CCM: Kamati Kuu Kulikoni Tena?

CCM: Kamati Kuu Kulikoni Tena?

Mkuu FMES,Saluti Mkuu! Hapo juu nakunukuu ukisema "tatizo kuu ni ufisadi na likitatuliwa matatizo mengine ya taifa letu yatajiondoa yenyewe", ndivyo ilivyo Mkuu? Sio kwamba ufisadi (malfeseance) ni matokeo ya matatizo makuu ya Taifa letu tokea na kabla ya Uhuru? Sio kwamba kwa namna moja au nyingine ufisadi umetokana na mfumo wa uchumi aliotuachia mkoloni ukichanganya na mfumo aliojaribu kuujenga Mwalimu?

- Eti ufisadi ni tatizo la system yetu ya uchumi tuliloachiwa na wakoloni? Can you define this mkuu kwanza kabla sijakujibu post yako nzima? Unasema wakoloni ndio waaliotuachia tabia za kuogopana kwenye uongozi wa juu wa taifa letu ambacho ndio hasa chanzo cha ufisadi?

- Unasema wakoloni ndio waliotufundisha kutoheshimu sheria zetu wenyewe, au the respect kwa rule of our laws? Unasema wakoloni ndio walio-create system ya vigogo kina Kahama, Rupia na Bomani ndani ya political system yetu ambao sasa na wao wamekuja kurithiwa na kina Rostam, Karamagi, na Lowassa, unasema this is wakoloni fault?

- Are you serious mkuu or you are just kidding! Mkuu ukinijbu hili basi nitaichambua post yako nzima, ila kwanza niwekee muongozo hapa!

Respect.

Field Marshall Es!
 
Wakuu kama tukiendelea kudanganyana kuwa matatizo yetu ya sasa yanatokana na mkoloni tutakuwa waongo. Watu walioishi na kufanya kazi na mkoloni wanasema wazi kabisa kuwa walikuwa ni watu wenye discpline, waliheshimu institutions, rules na laws. Pamoja na kwamba laws zao zilikuwa na lengo la kuendeleza wizi wa raslimali zetu lakini waliziheshimu sana, hata wale waliowato magaerezani walikuja kutawala makoloni wakiwa na discipline kubwa sana na kuheshimu taratibu walizojiweka.
Lakini hatukurithi hicho kutoka kwa wakoloni, tumeinnovate tabia mpya ya wizi, ukiukaji wa sheria na kuwalinda wezi na kuwapeleka wasiowezi mahakamani.
 
FMES,

Mimi si CHADEMA, hivyo unanizushia uongo. Ni sawa kama ningesema wewe ni Fisadi kisa unafahamiana na Mafisadi!
 
Rev.Kishoka,

..Samuel Sitta na madudu yake aliyofanya CDA na kwingineko leo ni kamanda na mpiganaji dhidi ya ufisadi.

..binafsi sitashangaa 10 or 15 years from now, Rostam Azizi naye amegeuka kuwa kamanda na mpiganaji.

..hawa wapiganaji "wanam-bip" Kikwete awakumbuke kwa chochote.

..halafu usidanganyike na dhana kwamba kwasababu baadhi yao wana biashara then they have nothing to loose. kumbuka kwamba they have a lot to gain kwa kuwepo in Kikwete's inner circle.

..hujiulizi kama watu hawa wana biashara na shughuli zao kwanini waingie kwenye siasa na ubunge?
 
FMES,

Mimi si CHADEMA, hivyo unanizushia uongo. Ni sawa kama ningesema wewe ni Fisadi kisa unafahamiana na Mafisadi!
Haa Hahaaaa!!! Kwi kwi!!!!! ndio maana naipenda JF. Mkuu Kishoka hapo umekata mzizi wa fitina! Ila tu heri umesema wewe kiazi, ningesema mimi mhogo ningeambiwa nina mzizi.
 
FMES,

Mimi si CHADEMA, hivyo unanizushia uongo. Ni sawa kama ningesema wewe ni Fisadi kisa unafahamiana na Mafisadi!

