CCM: Kamati Kuu Kukaa Chini Dar

Can we move on na masuala mengine?Kikao kimeshakwisha,na yaliyotarajiwa kuzungumwa hayakuzungumzwa.May be tusubiri Mkutano Mkuu wa CCM,or any other of its "extra-ordinary" meeting,mwakani!

One thing for certain is,I wouldnt miss my sleep expecting anything from a clique of fisadis...unless its about lies,and more lies,if not promises.
 
- The dataz ni kwamba kesho tarehe 29, kamati ya Secretariat itakutana kufuatia maagizo ya Kamati kuu, kuyarudia tena mafaili yanayohusu hoja ya makundi ndani ya CCM, na kamati kuu yenyewe itakutana tena tarehe 2, agenda ni moja tu, yaani makundi ndani ya CCM.

Respect.

FMES!
 
- Kamati kuu ya CCM, CC inatazamiwa kukutana tena tarehe 2, June yaani next week, inasadikiwa wkamba yatakayojadiliwa na pamoja na matayarisho ya uchaguzi mdogo wa bunge jimbo la Biharamulo,

- Pia CC itaendeleza majadiliano makali sana ambayo hayakumalizika kwenye kikao kilichopita mwezi uliopita, ambako wajumbe wengi wa kikao hicho nusura washikane mashati wakati wa kujadili muswaada wa makundi ndani ya CCM.

- Wajumbe wengi wa kutoka kundi la mafisadi wakiongozwa na Makamba, waliwajia juu wajumbe wa upande wa pili yaani wapiganaji kwa kuhusika na kukisambaratisha chama, infact kuna wajumbe waliokasirishwa sana na malumbano hayo na hata kuapa mbele ya kikao kwamba baada ya Busanda hawatajihusisha tena na shughuli za chama hicho hasa uchaguzi.

- Ni matumaini kwamba kutakuwa na habari mpya muhimu kwa masilahi ya taifa, katika kikao hiki muhimu sana kwa taifa, kama kawa tutazifuatilia sana kwa karibu sana habari za ndani ya kikao.

Respect.

FMES!
 
Mkuu FMES, hawa CCM ni WASANII TU hawana jipya na wala hakutakuwa na jipya lolote. Sasa hivi imebaki miezi 17 kabla ya October 2010 hawawezi kuja na jipya lolote maana sasa hivi ni mikakati ya 2010 tu, lakini haya yanayoliangamiza Taifa yatawekwa pembeni.

Walikuwa na miaka karibu minne ya kuyashughulikia matatizo mbali mbali hasa ya ufisadi ndani ya chama na Serikali lakini hadi hii leo hawajafanya chochote. Sidhani kama katika kikao cha June kutakuwa na jipya. Tusubiri labda wataamua kufanya kweli dakika za lala salama, lakini I doubt it!! Once a FISADI always a FISADI.
 
I think it should read this way:
- Ni matumaini kwamba kutakuwa na habari mpya muhimu kwa masilahi ya CCM, katika kikao hiki muhimu sana kwa CCM, kama kawa tutazifuatilia sana kwa karibu sana habari za ndani ya kikao.

For CCM to have meetings for constructive ideas for our NATION? No, they are planning for their SURVIVAL
 

Kaka umesomeka vizuri sana, msitari kwa msitari, neno kwa neno na hata hitimisho. Chungu kiko jikoni usiku huu (0223hrs EAT) na kuendelea hadi hiyo siku ya siku. Ila upo uwezekano wa kikao cha Kamati Kuu kufanyika Alhamisi Juni 4, 2009, ziku mbili baadaye kutokana na sababu za "kiufundi".
 
Ila upo uwezekano wa kikao cha Kamati Kuu kufanyika Alhamisi Juni 4, 2009, ziku mbili baadaye kutokana na sababu za "kiufundi".

- Mkulu Halisi nimekupata vizuri sana hapo, tupo pamoja ngoja niangalie dataz tena kwenye post.

Respect.

FMEs!
 


- Mkulu Bubu ninakusikia sana, lakini unafikiri wananchi wa Busanda wanaweza kukuelewa?

Respect.

FMEs!
 
tunasubiri wakulu warushe nyanga nzito,
 
tunasubiri wakulu warushe nyanga nzito,

- Mkulu samahani sana, toka juzi kumekua na mkutano wa National Business Council ambako rais alikuwepo huko sana, kwa hiyo kikao cha CC kilisogezwa na kitaanza kesho saa nne asubuhi, kwa hiyo samahani kwa usumbufu lakini kuna tetesi nyingi sana, na tetesi kubwa moja ni kwamba baada ya hiki kikao kuisha mambo hayatakuwa kama zamani tena, sasa sielewi how na where!

