Ertugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 14,705
- 30,041
Kama msimamo utaendelea kuwa huu huu kwamba Uchaguzi utaendelea kama kawaida,hapana shaka Chama changu Ccm kitashika hatamu za Uongozi na kushika dola kwa miaka mingine mitano
Sina shaka kabisa kwamba pamoja na No Election No Reforms kampeni, bado hakuna anayeweza kuzuia uchaguzi usifanyike
Sawa uchaguzi utafanyika na Ccm itashinda,je hii Serikali itakuwa na taswira gani kimataifa?
Je ndio wakati umefika sasa nasi Tanzania tuonekane tunanyima uwepo wa demokrasia hapa nchini katika jumuiya za kimataifa?
Hapa uchaguzi bado lakini tayar kelele zimekuwa nyingi sana, vipi ukifanyika uchaguzi?
Nafahamu kabisa Chama changu pendwa mna hazina kubwa ya viongozi wenye maono na uelewa mkubwa,kwani miongoni mwa Vyama vikongwe kabisa barani Afrika Ccm nayo ipo
Sisi sio wakufundishwa siasa,kwasababu sisi ndio tulifundisha siasa na kusapoti harakati nyingi za nchi za Afrika kuweza kujitawala
Je, leo iweje kaka mkubwa awekwe chini tena kuambiwa hapa umekosea haikutakiwa iwe hivyo,hapana hatuja fikia bado,bado tuna mda wa kuweka mambo sawa
Wakati mwingine kukubali kufanya mabadiliko sio udhaifu na wala sio shinikizo bali ni kuonyesha ukomavu na ndio kukua
Tusikurupuke kufanya uchaguzi katika namna ambayo itaonekana hakuna ushindani wa kweli,maana hata ushindi wetu hautakuwa na uhalali kwa asilimia mia moja
Ni bora tukachelewesha Uchaguzi lakini uwe ni wenye ushindani na ambao hata tukishinda basi hakutakuwa na kuonyeshana vidole
Kidumu Chama Cha Mapinduzi
Ni hayo tu!