Nianze kwa kutoa pole kwa viongozi wa upinzani na wanachama, kiukweli inaumiza sana, nchi haina demokrasia tena, hakuna tume huru hakuna ahueni kwa wagombea wa upinzani, mpaka sasa kwenye chaguz ndogo za udiwani, tayari CCM kwakushirikiana na tume ya uchaguzi ishafanya rafu amabapo karibu Madiwan 30 wa ccm washapita bila kupingwa wanasubiri kuapishwa, .Madiwani wa chadema na upinzan hasa, wanachofanyiwa hakiridhishi kwasisi wapenda haki, diwani wa chadema anaambiwa aandike neno ZINJANTHROPUS akishindwa tu anaambiwa Hajui kusoma wala kuandika, hivo hana vigezi, wa CCM anapitishwa bila kupingwa,
Kama mnakumbuka JIWE alishawahi kusema Haiwezekani Awachague wakurugenzi, wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa halafu wampitishe mgombea wa upinzani,
Na kwa uoga walionao viongozi, wateule wa bwana JIWE, sioni ni mkurugenzi gani, atawafanyia fair upinzani, anagalau wapite maana ikitokea Upinzani umepita kwenye eneo lako Itabidi uwajibishwe au kibarua kiote nyasi, kwa staili hii Naona Upinzani ukifa kibudu kama Viongozi na wanachama hawatachukua hatua madhubuti,
Kwasasa imekuwa kama maigizo, Chadema wamekuwa wakisusia uchaguz mpaka Kasoro zirekebishwe, lakin MA CCM hayarekebishi hata neno moja,
Chadema wanarud tena na kuanza kufanya uchaguzi, hawachukui hatua zozote, Tumeona yaliyotokea Siha, kinondoni, MA CCM yapo tayari damu imwagike ila wapinzani wasipate kitu.
Hii yote ni trela ya uchaguz wa 2020,
Naiona rafu kubwa ikichezwa hasa kwa wabunge nguzo za upinzani, naiona CCM ikijitangazia ushindi wa 99% hadi 100%
Tumeshaona Zitto akiandaliwa kisaikolojia atafute kazi nyingine, tumeona Msigwa akiwa njia panda na kuanza kujipelekapeleka ccm labda watamuhurumia, .
MBOWE KAMA MWENYEKITI CHUKUA HATUA MADHUBUTI, UPINZANI UNAULIWA MIKONONI MWAKO, MASHINJI UMEJIFICHA WAPI?