Mpaka sasa mimi najua CCM inafanya Kmpeni za wazi kabisa. Kwa sababu katika mikutano ile watu walikuwa pia na Tshirt zilizoandikwa" CAHGUA CCM, CHAGUA KIKWETE" na hii ni baada ya JK kuthibitisha kuwa anagombea.
Hizo ndo kampeni ambazo hata CHADEMA watawafunga vema CCM kama watawashitaki
waondoe hofu na waguate sheria tu!
MKUU, TAYARI CCM WAMESHAPELEKA MALALAMIKO, HII NGOMA INAPENDEZA, TUTAONA NINI NEC WATASEMA LAKINI SITOSHANGAA WAKAJA NA MAAMUZI AMBAYO YATAWALIZA WATANZANIA WALIO WENGI, TUSUBIRI HUKU TUKIMUOMBA MUNGU AWAPE NEC WOGA WA KUTOA MAAMUZI YA UPENDELEO.
SOMA HII HABARI HAPA CHINI KWA MUJIBU WA GAZETI LA MWANANCHI
CCM yailalamikia rasmi Chadema
Katika hatua nyingine Sadick Mtulya anaripoti kuwa CCM jana iliwasilisha rasmi malalamiko ya maandishi kwa Tume ya Uchaguzi (Nec), ikidai kuwa Chadema imeanza kampeni kabla ya muda.
Hatua hiyo, imefikiwa baada ya timu ya wanasheria wa CCM juzi usiku, kukamilisha kuandaa malalamiko hayo.
Malalamiko hayo yaliyawasilishwa na ofisi ya katibu mkuu wa CCM, kitengo cha mwanasheria wa chama hicho.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, katika malalamiko hayo, CCM imesema Chadema imevunja maadili ya uchaguzi yaliyotolewa na Nec kwa ajili ya uchaguzi wa rais, wabunge na madiwani kwa mwaka huu, yaliyotiwa saini na vyama vyote 18 vya siasa.
CCM inadai katika malalamiko hayo kuwa Chadema imetumia mwanya wa kutafuta wadhamini nchini kote, kufanya kampeni jambo ambalo ni ukiukwaji wa maadili katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.
Pamoja na mambo mengine, malalamiko ya CCM ni kuwa Chadema imetumia mwanya wa kutafuta wadhamini nchini kote, kufanya kampeni jambo ambalo ni ukiukwaji wa maadili katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, kilisema chanzo chetu.
Kwa mujibu wa Nec, maadili ya uchaguzi yaliyotiwa saini na vyama vya siasa hivi karibuni, yataanza kutumika rasmi kuanzia siku ya kwanza ya kampeni, Agosti 20 hadi kutangazwa kwa matokeo.
Akijibu tuhuma hizo juzi jijini Dar es Salaam mara baada ya kuchukua fomu ya kuwania urais, Dk Willbrod Slaa alisema umbumbumbu wa CCM wa kuelewa mambo ndio uliowafanya watoe malalamiko hayo .
CCM tumewazoea. Hawasomi sheria. Hawasomi sera za vyama vingine, alisema Dk Slaa akifafanua kwamba ilifanya kampeni kwa mabango sehemu mbalimbali za nchi ikiwa ni pamoja na Zanzibar, lakini anashangaa wanavyozungumza juu ya madai hayo.
Hata hivyo, Dk Slaa alikiri kuwa alipokuwa mikoani kutafuta wadhamini, umati mkubwa wa watu ulimfuata na ilibidi aueleze sababu zilizomfanya aamue kuwania nafasi hiyo.
Alifafanua kwamba wao hawakuwa na mabango wala hawakuwalazimisha watu waende kuwasikiliza, ila ile hali ya wananchi kuwa na shauku ya kumsikiliza ndiyo iliyomfanya aonekane kama anafanya kampeni.
Isitoshe, CCM hawajui sheria kwa maana kwamba sisi kama vyama vya siasa tuna wajibu wa kukutana na wananchi ili kuwaeleza sera zetu, alisema Dk Slaa.
Katika hatua nyingine, CCM imesema Rais Jakaya Kikwete atarejesha fomu za kutetea kiti chake Agosti 19, siku moja kabla ya kuanza rasmi kwa kampeni, zitakazomalizika Oktoba 30.