- I can live with this bila tatizo, tena unakaribishwa anytime ukimaliza na kunihusisha na ufisadi ingawa mimi sujakuita fisadi kwa sababu ya connection ya familia yako na BOT, the oficial shule ya ufisadi Tanzania then tunaweza kurudi tena kwenye real ishus za masilahi ya wananchi wa Tanzania,

- Now let me get this straight mkuu, kama wapiganaji 11 ni mafisadi, na mimi ni fisadi tena kwa 100%, na anytime ukiwagusa wapiganaji on the ishus za upiganaji bila dataz wala facts, it is my duty kujibu na nitawatetea with every ounce of my blood bila kuogopa wala kutishika kama nilivyofanya kwenye hii thread, and in the process you can call me anything you want, lakini siwezi kuwaangusha wapiganaji, they deserve respect tena big time kutoka kwetu wananchi wa Tanzania.

- Mifano ya kisiasa iliyokwisha tokea tayari iko wazi kwamba hatuwezi kuviamini vyama vya siasa nchini kutuokoa, sasa hatuna choice ila kuendelea kuwaamini some individuals member of our society kama kina Mengi, na baadhi ya viongozi wetu kama hawa wapiganaji, maana kama sio hawa tungekua na hali mbaya zaidi kitaifa na ufisadi, Lowassa angekua bado Waziri Mkuu, Msabaha angekua bado waziri, Karamagi angekua bado waziri, Mramba angekua bado waziri, Chenge angekuwa bado waziri, Meghji angekua bado waziri, Mgonja angekua bado katibu mkuu wa wizara, taifa tungekua bado tunalipia Richimonduli.

- Wapiganaji wenye majina ya bandia kwa sababu ya uoga, hatuwezi kuwatukana wapiganaji wanao-deal na mafisadi one on one kila siku ya Mungu in the real life bila ya uoga, it is just not fair na wala sio ustaarabu ni simply kuwa na secret agenda yenye lengo la kuwahadaa wananchi ili kujipatia madaraka, lakini sio kuwajali wananchi na masilahi ya taifa.

Mungu awajalie wapiganaji, na pia Aibariki Tanzania na hasa JF.

Respect.

Field Marshall Es
 
Naona nyasi hizi ni kavu kabisa dawa ni kumwaga petrol tu hapa halafu tutatumia DNA baadae kujua nani ni fisadi na nani ni mpinga ufisadi
 
Hivi kwanini Fisadi akiitwa Fisadi huwa anaona kama katukanwa?

Proverbs 22:16 He who oppresses the poor to increase his wealth
and he who gives gifts to the rich-both come to poverty.
 
- I can live with this bila tatizo, tena unakaribishwa anytime ukimaliza na kunihusisha na ufisadi ingawa mimi sujakuita fisadi kwa sababu ya connection ya familia yako na BOT, the oficial shule ya ufisadi Tanzania then tunaweza kurudi tena kwenye real ishus za masilahi ya wananchi wa Tanzania,

- Now let me get this straight mkuu, kama wapiganaji 11 ni mafisadi, na mimi ni fisadi tena kwa 100%, na anytime ukiwagusa wapiganaji on the ishus za upiganaji bila dataz wala facts, it is my duty kujibu na nitawatetea with every ounce of my blood bila kuogopa wala kutishika kama nilivyofanya kwenye hii thread, and in the process you can call me anything you want, lakini siwezi kuwaangusha wapiganaji, they deserve respect tena big time kutoka kwetu wananchi wa Tanzania.

- Mifano ya kisiasa iliyokwisha tokea tayari iko wazi kwamba hatuwezi kuviamini vyama vya siasa nchini kutuokoa, sasa hatuna choice ila kuendelea kuwaamini some individuals member of our society kama kina Mengi, na baadhi ya viongozi wetu kama hawa wapiganaji, maana kama sio hawa tungekua na hali mbaya zaidi kitaifa na ufisadi, Lowassa angekua bado Waziri Mkuu, Msabaha angekua bado waziri, Karamagi angekua bado waziri, Mramba angekua bado waziri, Chenge angekuwa bado waziri, Meghji angekua bado waziri, Mgonja angekua bado katibu mkuu wa wizara, taifa tungekua bado tunalipia Richimonduli.

- Wapiganaji wenye majina ya bandia kwa sababu ya uoga, hatuwezi kuwatukana wapiganaji wanao-deal na mafisadi one on one kila siku ya Mungu in the real life bila ya uoga, it is just not fair na wala sio ustaarabu ni simply kuwa na secret agenda yenye lengo la kuwahadaa wananchi ili kujipatia madaraka, lakini sio kuwajali wananchi na masilahi ya taifa.

