CCM kuweka mabadiliko ya Katiba kwenye ilani ya 2020-2025 wanalenga tupate Katiba ya wananchi au ya watawala?

Ililetwa mkatoroka....ikasimama mkalalama...inataka kuletwa tena mnata kukacha
 
Kuna uwezekano mkubwa wa kuondolewa ukomo wa mihula ya u-rais.
 
No Jambo jema katiba mpya ikiletwa- pia tume huru ya Uchaguzi. Wakifanya upuuzi mwingine ya Ivory Coast yatajirudia na Gabgo kuondolewa madarakani
 
Lengo kuu ni kutaka kuondoa ukomo wa mihura ya urais, Jiwe kawashika pabaya ccm hata wabunge watakaopitishwa awamu hii ni wale watakaoimba pambio la bwana asifiwe na aameeni.
 
Tuirudishe ya Warioba na Polepole. Mana haiwezekani wakazunguka nchi nzima bure kabisa. Hii katiba inafaa sana. Ila sasa Hawa wabunge wa darasa la Saba la nne na walio acha shule wasishiriki kwenye bunge la katiba. Mana hawa ndo wazee wa kugonga meza na kusema ndio kila kitu.
 
Mnajiandaa kupinga kwa vile hilo nalo linaelekea kutekelezwa?!?
Labda mabadiliko hasi na sio chanya tunayotaka wananchi wengi. Hiyo ni kutia upofu kwa wananchi wasio na uelewa wa katiba yetu.
 
Chama Cha mapinduzi kinakusudia kuja na agenda ya katiba mpya kwenye ilani,je kwa sheria iliyopitishwa juzi bungeni ya kuwawekea kinga ya kuishtakiwa viongozi wa mihimili tunategemea katiba iletwe na ccm?
Ikiwa walikataa rasimu ya mzee Warioba na haikutosha wakainajisi hata kumdhalilisha mzee yule "HAKUNA JIPYA" wala tusijidanye kupata katiba ya mwananchi chini ya ccm
 
Kuna uwezekano mkubwa wa kuondolewa ukomo wa mihula ya u-rais.
hii point niliisahau jana, nilijiuliza sana eti kwanini hakuna ukomo wa mihula ya wabunge? kuna wabunge wazee na wagonjwa hawako bungeni tangu bunge linaanza hadi linafungwa kwa five years ila pesa yao inaingia tu kina Nimrod Mkono na wengine kina Lissu, Nassaruu nk, Dr Bashiru umeonekana uko vizuri kwenye kusimamia haki hili mbona hulisemei wabunge wazee wanaliibia taifa wanalala tu bungeni sababu wameshachoka wanapaswa kukaa home! wabunge wengine wamelazwa mahospitali wengine wako home tu hawaendi bungeni ila kodi za wanyonge wanalipwa mishahara??

, nchi yetu ni maskini sababu imejaa viongozi wapumbavu eti wabunge wazee waliobakiza miaka michache duniani (Allahu Aalam) wakajiwekea ngao ya kutokuwa na ukomo bungeni na eti mbunge ajue kusoma na kuandika tu ili wasiguswe waibe hadi wafie bungeni hakuna mwisho!!shame on black skin idiots!!

hii agenda ya kudai ukomo wa ubunge nilitaka sana aichukue Zitto ila nayeye ni mbunge this has a conflict of interest!! wabunge hawaitaki kabisa na hawako tayari kutunga sheria ya kuondoa ukomo, kwanza hawataki hata kusikia kuna mtu anajua hilo ila jana kwenye mazungumzo ya Katibu Mkuu hii ishu ilipita kwa mbaaaaali!!
 
Chama Cha mapinduzi kinakusudia kuja na agenda ya katiba mpya kwenye ilani,je kwa sheria iliyopitishwa juzi bungeni ya kuwawekea kinga ya kuishtakiwa viongozi wa mihimili tunategemea katiba iletwe na ccm?
Mbona Ilani ya ua 2015/2020 suala la Katiba Mpya lilikuwemo katika Ilani mlishindwa nini kuitekeleza?
 
Mkuu wewe wa PHD kagombee ili uwashinde hao wa darasa la saba au wewe ni mtoa mapovu tu wa kwenye mitandao ya kijamii kama JF?
 
Polepole ana tonge mdomoni hawezi itaka katiba ile tena maana naye anaruzukiwa na "walewale..." nao si wajinga kumvuta upande wao...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…