- I can live with this bila tatizo, tena unakaribishwa anytime ukimaliza na kunihusisha na ufisadi ingawa mimi sujakuita fisadi kwa sababu ya connection ya familia yako na BOT, the oficial shule ya ufisadi Tanzania then tunaweza kurudi tena kwenye real ishus za masilahi ya wananchi wa Tanzania,
- Now let me get this straight mkuu, kama wapiganaji 11 ni mafisadi, na mimi ni fisadi tena kwa 100%, na anytime ukiwagusa wapiganaji on the ishus za upiganaji bila dataz wala facts, it is my duty kujibu na nitawatetea with every ounce of my blood bila kuogopa wala kutishika kama nilivyofanya kwenye hii thread, and in the process you can call me anything you want, lakini siwezi kuwaangusha wapiganaji, they deserve respect tena big time kutoka kwetu wananchi wa Tanzania.
- Mifano ya kisiasa iliyokwisha tokea tayari iko wazi kwamba hatuwezi kuviamini vyama vya siasa nchini kutuokoa, sasa hatuna choice ila kuendelea kuwaamini some individuals member of our society kama kina Mengi, na baadhi ya viongozi wetu kama hawa wapiganaji, maana kama sio hawa tungekua na hali mbaya zaidi kitaifa na ufisadi, Lowassa angekua bado Waziri Mkuu, Msabaha angekua bado waziri, Karamagi angekua bado waziri, Mramba angekua bado waziri, Chenge angekuwa bado waziri, Meghji angekua bado waziri, Mgonja angekua bado katibu mkuu wa wizara, taifa tungekua bado tunalipia Richimonduli.
- Wapiganaji wenye majina ya bandia kwa sababu ya uoga, hatuwezi kuwatukana wapiganaji wanao-deal na mafisadi one on one kila siku ya Mungu in the real life bila ya uoga, it is just not fair na wala sio ustaarabu ni simply kuwa na secret agenda yenye lengo la kuwahadaa wananchi ili kujipatia madaraka, lakini sio kuwajali wananchi na masilahi ya taifa.
Mungu awajalie wapiganaji, na pia Aibariki Tanzania na hasa JF.
Respect.
Field Marshall Es
FMES,
Jadili hoja na don't try to get personal.
Wewe umedai na kunituhumu mimi CHADEMA, nimekuuliza ni lini nimesema kuwa mimi ni CHADEMA? Ndio maana nikakupa mfano wa kusema wewe kujua Mafisadi (na ni mafisadi kweli na si hao Wapiganaji) tuanze kukuita Fisadi.
Mfano, kuoana kwa mawazo yangu na Sera za CHADEMA, CUF au hata CCM hakunifanyi mimi niwe mwanachama wa chama hicho.
Urafiki wako na Masha, haukufanyi wewe kuwa sawa na Masha ambaye leo hii anayuhumiwa kutumia madaraka yake vibaya na tena sera na itikadi zake haziendani na za "Wapiganaji".
Je Wapiganaji wakijua kuwa una Uswahiba na Masha, na wao na Masha ni vitu viwili tofauti, itakuwa sahihi ya wao kukuita Msaliti? Je sisi hapa JF ambao tumekusikia ukimtetea Masha na urafiki wenu tukisikia leo unaandamana na "Wapiganaji" unataka tuanze kukuhoji mahusiano yako?
So please do not try to get personal here. Yes my father worked at BOT and retired in 1994 and he is a peasant right now enjoying his Tshs 25000.00, pension a month, so I am not sure what were you trying to imply here.
I have never called on your parents or relatives in relationship of anything that goes in Tanzania or even insinuating anything about them here ta JF or anywhere! So keep of my family and personal life out of this, lets focus on issues.
Tukirudi kwenye issues, ni wapi nimesema kuwa Wapiganaji ni mafisadi? Hivi kuhoji nguvu zao na dhamira ya vita hii ni kuwaita Mafisadi?
Hivi nilipouliza kwa nini Spika wa Bunge na Mwakyembe wanahalalisha Rushwa kwa kuwaambia wananchi wakihongwa wachukue hizo fedha kwa kuwa ni "haki yao" badala ya kuripoti Polisi kuwa wamepewa hongo nilikosea?
Previously, umedai kuwa "Wpiganaji" wameanza kazi miaka 4 iliyopita, je miaka kabla ya hapo walikuwa wapi? Hauoni coincidence ya vita vyao na matokeo ya Ugombea uongozi ndani ya CCM 2005 na matokeo yake?
Mbona hawajamwenda Rais na kumuomba ripoti ya Warioba au ripoti ya Chifupa? Sijasikia kwenye mkutano wa Bunge kuwa wamewasilisha hoja binafsi kuomba ripoti hizo ziwekwe hadharani.
Mbona hawakupinga uteuzi wa Mawaziri ambao tangu awali walijulikana kuwa wana chembe chembe za Ufisadi? watu kama Mramba, Karamagi na Chenge?
Unatutukana Wapiganaji wa humu kwa kudai kuwa tunawahada Wananchi. Je unajua ni wangapi humu ambao maisha yetu yameshakuwa hatarini na familia zetu kutokana na kuwa "wasema hovyo"? Je unajua ni sheria ngapi na miongozo mingapi imetunga ili kukabiliana na sisi Wapiganaji tusio na sura?
Je wewe si unafahamu kuwa kuna wengine wetu humu ndani tunawindwa na Mafisadi kwa kutumia dola na vyombo vya usalama kwa kuwa tumewaudhi wakubwa kwa kujua mambo mengi na kufuna siri nyingi? Je huoni kuwa hilo pia ni hatari kwa maisha yetu?
Ikiwa leo dola iliyotawaliwa na Mafisadi kutokana na mfumo mbovu wa kiutawala, inatuma makachero pande zote za dunia kujua nani ni Mwanakjiji, anafananaje, nani Mchungaji alisoma wapi, nani Fundi Mchundo, nani kampa hii habari na wengine wengi, huoni kuwa nasi tunafanya kazi kama hao "Wapiganaji" walioko mstari wa mbele?
So do not ever question my patriotism!