Mungu awajalie wapiganaji, na pia Aibariki Tanzania na hasa JF.

Respect.

Field Marshall Es

FMES,

Jadili hoja na don't try to get personal.

Wewe umedai na kunituhumu mimi CHADEMA, nimekuuliza ni lini nimesema kuwa mimi ni CHADEMA? Ndio maana nikakupa mfano wa kusema wewe kujua Mafisadi (na ni mafisadi kweli na si hao Wapiganaji) tuanze kukuita Fisadi.

Mfano, kuoana kwa mawazo yangu na Sera za CHADEMA, CUF au hata CCM hakunifanyi mimi niwe mwanachama wa chama hicho.

Urafiki wako na Masha, haukufanyi wewe kuwa sawa na Masha ambaye leo hii anayuhumiwa kutumia madaraka yake vibaya na tena sera na itikadi zake haziendani na za "Wapiganaji".

Je Wapiganaji wakijua kuwa una Uswahiba na Masha, na wao na Masha ni vitu viwili tofauti, itakuwa sahihi ya wao kukuita Msaliti? Je sisi hapa JF ambao tumekusikia ukimtetea Masha na urafiki wenu tukisikia leo unaandamana na "Wapiganaji" unataka tuanze kukuhoji mahusiano yako?

So please do not try to get personal here. Yes my father worked at BOT and retired in 1994 and he is a peasant right now enjoying his Tshs 25000.00, pension a month, so I am not sure what were you trying to imply here.

I have never called on your parents or relatives in relationship of anything that goes in Tanzania or even insinuating anything about them here ta JF or anywhere! So keep of my family and personal life out of this, lets focus on issues.

Tukirudi kwenye issues, ni wapi nimesema kuwa Wapiganaji ni mafisadi? Hivi kuhoji nguvu zao na dhamira ya vita hii ni kuwaita Mafisadi?

Hivi nilipouliza kwa nini Spika wa Bunge na Mwakyembe wanahalalisha Rushwa kwa kuwaambia wananchi wakihongwa wachukue hizo fedha kwa kuwa ni "haki yao" badala ya kuripoti Polisi kuwa wamepewa hongo nilikosea?

Previously, umedai kuwa "Wpiganaji" wameanza kazi miaka 4 iliyopita, je miaka kabla ya hapo walikuwa wapi? Hauoni coincidence ya vita vyao na matokeo ya Ugombea uongozi ndani ya CCM 2005 na matokeo yake?

Mbona hawajamwenda Rais na kumuomba ripoti ya Warioba au ripoti ya Chifupa? Sijasikia kwenye mkutano wa Bunge kuwa wamewasilisha hoja binafsi kuomba ripoti hizo ziwekwe hadharani.

Mbona hawakupinga uteuzi wa Mawaziri ambao tangu awali walijulikana kuwa wana chembe chembe za Ufisadi? watu kama Mramba, Karamagi na Chenge?

Unatutukana Wapiganaji wa humu kwa kudai kuwa tunawahada Wananchi. Je unajua ni wangapi humu ambao maisha yetu yameshakuwa hatarini na familia zetu kutokana na kuwa "wasema hovyo"? Je unajua ni sheria ngapi na miongozo mingapi imetunga ili kukabiliana na sisi Wapiganaji tusio na sura?

Je wewe si unafahamu kuwa kuna wengine wetu humu ndani tunawindwa na Mafisadi kwa kutumia dola na vyombo vya usalama kwa kuwa tumewaudhi wakubwa kwa kujua mambo mengi na kufuna siri nyingi? Je huoni kuwa hilo pia ni hatari kwa maisha yetu?

Ikiwa leo dola iliyotawaliwa na Mafisadi kutokana na mfumo mbovu wa kiutawala, inatuma makachero pande zote za dunia kujua nani ni Mwanakjiji, anafananaje, nani Mchungaji alisoma wapi, nani Fundi Mchundo, nani kampa hii habari na wengine wengi, huoni kuwa nasi tunafanya kazi kama hao "Wapiganaji" walioko mstari wa mbele?

So do not ever question my patriotism!
 