- Halafu pia kuna dataz za mashambulizi mazito na co-ordinated dhidi ya Mzee Mengi, na kuna mpaka waandishi wa habari tena wanaoaminika sana na taifa tayari wamenunuliwa na wanahusika na hiyo kampeni nzito sana, ndugu zangu tunaomuaminia huyu Mzee, huu ni wakati wa kumuombea sana tena sala nzito, maana something is up! Masikini ya Mungu ndiyo bongo yetu hii!

Anyways, by kesho tutakuwa na habari zaidi za kikao, tutaziweka kama kawa hapa JF.

Respect.

FMEs!
 
Ikulu yamuonya Reginald Mengi

*Yamtaka aheshimu vyombo vya dola
*Yasema athibitishe tuhuma alizotoa
*Yakanusha taasisi zake kumuandama
*Jeshi la Polisi latamka kumchunguza

Na Waandishi Wetu
SIKU moja baada ya mfanyabiashara maarufu hapa nchini, Reginald Mengi, kutoa madai mazito ya kuandamwa na baadhi ya viongozi wa serikali na taasisi za dola, Ofisi ya Rais Ikulu, imetoa tamko la kumuonya, ikimtaka aviheshimu vyombo vya dola.

Imesema Mengi anapaswa kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola ili viweze kufanyia kazi tuhuma za ufisadi alizozitoa katika vyombo vya habari dhidi ya wafanyabiashara watano kati ya kumi aliodai kuwa ni mapapa wa ufisadi hapa nchini.

Aidha, Ikulu imekanusha madai ya Mengi kuandamwa na baadhi ya viongozi wa kiserikali pamoja na taasisi zake, na kueleza kuwa, anapaswa kutoa ushahidi na vielelezo vya tuhuma alizozitoa dhidi ya wenzake, ili ziweze kufanyiwa kazi.

Msimamo huo wa Ikulu dhidi ya kauli za Mengi, ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, ulitolewa jana na Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi, Premi Kibanga, katika mahojiano maalumu na Tanzania Daima Jumatano kupitia simu yake ya kiganjani.

“Mengi anavyosema ameandamwa sasa, ameandamwa vipi? Alitoa sijui tuseme ndiyo kashfa au tuhuma za ufisadi, kwa hiyo ulikuwa ni wajibu wa vyombo vinavyohusika kumwita ili atoe ushahidi na vielelezo vyake ili viweze kufanyiwa kazi.

“Hakuitwa yeye tu, ameitwa pia Rostam Aziz, katika idara zote hizo. Hawa wote walitoleana kashfa za ufisadi na wote waliitwa ili watoe ushahidi wao. Sasa kwanini Mengi anasema ameandamwa?” alihoji Kibanga.

Akizungumzia kauli ya Mengi kuwa anamtegemea Rais Kikwete kumnusuru, Kibanga alisema kama anadai hivyo basi anao wajibu wa kumsaidia katika vita ya ufisadi.

Alisema anapaswa kutumia nafasi hiyo si tu kwa kuwataja mafisadi, bali pia kwa kutoa ushirikiano kwa vyombo vyote vya dola vilivyo chini ya Rais Kikwete, ili viweze kuufanyia kazi ushahidi wake na kuchukua hatua zinazostahili dhidi ya wahusika, ikiwa watathibitika kufanya ufisadi.

‘‘Vyombo vya dola havimwandami mtu. Na anaposema rais atamlinda, ni vema akaelewa kuwa Rais Kikwete ni rais wa wananchi wote. Rais Kikwete halindi mtu mmoja mmoja, analinda Watanzania wote.

‘‘Kama yeye ni rafiki wa Kikwete, basi autumie urafiki huo vizuri kama anavyofanya katika vita ya ufisadi. Lakini sasa asiishie tu katika kuwataja mafisadi, maana sasa kila mtu tu akitaja fulani fisadi kutakuwa na utulivu kweli? Yeye aviheshimu vyombo vya dola na amsaidie rafiki yake (Kikwete), kwa kuvipa ushirikiano vyombo hivyo,” alisisitiza Kibanga.

Naye Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Robert Manumba, alipohojiwa na gazeti hili kupitia simu yake ya kiganjani kuhusu madai ya Mengi kuandamwa na taasisi za dola, likiwamo Jeshi la Polisi, alisema anachojua ni kwamba, polisi wanamchunguza Mengi, lakini hawamuandami.

