CCM kuondoka Madarakani siku zake inahesabika

Prof Koboko

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2020
Posts
350
Reaction score
2,550
Kila nikimtazama mambo yanayoendelea kwa mfano hili la kukataa katiba mpya wazi wazi tena bila sababu za msingi, ni wazi kabisa kua chama hakiko mbali kuondoka ni suala la muda tu.

Huwezi kukana mwongozo wa kitaifa ambao unajua kabisa moyoni mwako mazingira ya sasa yanaendani na mwongozo ulipo. Kila mtu yeyote atakayefungwa au kupigwa ama kupotezwa kwa ajili ya kudai katiba mpya ni dhambi kubwa kwa viongozi wa serikali na CCM kwa ujumla. Mungu hutoa adhabu kali sana maana utawaumiza watu bure kwa kudai kitu cha haki.

Mama angeukwepa huu mtego akaacha watu wajadili katiba wawezavyo, sijaona popote CHADEMA wakipiga wala kutukana mtu au sijaona popote wakidai katiba kwa nguvu, wanadai kwa njia za kistaarabu sana kwa sababu wanatumia makongamano ya ndani na siyo mtaani. Kuwakamata na kuwatia ndani ni uonevu na ni dhambi, Mola atachukizwa na matendo haya.

Endeleeni kumshikilia Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani nchini kwa makosa ya kubambika huku dunia inaona, wananchi wanaona, tayari media zote za dunia na hapa nchini zinajua kua tuhuma ya Ugaidi ya Mbowe ni ya kubambika na sababu kuu ni kudai katiba. Nani asiyejua kua serikali na CCM hawaitaki Katiba na kwamba siyo ajenda yao?

CCM kwa sasa kinahemea nguvu ya dola, hakuna asiyekua kua wabunge wa kuchaguliwa wa CCM zaidi ya 50% walipitishwa kimabavu na wizi wa kura. Kudhibitisha haya ni kauli ya DC wa Wilaya ya Ikungi ndugu Jerry Muro kwamba hua wanafunga ofisi na akishinda mtu hatangazwi. Ni dhahiri kua CCM kwa sasa haiwezi kusimama chenyewe, mabadiliko yeyote ya katiba kuhusu tume huru ya uchaguzi na utawala wa nchi kwa ujumla ni kiama kwa CCM.

Kama hutaki kuamini hili tuendelee kuamini kua CCM ni chama imara. Kama kutakuwa na miaka 10 mbele basi mtakumbuka haya maneno.
 
Siku za CCM MAKINI kuwapa kijiti upinzani Ni nyingi zaidi ya vinyweleo mwilini
Nyie vimada wa lumumba tutawatoa madarakani sisi wananchi wenyewe, wala sio vyama vya upinzani au kwa sanduku la kura. Hamtakuja kuamini kabisa. Kila chenye mwanzo hakikosi kuwa na mwisho.

Endeleeni kuishi kwa kukariri maisha kwamba watanzania ni waoga, maboya, hatupendi fujo, mnatuburuza mnavyotaka na tunapiga kelele tu mitandaoni. Kama mna akili mnapaswa kutambua kwa sasa uoga na ubinaadamu katika mioyo yetu ushatoweka.

Na ukitaka kuthibitisha hilo kwamba watanzania roho zimesha badilika, mwambie Waziri Mwigulu Nchemba aende kufanya ziara hata pale Kariakoo tu ya nusu saa. Kama sio wananchi kumtoa meno ya sebuleni au kumkimbiza na mawe, basi watamchomea gari hata moto mchana kweupe.

Its just a matter of time and a right booster to trigger the revolution.
 
Nyie vimada wa lumumba tutawatoa madarakani sisi wananchi wenyewe, wala sio vyama vya upinzani au kwa sanduku la kura. Hamtakuja kuamini kabisa. Kila chenye mwanzo hakikosi kuwa na mwisho.

Endeleeni kuishi kwa kukariri maisha kwamba watanzania ni waoga, maboya, hatupendi fujo na tunapiga kelele tu mitandaoni. Kama mna akili mnapaswa kutambua kwa sasa uoga na ubinaadamu katika mioyo yetu ushatoweka.

Its just a matter of time and a right booster to trigger the revolution.
Labda madaraka ya mitandaoni
 
Watanzania tuna damu baridi na tumelala sana.

Itachukua miaka mingi kuiondosha CCM madarakani.

Huo ni ukweli mchungu japo unauma.
 
CCM kuondoka ni mpk tuchapane na damu imwagike.

Bila hivyo, wataendelea kuwepo lkn wataua watu wengi sana
 
Kwa katiba hii na tume ya uchaguzi jinsi inavyojiendasha tutasubiri sana,labda wenyewe waamue kuachia vyama vingine.
 
Kila nikimtazama mambo yanayoendelea kwa mfano hili la kukataa katiba mpya wazi wazi tena bila sababu za msingi, ni wazi kabisa kua chama hakiko mbali kuondoka ni suala la muda tu.

Huwezi kukana mwongozo wa kitaifa ambao unajua kabisa moyoni mwako mazingira ya sasa yanaendani na mwongozo ulipo. Kila mtu yeyote atakayefungwa au kupigwa ama kupotezwa kwa ajili ya kudai katiba mpya ni dhambi kubwa kwa viongozi wa serikali na CCM kwa ujumla. Mungu hutoa adhabu kali sana maana utawaumiza watu bure kwa kudai kitu cha haki.

Mama angeukwepa huu mtego akaacha watu wajadili katiba wawezavyo, sijaona popote CHADEMA wakipiga wala kutukana mtu au sijaona popote wakidai katiba kwa nguvu, wanadai kwa njia za kistaarabu sana kwa sababu wanatumia makongamano ya ndani na siyo mtaani. Kuwakamata na kuwatia ndani ni uonevu na ni dhambi, Mola atachukizwa na matendo haya.

Endeleeni kumshikilia Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani nchini kwa makosa ya kubambika huku dunia inaona, wananchi wanaona, tayari media zote za dunia na hapa nchini zinajua kua tuhuma ya Ugaidi ya Mbowe ni ya kubambika na sababu kuu ni kudai katiba. Nani asiyejua kua serikali na CCM hawaitaki Katiba na kwamba siyo ajenda yao?

CCM kwa sasa kinahemea nguvu ya dola, hakuna asiyekua kua wabunge wa kuchaguliwa wa CCM zaidi ya 50% walipitishwa kimabavu na wizi wa kura. Kudhibitisha haya ni kauli ya DC wa Wilaya ya Ikungi ndugu Jerry Muro kwamba hua wanafunga ofisi na akishinda mtu hatangazwi. Ni dhahiri kua CCM kwa sasa haiwezi kusimama chenyewe, mabadiliko yeyote ya katiba kuhusu tume huru ya uchaguzi na utawala wa nchi kwa ujumla ni kiama kwa CCM.

Kama hutaki kuamini hili tuendelee kuamini kua CCM ni chama imara. Kama kutakua na miaka 10 mbele basi mtakumbuka haya maneno.

Bwana Prof Wewe Ni Prof wa Nini. So nani atakuja ongoza Tz. Hawa wasanii wa Bongo Movie. Sasa wana nguo red.
 
Back
Top Bottom