Huu ndiyo ukigeugeu niliousema huko nyuma kwamba kauli za Kikwete na wasemaji wake wa CCM zinabadilika kila dakika, kwa hiyo siyo watu kuamini. Chiligati baada ya kikao cha NEC aliwashambulia First 11 akisema wamegeuza Bunge limekuwa Ze Comedy (hili ni kosa na anastahili kuchukuliwa hatua na Bunge kwa kulidhalilisha). Leo hii anakuja na kauli nyingine kwamba anawaunga mkono hao First 11.

CCM sasa wasema waunga mkono vita dhidi ya mafisadi

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa CCM, John Chiligati amesema chama hicho hakina ugomvi wala uadui na wabunge wake wanaoongoza vita dhidi ya mafisadi nchini.

Kauli hiyo imetolewa siku chache baada ya mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kuondoa utata uliotokana na maazimio ya Halmashauri Kuu ya chama hicho ukionyesha kuwa wabunge wanaopiga kelele za ufisadi, wanakichafua chama na serikali yake.

Chiligati ndiye aliyetoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari ambayo ilisisitiza kuwa vita hiyo si ya kikundi cha watu wachache bali ya CCM.

Jana, Chiligati alikuwa ni mtu mwenye kuunga mkono kikundi hicho wakati Mwananchi ilipotaka maoni yake kuhusu wabunge hao ambao wanaonekana kukaidi maazimio ya Nec, huku wakitamba kuwa hakuna anayeweza kuwafunga mdomo.

“CCM haina ugomvi na wabunge wake wala mtu yeyote anayejitoa mhanga kupinga ama kupambana na mafisadi,” alisema Chiligati ambaye pia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

“Msimamo wa chama chetu ni kwamba rushwa ni adui wa haki, usichukue, kuomba wala kutoa rushwa, huo ndio wimbo wa kila mwana-CCM.

“Hatuna ugomvi wala uadui na mtu yeyote anayepambana na rushwa, ufisadi, uporaji, wizi na ujambazi. Huo ndio msimamo wa CCM.”

Baada ya kikao cha Nec kilichofanyika Dodoma mwezi uliopita, Chiligati alisema CCM imeunda kamati ya watu watatu, inayoongozwa na rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi kuwachunguza wabunge wenye tabia ya kuishambulia serikali nje ya vikao vya chama.

Habari za ndani ya kikao hicho ambazo baadaye zilivuja kwa vyombo vya habari, zilieleza kuwa Nec ilimweka kitimoto Spika Samuel Sitta kwa madai kuwa anaruhusu mijadala inayokichafua chama na serikali, huku baadhi ya wajumbe wakishinikiza anyang'anywe kadi ya CCM kwa kile kilichoelezwa kuwa anawapa uhuru bungeni watu wanaoishambulia serikali kwa ufisadi.

Kauli hiyo mpya ya Chiligati, inaweza kuwa imetokana na msimamo wa Rais Kikwete ambaye alisema CCM haiwezi kuwafunga midomo wabunge wake.

Katika mazungumzo yake na wananchi aliyoyafanya kwa njia ya televisheni na redio katikati ya wiki iliyopita, Rais Kikwete alisema kuikosoa serikali ni kuifanya ijiangalie na kujirekebisha na hivyo haiwezi kuwazuia wabunge kuikosoa.

Kauli ya Kikwete ilifuatiwa na ya waziri mkuu wa zamani, John Malecela ambaye alimsifu mwenyekiti wake kwa kuruhusu mijadala hiyo na kuongeza kuwa vita dhidi ya mafisadi ni takatifu kwa kuwa ilikuwapo tangu enzi za TANU.

Tangu kumalizika kwa Nec, wabunge ambao wamekuwa wakijinadi kuwa ni makamanda wa vita dhidi ya ufisadi wamekuwa wakikaririwa na vyombo vya habari wakisema kuwa hakuna mtu anayeweza kuwafunga midomo.

Wabunge hao pia walifanya mikutano ya hadhara kwenye majimbo ya baadhi yao na kusisitiza msimamo wao kuwa wataendelea na vita hiyo kwa kuwa ilani ya CCM inawaruhusu.

