CCM Kilimanjaro inayumba, Viongozi hawaelewani

CCM Kilimanjaro inayumba, Viongozi hawaelewani

A

Anonymous

Guest
Kuambiwa ukweli kunauma sana, lakini ndio dawa pekee inayofaa kutatua changamoto iliyopo katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Kilimanjaro.

Nakumbuka watu walifurahi hususani Wana CCM waliposikia Katibu wa Chama wakati huo Komredi Jonathan Mabhiya akiondoka baada ya kuongoza miaka takribani mitano hivi, walipika mpaka pilau na vinywaji vya bei ghali walijipendelea siku hiyo.

Sasa hali imekuwa mbaya, dalili zinaonyesha hakuna maelewano baada ya kuletwa mwanamama Mercil Molel kuchukua nafasi hiyo, utulivu baina yake na baadhi ya Idara ikiwamo Idara ya Uenezi sio shwari.

Bi. Molel hataki kusikia lolote kutoka kwenye Idara hiyo, miezi michache iliyopita alikuja Mlezi wa CCM mkoa wa Kilimanjaro Bi. Rabia siku hiyo walipokea wanachama wapya kutoka Chadema lakini cha kustaajabisha mvutano ulijionyesha baina yake na Mkuu wa Idara ya Uenezi Bw. Ibrahim Urio.

Urio kila alipotaka kuzungumza mafanikio yanayotokana na Rais Samia Suluhu Hassan alikuwa akinyang'anywa microphone, kijana wa watu akaona isiwe tabu akajiweka pembeni lipite.

Lingine likatokea wakati wa kuapisha wanachama wapya, kiprotokali linatakiwa lifanyike na Mkuu wa Idara ya Uenezi Mkoa kwani shughuli hiyo ni ya kimkoa lakini ikafanya na mtu mmoja kutoka CCM Moshi Vijijini anayeitwa Mahayu ambaye kiitifaki haruhusiwi.

Mwenyekiti wa CCM mkoa Komredi Patrick Boisafi alikuwepo siku hiyo lakini akatumia busara ngoja liendelee tu, kwasababu hao kina Mahayu wako pamoja na Bi. Molel, hivyo wengine watataga tu.

Haikushia hapo hivi karibuni wamekuwa na semina za Makatibu wa Uenezi ngazi ya kata na vitongoji mchezo baina yake na kijana wa watu Urio ni ule ule, kumwingilia majukumu yake ya Uenezi Jambo ambalo unashindwa kuelewa Nini kitatokea huko mbeleni.

Hatukatai Kila mtu ana udhaifu wake lakini katika kukijenga Chama hii ni changamoto kubwa isitoshe kwa mkoa kama Kilimanjaro ambao Kisiasa ni mkoa wa kimkakati.

Wakati Bi. Rabia alipokuja aliweka bayana kuwa fitina za kisiasa ndani ya chama zimezidi ikiwamo Moshi kuwa kinara ambako makao makuu ya CCM mkoa yapo.

Unafikiri wakiendelea hivi hivi chama kitakuwa salama? Bi. Molel ambaye ni Katibu hivi hajui kutoshikamana na Idara nyingine ni kuwa CHADEMA watajipatia nafasi maridhawa tena kiulaini.

Halafu unashindwa kuelewa Bi. Molel ni lile kundi linalompinga SSH au la, maana matendo yake huyu Katibu wa Chama mkoa wa Kilimanjaro yanatishia Umoja na mshikamano wa Chama.

Bi. Molel akisikia yeyote yule akimtaja Mabhiya ananuna vibaya mno sasa hapo imekaaje, hii ni hatari kwa uhai wa Chama, watu wanakuja wanagawa hela anaangalia tu, hachukui hatua yoyote.

CCM Kilimanjaro inakukumbuka sana Komredi Mabhiya, kwa msimamo yako ndani ya Chama, huyu Mama Bi. Molel amekuja wakati mbaya ambao wale machawa na watoaji rushwa kuwahonga wapiga Kura wao wanafurahi kwasababu wanammudu.

Tunasubiri Makatibu wa Uenezi CCM watakapoenda Dodoma kwa ajili ya Semina, siku chache zijazo watarudi na Nini katika mikoa yao kwa ajili ya ujenzi wa chama. Idara ya Uenezi ni muhimu mno kwa wakati huu.

Naomba kuwasilisha.





ACg8ocIWDWuN2z4VT1bU66hasYAsGWSgMqjjzB-l-9vxHn0H3IbDUQc=s40-p
ReplyForward

Add reaction
 

Attachments

  • mabhiya_urio.jpg
    mabhiya_urio.jpg
    60.4 KB · Views: 3
Back
Top Bottom