CCM jitahidini kuweka uwazi na uwajibikaji katika kodi za wananchi,nina sisitiza hakuna mbadala wenu.

CCM jitahidini kuweka uwazi na uwajibikaji katika kodi za wananchi,nina sisitiza hakuna mbadala wenu.

Mhafidhina07

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2014
Posts
3,340
Reaction score
4,659
uwajibikaji ni kitendo cha kutekeleza sera,sheria na utaratibu kwa uadilifu na uwazi,kuna faida kadhaa za kuwepo uwajibikaji naelezea kama zifuatavyo kujenga misingi imara ya uongozi,uadilifu,utekelezaji wa shughuli za kijamii na kuweka mfumo zuri kati ya serikali na wananchi,inapotokea serikali imekosea wananchi wanaweza kuiwajibisha au kuwaajibisha viongozi.

hakuna mbada wa mbegu isipokuwa ubora wa mbegu nyengine zote ni fake,kiuhalisia wananchi hawataki maendeleo makubwa ila wanahitaji sura mpya katika mfumo mkongwe,suala la wananchi kuwa pinzani kwa ccm haimaanishi kuwa chadema kina sera bora, ila wananchi wanatumia namna bora ya kulinganisha kwa kuwa ccm imekubali kujenga mfumo wa ulinganifu/upinzani.

madhaifu ya ccm ndiyo misingi imara kwa chadema,hivyo nawatanabaisha ccm kuchukua maoni ya chadema ili kuleta maendeleo endelevu kwa taifa la tanzania,si kila jambo la kuchukua mengine waachieni wenyewe.

kama serikali ya ccm itajenga mifumo ya wazi katika utekelezaji,ukusanyaji wa kodi kwa ufanisi sioni lawama za wananchi dhidi ya serikali.
 
Back
Top Bottom