Maswali yangu yanabaki pale pale, kwanini wakijifungia kwenye vikao vya siri wanaonekana kuunga mkono ufisadi, na wakija kwenye public wanajifanya wanapiga vita ufisadi. Sasa hapa ni nani msanii wa Comedy? Anayetamka Bungeni mbele ya watu ama anayebadilika kama kinyonga kila wakati kwa kuangalia mazingira yakoje?

Hii vita ya ufisadi ni ngumu sana na kupiganiwa na watu 11 au hata 20 tu ndani ya mfumo wa CCM ni kazi ngumu sana. Ushindi hauwezi kupatikana na hasa kama vikao vya maamuzi ya juu viko-dominated na mafisadi, kuanzia Kamati ya Maadili, CC na NEC.

Hawa makamanda wa vita ya ufisadi watabebwa na Kikwete kwa kuwa anawahitaji kama mfano wa kutolea itakapofika wakati wa kuomba kura 2010 kwa wananchi. Atasema wabunge wa CCM ni machachari sana wanaisakama sana serikali yao wenyewe na hivyo wanapigania maslahi ya wananchi.

Tusubiri mwezi Novemba maana si mbali sana, swala la Richmond litarudi tena Bungeni na hapo ndipo nitakapoona kama vita hii takatifu inapiganwa kweli ama wabunge wanaisafisha CCM iliyochafuka mbele ya macho ya wananchi.

Kosa la hawa First 11 ni kuamini kauli za JK na hivyo kumuweka kwenye kundi lao kwamba yuko upande wao, lakini akiwa kwenye Kamati ya Maadili na CC, hasemi yuko upande gani. Kwa kuwa JK ni kipenzi cha First 11, kama serikali haiko tayari kutekeleza yale maazimio ya Bunge, basi JK atawaita na kuwaweka sawa na mwisho wa siku ngoma itapita kiulaini.

Richomond ndiyo chanzo cha mvurugano kwenye kikao cha NEC ya majuzi na kwa bahati mbaya the same Richmond ni bomu linalomgusa JK mwenyewe na ndiyo maana analibeba kwa umakini mkubwa sana ili lisije likamlipukia mikononi mwake na akaishia kupata ulemavu wa muda ama wa kudumu, kama ilivyotokea kwa EL. Kwa hiyo njia pekee ya kulibeba kwa umakini ni kuendelea kuwabeba First 11 na mafisadi kama walivyo bila kumfukuza yeyote wala kunyang'anya kadi. Akifanya kosa la kumtoa yeyote ajue kwamba ngoma itakuwa nzito sana ifikapo 2010.

Akina Mwakyembe wanatembea kifua mbele kwa kuwa wanajua wamebeba nini kwenye mikoba yao, siku JK na CCM yake wakiwageuzia kibao, mtakuja kuambiwa yale ambayo hawakuyasema kwenye report yao. Mwakyembe aliomba kwamba kama kuna mtu hakuridhika na ile report yao, wairudishe Bungeni ili wakamwage kila kitu, maana kuna vingine hawakuvisema kwa kuwa walikuwa "wanalinda heshima ya serikali" (sijui ni heshima gani hiyo ambayo itabidi iwekwe kando iwapo mafisadi wataendelea kuwaandama)!

Mwezi Novemba tutajua chuya na mchele vinafananaje. Kila la heri kwa wapiganaji katika hiyo vita takatifu.
 
Rev. Kishoka;
FMES,

Jadili hoja na don't try to get personal.

Wewe umedai na kunituhumu mimi CHADEMA, nimekuuliza ni lini nimesema kuwa mimi ni CHADEMA? Ndio maana nikakupa mfano wa kusema wewe kujua Mafisadi (na ni mafisadi kweli na si hao Wapiganaji) tuanze kukuita Fisadi. Mfano, kuoana kwa mawazo yangu na Sera za CHADEMA, CUF au hata CCM hakunifanyi mimi niwe mwanachama wa chama hicho. Urafiki wako na Masha, haukufanyi wewe kuwa sawa na Masha ambaye leo hii anayuhumiwa kutumia madaraka yake vibaya na tena sera na itikadi zake haziendani na za "Wapiganaji". Je Wapiganaji wakijua kuwa una Uswahiba na Masha, na wao na Masha ni vitu viwili tofauti, itakuwa sahihi ya wao kukuita Msaliti? Je sisi hapa JF ambao tumekusikia ukimtetea Masha na urafiki wenu tukisikia leo unaandamana na "Wapiganaji" unataka tuanze kukuhoji mahusiano yako?

