ukomo wa kutoa like lakini ningekupa elfu kabisa. Hapa utakuwa ujinga kuwalaumu watawala wakati mamlaka yako mikononi mwetu wenyewe. Watu wakionyesha wazi hawataki wanavyotendewa watawala wataamua eitha watumie nguvu kulazimisha ujinga wao au wananchi wafanye wwezalo kuwaondoa na wakishindwa hata msaada wa nje utatumika.
Sio aibu kupata msaada nje wakutoa kile ambacho hakitendi haki na wengi hawakitaki ila wachache wanatumia dola kulazimisha.
 
Good discussion but tujue mabadiliko ni lazima sio budi kujiandaa yasije kutudhuru, zama za ushindi wa kura umepitwa sasa ni kulazimisha ndio mwisho we era fulani, historia imetufunza hivyo kwa mataifa mengine. Hata watawala wamekuwa waoga hawadhubutu tena kuingia kwenye ushindani kwani viashiria vyote vimeshaonyesha umma unahitaji mabadiliko na upewe nguvu stahiki.
 
hakuna kazi ngumu kwa kiongozi mkuu wa inchi anapopewa jukumu la kuhakikisha chama tawala kinabaki madarakani. Hili jukumu ni gumu kuliko yote. Katika kuhakikisha hili ndio utaona nguvu nyingi hutumika na hata ufisadi mwingi tunapokaribia chaguzi kuu. This will repeat very after 5 years. Hii ni katika kijilinda kwa viongozi wanaotoka madarakani.
 
ccm lazima washinde kwa kishindo maana watapiga kura wenyewe itakuwa kama uchaguzi wa chama
 
Umesikia anayosema katibu mkuu wa CCM? Hiyo ndio hali halisi nachokiona nami nakiona, nimefurahi hataviongozi wetu wameona. Tunahitaji kugeuza mwelekeo na kuhuisha sera zetu ili chama kiuzike upya.
 
Nasikia yule mwalimu wa DS Dr Bashiru kawakumbusha ishu kali mno!

Jiwe atamla kichwa nadhani!
 
CHADEMA wewe umavumbi na mavumbini utarudi bwana alitoa na bwana ametwaaa jina lake libarikiwe. Hamina
 
Nasikia yule mwalimu wa DS Dr Bashiru kawakumbusha ishu kali mno!

Jiwe atamla kichwa nadhani!
But that is the fact for the party. Former presida, alieleza pia tusitegemee sana Police ili kupata ushindi. Nafikiri hawakumwelewa. Some reform should be done to make the level ground otherwise we are splitting the Country into pieces. Nakumbuka hata marehemu Kingunge alisema kabla hajaenda kwa Mola wake.
 
But that is the fact for the party. Former presida, alieleza pia tusitegemee sana Police ili kupata ushindi. Nafikiri hawakumwelewa. Some reform should be done to make the level ground otherwise we are splitting the Country into pieces. Nakumbuka hata marehemu Kingunge alisema kabla hajaenda kwa Mola wake.

Nakusoma mkuu....Ila Jiwe kuna wadudu wake kichwani wanamtumaga vitu vya ajabu sana..na hiyo itakua demise yake!
 
Nakusoma mkuu....Ila Jiwe kuna wadudu wake kichwani wanamtumaga vitu vya ajabu sana..na hiyo itakua demise yake!
Chama kimsaidie, kuongoza inchi na chama sii kazi rahisi sana, walipo kwenye chama wafanye kazi na kutoa ushauri stahiki utaokoa inchi isiingie kwenye machafuko. Uchaguzi wa Meya ilala ni dalili mbaya. Inabidi kifanyike kitu to address the situation, more and more will go into confrontation and that is not healt for the Country I repeat it again. Tujifunze kwa kila tukio linalojitokeza. Hata kivuko kilicho zama je kama inchi tumejifunza nini? Naona hela za michango zinajengea Dispensary why not doing something to deter future accident of similar nature.
 
Nianze kwa kutoa pole kwa viongozi wa upinzani na wanachama, kiukweli inaumiza sana, nchi haina demokrasia tena, hakuna tume huru hakuna ahueni kwa wagombea wa upinzani, mpaka sasa kwenye chaguz ndogo za udiwani, tayari CCM kwakushirikiana na tume ya uchaguzi ishafanya rafu amabapo karibu Madiwan 30 wa ccm washapita bila kupingwa wanasubiri kuapishwa, .Madiwani wa chadema na upinzan hasa, wanachofanyiwa hakiridhishi kwasisi wapenda haki, diwani wa chadema anaambiwa aandike neno ZINJANTHROPUS akishindwa tu anaambiwa Hajui kusoma wala kuandika, hivo hana vigezi, wa CCM anapitishwa bila kupingwa,

Kama mnakumbuka JIWE alishawahi kusema Haiwezekani Awachague wakurugenzi, wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa halafu wampitishe mgombea wa upinzani,

Na kwa uoga walionao viongozi, wateule wa bwana JIWE, sioni ni mkurugenzi gani, atawafanyia fair upinzani, anagalau wapite maana ikitokea Upinzani umepita kwenye eneo lako Itabidi uwajibishwe au kibarua kiote nyasi, kwa staili hii Naona Upinzani ukifa kibudu kama Viongozi na wanachama hawatachukua hatua madhubuti,

Kwasasa imekuwa kama maigizo, Chadema wamekuwa wakisusia uchaguz mpaka Kasoro zirekebishwe, lakin MA CCM hayarekebishi hata neno moja,

Chadema wanarud tena na kuanza kufanya uchaguzi, hawachukui hatua zozote, Tumeona yaliyotokea Siha, kinondoni, MA CCM yapo tayari damu imwagike ila wapinzani wasipate kitu.

Hii yote ni trela ya uchaguz wa 2020,

Naiona rafu kubwa ikichezwa hasa kwa wabunge nguzo za upinzani, naiona CCM ikijitangazia ushindi wa 99% hadi 100%

Tumeshaona Zitto akiandaliwa kisaikolojia atafute kazi nyingine, tumeona Msigwa akiwa njia panda na kuanza kujipelekapeleka ccm labda watamuhurumia, .

MBOWE KAMA MWENYEKITI CHUKUA HATUA MADHUBUTI, UPINZANI UNAULIWA MIKONONI MWAKO, MASHINJI UMEJIFICHA WAPI?
je wakishinda kwa asilimia wataongeza mishahara ya wafanyakazi wa umma na kupunguza kodi za uaguzaji magari?
 
Chama cha Mapinduzi kimejifunza mbinu za kushinda kwa asilimia 99 kutokwa kwa akina Sadam Hussein wa Iraq na Kim Jong Un wa North Korea.

2020 KUTAKUWA NA UCHAGUZI WA KUWACHAGUA MWENYEKITI WA CCM NA WAWAKILISHI WA NEC YA CCM.

VYAMA VYA UPINZANI NAVYO VIITISHE PARALLEL ELECTIONS ZA MUUNGANO WA UKAWA TUCHAGUE PEOPLE'S PRESIDENT WA UKAWA NA WAWAKILISHI WA MATATIZO YA WANANCHI WA UKAWA BILA KUITEGEMEA TUME HII YA UCHAGUZI.
WAO WAUNDE BUNGE LA CCM, SISI TUUNDE BUNGE LA WANANCHI LA UKAWA, WAO WAKIMUAPISHA RAIS, SISI TUNAMUAPISHA RAIS WA WATU WA UKAWA. HAPO NGOMA INAKUWA DROO.
 
Back
Top Bottom