Manumba alikataa kuzungumzia suala hilo kwa undani, kwa maelezo kuwa msemaji wa jeshi hilo kuhusu suala hilo ni mkuu wa jeshi hilo, Inspekta Jenerali Said Mwema.

Gazeti hili lilipomtafuta Mwema kupitia simu yake ya kiganjani, ilipokelewa na msadizi wake ambaye alikataa kutaja jina lake na kueleza kuwa yupo katika kikao.

Hata hivyo, alipoulizwa kama anaweza kuzungumza lolote kuhusu madai yaliyoelekezwa kwa jeshi hilo na Mengi, alisema si madai ya kweli, kwa sababu jeshi hilo halina kawaida ya kufanya kazi zake kwa kumwandama mtu.

‘‘Hakuna chombo cha dola kinachomwandama mtu. Jeshi la Polisi linafanya kazi zake kwa mujibu wa sheria, kanuni na maadili yanayoliongoza, lakini kama unataka kupata taarifa zaidi kuhusu kinachofanyika kwa sasa, wasiliana na Kamishina wa Utawala na Rasilimali Watu, CP Clodwig Mtweve.

Kamishina huyo alipotafutwa, hakuweza kupatikana na simu yake ya kiganjani ilikuwa haipatikani.

Jumapili iliyopita, wakati Mengi akizungumza katika ibada iliyofanyika kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri la Kisereny wilayani Hai, mkoani Kilimanjaro, alisema baada ya kutaja majina ya mafisadi papa, alianza kuandamwa na baadhi ya mawaziri, vyombo vya dola na taasisi za serikali.

Huku akishangiliwa na umati wa waumini wa kanisa hilo lililopo katika eneo la kijiji alichozaliwa, Mengi alimtaja waziri wa kwanza kumwandama kuwa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Sophia Simba.Mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Hai, Dk. Norman Sigalla na Mbunge wa Hai, Fuya Kimbita (CCM).

Mengi alimtaja waziri mwingine aliyemwandama baada ya kutaja mafisadi papa kuwa ni Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, George Mkuchika, aliyesema alimwita mbaguzi wa rangi.

Alisema mbali ya mawaziri hao kutoa kauli hizo, pia wahariri wa magazeti yake anayoyamiliki, walihojiwa na Msajili wa Magazeti wa Idara ya Habari.

Huku waumini wa kanisa hilo wakiwa kimya, Mengi alisema yeye mwenyewe pia aliitwa na kuhojiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), ikidai alivunja sheria ya utangazaji kwa kutaja majina ya watu kuwa ni mafisadi papa, na kwamba hatua hiyo iliashiria ubaguzi wa rangi.

Mengi ambaye alikuwa mgeni mwalikwa kwenye hafla hiyo, alivitaja vyombo vingine vya dola vilivyomwandama kuwa ni pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), ikimtaka apeleke vielelezo.

Pia alisema aliitwa na maofisa wa Jeshi la Polisi, linaloongozwa na IGP, Said Mwema, chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani, inayoongozwa na Laurence Masha, wakimtaka apeleke vielelezo vya tuhuma zake.

“Nimeitwa na Kamati Ndogo ya Ulinzi na Usalama wa Taifa ili kuhojiwa juu ya tamko langu kuhusu ufisadi. Yote haya yamefanyika pamoja na kwamba kuna kesi mahakamani juu ya jambo hili.

“Tukumbuke kwamba Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alikwishatoa tamko bungeni kuwa wote waliotajwa, kama wanaona hawakutendewa haki, waende mahakamani. Sasa ni nani ana tamko la mwisho katika hili? Ni mawaziri, taasisi za serikali, vyombo vya dola ama Waziri Mkuu?

“Kama raia wa Tanzania, vyombo vya dola ni moja ya mategemeo yangu ya kunilinda mimi na mali zangu, kama raia wengine, lakini pamoja na kusakamwa na vyombo hivyo, nasema siogopi. Ulinzi wangu unatoka kwa Mwenyezi Mungu, pili utatoka kwa Rais Jakaya Kikwete, ambaye naamini hatakubali kuona sitendewi haki, na tatu ulinzi wangu utatoka kwa Watanzania wanaochukia ufisadi, hasa masikini na wanyonge.

“Hawa hawana fedha nyingi, ama madaraka, lakini wana nguvu ya sala na umoja bila kujali dini zao,” alisema Mengi na kushangiliwa na waamini wa kanisa hilo.

Alisisitiza kuwa, hatarudi nyuma katika msimamo wake wa kupiga vita ufisadi, kwani anaamini rushwa ikiachwa bila kukemewa, wananchi watagawanyika katika makundi mawili; la watu wenye kipato na madaraka na la watu masikini.