- Mchungaji sina sababu ya kwenda personal na wewe ila umetukana sana matusi wapiganaji na hii thread, na ni tabia umekua nayo sana na nimejaribu tu kukuheshimu siku zote, lakini heshima ikibidi kufika mwisho sina tatizo mkuu maana wapiganaji kwangu ni personal, ndio kwanza nimerudi kumpandisha ndege mpiganaji mmoja.

- Masha nimeitetea background yake always kama nilivyomtetea Mwakalinga, wapiganaji wote wanajua fika marafiki zangu wote wa karibu sana, na wengi ni marafiki zao pia maana siasa sio vita wala ugomvi ni hoja tu, unaweza kuhoji anything you want kuhusu maisha yangu mkuu you know me weka hapa, lakini usijaribu kunitisha na anything kwa sababu sina uchafu wala ufisadi, I am clean ndio maana huwa sibabaiki na anything, Masha ni rafiki yangu wa karibu sana, so is you na wengine wengi huku JF,

- Sasa kama wewe au anybody humu ana tatizo na urafiki wangu na Masha ulipaswa kusema kabla ya hizi ishu ili nikujibu, ukiona unajaribu kumshambulia mtu kwa sababu ya urafiki na mtu mwingine, either ni wivu au ni kukosa hoja au kukosa facts za ufisadi over yule mtu, Mchungaji kama unaujua ufisadi wangu au ushiriki wangu kwenye any ufisadi basi wewe uweke hapa JF mkuu siogopi nitakubali au nitasema ukweli tu kama ninao, kwa sababu sina ufisadi never hata senti tano yangu haijawahi kutoka kwenye ufisadi, ila huwezi kuwatukana wapiganaji ukategemea a free pass kutoka kwa mtu kama mimi, nada na never!

- Again, Masha ni rafiki yangu na wewe pia, sasa na wewe ni fisadi kwa sababu mimi ni rafiki wa Masha fisadi? Bwa! ha! ha! hata wewe ukishambuliwa chochote kwa maneno ya uongo nitakutetea tu, ila kama unaujua ufisadi wangu huna sababu ya kuzunguka mbuyu weka hapa nitabeba msalaba wangu! Lakini tusitishane na maneno ya ufisadi bila facts wala dataz maaan tunapoteza muda wa wananchi bure hapa!

So please do not try to get personal here. Yes my father worked at BOT and retired in 1994 and he is a peasant right now enjoying his Tshs 25000.00, pension a month, so I am not sure what were you trying to imply here. I have never called on your parents or relatives in relationship of anything that goes in Tanzania or even insinuating anything about them here ta JF or anywhere! So keep of my family and personal life out of this, lets focus on issues.

- Unaona mlivyo wepesi kusahau, hebu nenda kwenye ishu ya kifo cha Bhoke Munanka, ulsiema nini mkuu? maaan hata muda wa kuyarudia sina, ila nilikupa break tu haya ya personal umeyaanza siku nyingi sana mkuu, mimi huwa ninauvumilivu hasa na watu ninaowajua kama wewe, lakini ya personal uliyaanza siku nyingi sana mkuu sasa next time usifanye tena mkuu tujadili hoja badala ya kujaribu kulazimishana ishus bila facts, labda mkuu ungeanza na wewe kuanza kuweka personal nje ya ishus muhimu za taifa.

Respect.

FMEs!
 
FMES,

Tukirudi kwenye issues, ni wapi nimesema kuwa Wapiganaji ni mafisadi? Hivi kuhoji nguvu zao na dhamira ya vita hii ni kuwaita Mafisadi?

Hivi nilipouliza kwa nini Spika wa Bunge na Mwakyembe wanahalalisha Rushwa kwa kuwaambia wananchi wakihongwa wachukue hizo fedha kwa kuwa ni "haki yao" badala ya kuripoti Polisi kuwa wamepewa hongo nilikosea?

Previously, umedai kuwa "Wpiganaji" wameanza kazi miaka 4 iliyopita, je miaka kabla ya hapo walikuwa wapi? Hauoni coincidence ya vita vyao na matokeo ya Ugombea uongozi ndani ya CCM 2005 na matokeo yake?

