CCM,kampeni ya kazi gani?

CCM,kampeni ya kazi gani?

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,307
Reaction score
25,932
Katiba Inayopendekezwa ni yenu;Serikali ni yenu;Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni yenu;Wapigakura mnao kwa mamilioni;UKAWA hawatashiriki,kampeni ya kazi gani?

Au hamjiamini katika kufikia akidi? Hofu inatoka wapi hadi muendelee kutumia mabilioni kufanya kampeni luningani,magazetini,mitandaoni na mikutanoni?

Kama kweli nyinyi ni nambari wani,kampeni hazina haja. Msubiri tu Aprili 31 na mjaze kura.
 
Huo ni mradi wa kutafuna pesa hawawezi uacha hata useme nini; au hujui kofia, kanga na vitenge ni bei?
 
mimi nimeshatoka kanisani na kwa jinsi nilivyoelewa na padre wangu alipokuwa anatusomea tamko hilo hakuna wa kunishawishi kuipigia kura ya ndiyo katiba feki ya Chenge.
 
Wamchukue na Zitto awasaidie kupiga Kampeni. Maana naona wakati wa Escrow kila gamba alimkashifu Zitto kuwa ni Kibaka. Leo amefukuzwa Chadema wanamuona Malaika.
 
Mkuu hayo yalishanenwa tangu kale, Chema chajiuza kibaya chajitembeza. Wakati Rasimu ya Sitta/Chenge ikijitembeza, ile Jaji Warioba itaendelea kuuzika kwa miaka mingi ijayo; itadumu vifuani mwetu vizazi na vizazi. Itatumika kama rejea katika uga wa taaluma vizazi na vizazi kama mfano wa rasimu bora kabisa ya Katiba kuwahi kutokea nchini. Watakaokuwepo enzi hizo watatushangaa na kutudharau kama kizazi cha hovyo kabisa kuwahi kuwepo.
 
Back
Top Bottom