CCM kufadhili kitabu cha mzee Songambele kuenzi historia ya nchi, chama na serikali

CCM kufadhili kitabu cha mzee Songambele kuenzi historia ya nchi, chama na serikali

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,773
Reaction score
1,174
CCM KUFADHILI KITABU CHA MZEE SONGAMBELE KUENZI HISTORIA YA NCHI, CHAMA NA SERIKALI

- Balozi Nchimbi atoa neno, akimwakilisha Dkt. Samia msibani

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi amesema kitabu alichoandika Alhaj Mzee Mohamed Mustafa Songambele kitakuwa mojawapo ya rejea adhimu za historia ya Tanzania.

Balozi Nchimbi amesema kuwa kitabu hicho kiitwacho “Safari ya Karne”, kina utajiri wa maelezo kuhusu mapambano ya kutafuta uhuru wa Tanganyika, kupatikana kwa nchi na taifa la Tanzania na kuundwa kwa CCM.

Dkt. Nchimbi amesema hayo alipokuwa akitoa salaam za pole na rambirambi kwenye msiba wa Hayati Alhaji Mzee Songambele, akimwakilisha Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, mjini Songea, mkoani Ruvuma, leo Jumatatu tarehe 2 Juni 2025.

“Kutokana na heshima na mchango mkubwa wa Mzee Songambele kwa nchi yetu, taifa letu na chama chetu, Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuguswa sana na msiba huu, ameniagiza rasmi kumwakilisha na ameagiza Chama na Serikali kuchukua gharama zote za msiba huu.

“Mzee Songambele amefariki akiwa amemaliza kuandika kitabu chake. Hadi mwezi Machi mwaka huu, alikuwa amekiita jina la “Swahiba wa Nyerere”, lakini miezi miwili iliyopita akabadili, nadhani aliona atatimiza miaka 100, akakiita “Safari ya Karne,” amesema Balozi Nchimbi na kuongeza;

“Kutokana na umuhimu wa kitabu hicho, ambacho aliniomba niandike dibaji na niliandika, humo ameelezea mengi kuhusu yeye na Nyerere, harakati za uhuru, utaifa wetu na CCM pia, Chama Cha Mapinduzi kitasimamia ili kitabu hicho kitoke ili Watanzania wapate kujifunza historia vizuri,” alisema Balozi Nchimbi.

Aidha, Balozi Nchimbi alisema Mzee Songambele pia alikuwa mmoja wa viongozi waliotoa mchango mkubwa kwa nchi, taifa, chama na serikali kutokea Mkoa wa Ruvuma, akisisitiza kuwa hilo ni jambo linalostahili kuenziwa na viongozi wa kizazi cha sasa kwa kuwa waadilifu, wanaowajibika, wazalendo kwa nchi na kuwatumikia watu.

Hayati Alhaji Mzee Songambele, mwanasiasa na kiongozi mkongwe nchini, ambaye alifariki usiku wa kuamkia Jumapili ya tarehe 1 Juni, mwaka huu, alizikwa Jumatatu Juni 2, 2025 katika makaburi ya familia yaliyoko Bombambili, mjini Songea.
IMG-20250602-WA0229.jpg
IMG-20250602-WA0228.jpg
IMG-20250602-WA0233.jpg
 

Attachments

  • IMG-20250602-WA0232.jpg
    IMG-20250602-WA0232.jpg
    463.7 KB · Views: 40
  • IMG-20250602-WA0231.jpg
    IMG-20250602-WA0231.jpg
    392.8 KB · Views: 36
  • IMG-20250602-WA0230.jpg
    IMG-20250602-WA0230.jpg
    596.5 KB · Views: 35
Rip jirani yangu Mwananyamala komakoma

Kijana wako Mvula alituanzishia Super Matimila band ya akina Remmy Ongala, Moses Fan Fan, Kyanga Songa, Kasaloo Kasambula nk nk
 
Pole kwa familia ya Songambele,Aza Songambele,Binti yake Mzee Songambele.
Huyo Mzee wa zamani sana. Sijui alipofariki alikuwa na umri gani.
 
Ilo songambele ni lenu ila sisi wakunyumba tunamtambua kama NGONYANI ,Hatuna izo songa uku bombambili.
Anyway upumzike Sasa Babu sisi vitukuu tutakuenzi kama alivoagiza mwanao.
 
Back
Top Bottom