Mbona hawajamwenda Rais na kumuomba ripoti ya Warioba au ripoti ya Chifupa? Sijasikia kwenye mkutano wa Bunge kuwa wamewasilisha hoja binafsi kuomba ripoti hizo ziwekwe hadharani.

Mbona hawakupinga uteuzi wa Mawaziri ambao tangu awali walijulikana kuwa wana chembe chembe za Ufisadi? watu kama Mramba, Karamagi na Chenge?

Unatutukana Wapiganaji wa humu kwa kudai kuwa tunawahada Wananchi. Je unajua ni wangapi humu ambao maisha yetu yameshakuwa hatarini na familia zetu kutokana na kuwa "wasema hovyo"? Je unajua ni sheria ngapi na miongozo mingapi imetunga ili kukabiliana na sisi Wapiganaji tusio na sura?

Je wewe si unafahamu kuwa kuna wengine wetu humu ndani tunawindwa na Mafisadi kwa kutumia dola na vyombo vya usalama kwa kuwa tumewaudhi wakubwa kwa kujua mambo mengi na kufuna siri nyingi? Je huoni kuwa hilo pia ni hatari kwa maisha yetu?

Ikiwa leo dola iliyotawaliwa na Mafisadi kutokana na mfumo mbovu wa kiutawala, inatuma makachero pande zote za dunia kujua nani ni Mwanakjiji, anafananaje, nani Mchungaji alisoma wapi, nani Fundi Mchundo, nani kampa hii habari na wengine wengi, huoni kuwa nasi tunafanya kazi kama hao "Wapiganaji" walioko mstari wa mbele?

So do not ever question my patriotism!

- Mchungaji, wapiganaji wameanza kazi nzito in four years tu, ni kwa sababu siku zote Tanzania tumekwua na siasa za kuzibwa midomo, zilizoanza na Mwalimu na kuigwa na wote wengine waliofuata, mpaka Rais Kikwete aliposhika nchi ndiyo viongozi wameanza kuruhusiwa kusema wazi bila uoga, na ndipo wapiganaji wakaanza kazi yao ambayo tayari imeshaqleta matunda makubwa sana ingawa bado kazi mbele yao ni nzito sana, wanachohitaji ni support yetu wananchi sio unfounded attacks, kama zako kwenye hii thread.

- Kama wapiganaji hawakupinga majina ya mawaziri mafisadi, wewe kama mpiganaji ulifanya nini mkuu kuhusu hayo majina? Maana to me what counts ni kwamba hao uliowataja sio mawaziri tena, na ni kutokana na vita kubwa ya wapiganaji.

- Kwamba ninawatukana wapiganaji wa JF, ni hadithi za alfu-lela-ulela, maana kama ni matusi umeyaanza wewe dhidi ya wapiganaji wa kweli, nimekukumbusha kwamba heshimu wapiganaji wa kweli wanao-risk maisha yao mbele ya taifa na wananchi, sasa huwezi kuwashusha hadhi na eti kutaka waje kwako kuomba ushauri that is a joke mkuu!

- Ya kuwindwa na kutokuwindwa kwa members hapa JF, ninaomba kutoligusa, otherwise mkuu tuendele kukata ishus za taifa kama hutaki kuulizwa your patriotism kwa taifa lako, vipi tena wewe ku-question ya wengine bila sababu za msingi?

Respect.

FMEs!
 
CCM sasa wasema waunga mkono vita dhidi ya mafisadi

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa CCM, John Chiligati amesema chama hicho hakina ugomvi wala uadui na wabunge wake wanaoongoza vita dhidi ya mafisadi nchini.

Kauli hiyo imetolewa siku chache baada ya mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kuondoa utata uliotokana na maazimio ya Halmashauri Kuu ya chama hicho ukionyesha kuwa wabunge wanaopiga kelele za ufisadi, wanakichafua chama na serikali yake.

Chiligati ndiye aliyetoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari ambayo ilisisitiza kuwa vita hiyo si ya kikundi cha watu wachache bali ya CCM.

Jana, Chiligati alikuwa ni mtu mwenye kuunga mkono kikundi hicho wakati Mwananchi ilipotaka maoni yake kuhusu wabunge hao ambao wanaonekana kukaidi maazimio ya Nec, huku wakitamba kuwa hakuna anayeweza kuwafunga mdomo.