“Watanzania wenzangu wanaochukia umaskini, wanaochukia ufisadi, ndugu zangu waumini, nawaomba mniombee na tuimbe wimbo namba 59 katika kitabu cha ‘Mwimbieni Bwana’, usemao ‘Kazi ni yako Bwana’,” alisema.

Hatua ya Mengi kutoboa siri ya kusakamwa kwake mara baada ya kutaja majina ya aliowaita mafisadi papa, ilitokana na mahubiri ya Mhashamu Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Dayosisi ya Kaskazini, Dk. Martin Shayo, aliyeunga mkono harakati zake katika vita dhidi ya ufisadi.

Askofu huyo alimtaka Mengi asikatishwe tamaa na wajanja wachache, ambao wamekusudia kurejesha nyuma juhudi za kujiletea maendeleo.

“Taifa letu limegubikwa na mafisadi wachache, wapo Watanzania wenzetu kama Mengi, wamekuwa mstari wa mbele kupinga vitendo vya kifisadi, lakini wanakwamishwa na baadhi ya viongozi walioko madarakani, tukemee kwa pamoja.

“Mwaka huu na mwaka ujao, ni vipindi vya uchaguzi mbalimbali, kuna watu wamejaa choyo, wivu, chuki na ubinafsi miongoni mwetu, hakika watu hao ni wabaya kwa maendeleo ya taifa, msiwachague,” alisema.

Alisema, Mengi hataki urais wala hana nia ya kuwania kiti hicho, wala uongozi wa aina yoyote, lakini amejitoa kusaidia wanyonge, na rafiki zake ni masikini, walemavu, wajane, wanaoishi na virusi vya VVU pamoja na wenye matatizo mengine ya kijamii.


 
haya mambo ya simu za mkononi na TZ daima yana utata
kwa nini serikali isi issue statement kupitia daily news na tbc
huwezi ukaaita hii oficial statement ya ikulu, ingekuwa official ingeambatana na maandishi na wangetumia media zao hao TZdaima ni wapika majungu....
mbona mengi amesema wazi na kila mtu amemsikia
kwa nini huyo msemaji wa ikulu asiseme wazi na badala ya kujidai na simu ya mkononi
 

- Behind hii ishu kuna la mgambo linakuja, ninaamini soon tutaliona wanalolipika, lakini kuna something hapa.

FMEs!
 
Kazi kweli kweli mwaka huu!
 
Jk hana meno hiyo inajulikana nchi haina mwenyewe...jamani eehhh tumechoka sasa
 
Kamati Kuu leo vipi jamani? CCM watawahi dedline ya uteuzi Biharamulo au kwa kuwa wao ndio wenye dola? Chadema fuatilieni wasije peleka fomu baada ya kesho kwa njia za panya. Hakikisheni munaziona fomu kesho.
 
- Kamati kuu imemaliza kikao jana usiku sana, the dataz ni baada ya malumbano ya siku nzima, kimempitisha Bwana Mukasa, kuwa mgombea wake rasmi wa jimbo la Biharamulo.

- Inasemekana kwamba kulikuwa na malumbano mazito sana kuhusiana na suala la kupitisha nani awe mgombea wa jimbo hilo, kutokana na hoja nyingi kali na nyeti za wajumbe, ambazo kwa sasa bado wakati sio muafaka kuziweka hapa.

Otherwise, bado tunafuatilia zaidi kujua yaliyojiri humo ndani, tukizipata kama kawa ingawa hoja iliyochambuliwa ilikuwa ni moja tu yaani mgombea awe nani, na sasa Mkuchika anaondoka kuelekea huko tayari na mapambano.

Respect.

FMEs!
 


FMES;

Oscar Mukasa ni Kijana mwenzetu na yuko makini sana. Kitaaluma yeye ni mtu wa ICT na anafanya kazi Ifakara Health Research And Development Centre (IHRDC) ofisi yao iko maeneo ya Mikocheni. Toka harakati hizi zianze alikuwa na matumaini sana. Hata hivyo kwa mujibu wake mwenyewe si mzoefu sana wa mambo ya siasa.

Ila kama Wapinzani wataunganisha nguvu, then atakuwa na Changamoto kubwa sana ya kushinda.
 

Acha mambo yako wewe humjui kabisa huyo jamaa...nani kakwambia yuko makini? hajui kabisa siasa ...usimuharibie wengine twamjua inside out... kwa hili nakukatalia

Mas
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…