“CCM haina ugomvi na wabunge wake wala mtu yeyote anayejitoa mhanga kupinga ama kupambana na mafisadi,” alisema Chiligati ambaye pia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

“Msimamo wa chama chetu ni kwamba rushwa ni adui wa haki, usichukue, kuomba wala kutoa rushwa, huo ndio wimbo wa kila mwana-CCM.

“Hatuna ugomvi wala uadui na mtu yeyote anayepambana na rushwa, ufisadi, uporaji, wizi na ujambazi. Huo ndio msimamo wa CCM.”

- This is hillarious, Chiligati tena I mean Mungu Alibariki hili Taifa.

- Huyu si majuzi tu aliita wapiganaji walevi?

Respect.

FMEs!
 
- This is hillarious, Chiligati tena I mean Mungu Alibariki hili Taifa.

- Huyu si majuzi tu aliita wapiganaji walevi?

Respect.

FMEs!

Mkuu watu wanaangalia upepo. Baada ya kikao cha NEC Bob Chill alijua kwamba mafisadi wameshinda na hata wewe ulionyesha dalili za kukata tamaa kwa kuwa NEC iliwatikisa makamanda na walitikisika. Lakini kwenye mapambano kuna nadharia moja, mkipigwa sana mkaonekana kusambaratika na kama hawajawaua hata mmoja wenu, basi kuna opportunity ya kurudi nyuma na kujikusanya upya (retreat) na kuanza kujijenga upya tayari kwa kupanga mikakati ya mashambulizi mapya.

Walichofanya makamanda wako ni kwamba wamegoma kunyenyua mikono juu, ila wameamua kuchukua njia ya kivyao ya kujikusanya upya na kupanga mikakati ili waone move inayofuata ni ipi.

Majibu ya JK ya majuzi yamewapa matumaini na nina uhakika mafisadi bado wanatafakari kauli za JK. Lakini kauli za JK huwa sizichukulii seriously mpaka siku nitakapoona amefanya kweli. Ndiyo maana akina Bob Chill na Makamba wamebaki kuwa watu wa kusema hili leo, after few days utawasikia wakibadilisha ama wanakana kauli zao kwa kuwa Muungwana haeleweki yuko upande gani.
 
Rev. Kishoka,

Achana na huyo FMES maana atakupotezea muda tu. Umejaraibu kujenga hoja yeye anaenda kwenye mambo ya familia. Watu wengine wakienda mambo ya familia yake anakuja juu.

Hapo mamake yuko kweye hilo kundi basi atamtetea mpaka siku ya kufa. Hao hao walioitwa wahuni na Nyerere tunaambiwa ndio wanaongoza kutupigania sisi maskini, ni uwizi mtupu.

Nimepata points nyingi sana kwenye hii thread za kutumia huku vijiweni. Asante kwa somo la nguvu mkuu Kshoka.
 
Engineer, Kishoka na FMES;

Naombeni muwe na amani. Hasa nyie wawili FMES na Kishoka jamani tofauti zetu tulizizika kule BCS. Mbona mnaendeleza ugomvi utafikiri hamjuani?, YAP tunajuana kimaandishi na kimtazamo humu.

Ninasisitiza naombeni AMANI iwatawale.

Asanteni sana.
 
Acha kulia lia wewe kama kasichana ka A level...wacha wakate nondo, hapendwi mtu hapa ni hoja....na si vioroja!
 
Acha kulia lia wewe kama kasichana ka A level...wacha wakate nondo, hapendwi mtu hapa ni hoja....na si vioroja!

Some people live because it is illegal to................them.

Masa;

Toka upate internet access basi mgogoro!.

Sio lazima uandike au useme hata kama unaruhusiwa kisheria kuandika au kusema, kabla ya kuandika au kusema lazima upime unataka kuandika au kusema nini!
 
I think this applies to you as well....! Nashindwa jua IQ za wengine hapa!
 
I think this applies to you as well....! Nashindwa jua IQ za wengine hapa!

Toa hoja zako. Kwahiyo unakubaliana na hayo niliyoandika eeeh!! Safi, sasa mimi sipo kihivyo.

Anyway ngoja niachane na wewe watashindwa kutofautisha...
 
Back
Top Bottom