CCM kuweni makini kwenye uteuzi, mkiharibu watia nia ni wengi watatawanyikia upinzani kutia nia

CCM kuweni makini kwenye uteuzi, mkiharibu watia nia ni wengi watatawanyikia upinzani kutia nia

Japhet Karibu

Member
Joined
Feb 27, 2020
Posts
79
Reaction score
129
Kiukweli watia nia ni wengi sana kupitia Chama cha Mapinduzi hivyo mnatakiwa kuwa makini sana kwenye kuwapitisha wagombea wenu kukiwakilisha chama, la sivyo mkichaguana kwa upendeleo na huku mkifurahia kwa watia nia walio wengi kupitia chama chenu na ni hao hao watawahama na kwenda kutia nia katika vyama vingine hivyo viongozi wakuu muwe makini katika hili lasivyo mtakwenda kutawanyika kwa kiasi kikubwa.
 
Sisiemu hawawezi kwenda upinzani, ni waoga sana kipindi hiki, wataona ni bora kubaki humo kuliko kufanya kama Membe.
 
Kinachotakiwa ccm ni mtu shujaa wa kumfunga paka kengele manake kweli wana ccm wanalilia ccm yao iliyopokwa na mwenyekiti. Lolote laweza kutokea hadi October watu wamechoka kuburutwa.
 
Katika awamu ya tano ni rais Mh. Dkt. Magufuli pekee ndiye aliyefanya kazi bora kabisa na hiyo haina ubishi. Hii inadhihirishwa na mawaziri, wabunge na watendaji wote wa serikali ya awamu hii kwa kauli zao wenyewe kwamba Mh. rais amefanya yale yote mazuri tunayoyaona na sifa ziende kwake. Watu hawajaridhishwa na utendaji wa bunge lililopita ndiyo maana wamejitokeza kwa wingi kutaka kuhakikisha kuwa wabunge wa bunge la 11 hawarudi mjengoni tena. Kutokana na hilo bila shaka na mawaziri ambao hutokana na wabunge, wale wa zamani hawatarudi tena. Kwa maana hiyo tunatarajia mamlaka za uteuzi watatuletea sura mpya ili kukidhi hamu ya wananchi iliyodhihirishwa na utitili wa watia nia kutokana na vyama vyote!!
 
Saaizi hakuna kwa kukimbilia acha wafie humohumo maana ccm ni mali ya mtu yeye ndio anaamua nani agombee wapi na nani ateuliwe wapi
 
Yaani mpaka dakika hii hujagundua kama huu ni mkakati ambao ni well designed kuonyesha kukua kwa demokrasia ndani ya chama na pili kila aliyechukua form jina lake limeandikwa kwa kalam ya dhahabu, na kuahidiwa kuwa ulaji upo tu, ngoja tuchukue dola. Watu wanaweka akiba ya baadae wala hakutakuwa na mgogoro hilo sahau
 
Yaani mpaka dakika hii hujagundua kama huu ni mkakati ambao ni well designed kuonyesha kukua kwa demokrasia ndani ya chama na pili kila aliyechukua form jina lake limeandikwa kwa kalam ya dhahabu, na kuahidiwa kuwa ulaji upo tu, ngoja tuchukue dola. Watu wanaweka akiba ya baadae wala hakutakuwa na mgogoro hilo sahau
Hii dhana yako ina ukweli nusu. Tunawajua watu wengi wasio na connection yoyote. Wengi wamejituma wenyewe wakiamini ukionekana tu hata kama hutapata basi utalamba teuzi.
 
Kwa kweli wengine li liability kwa CCM sio assets. Kwa mfano, Jimbo lina watia nia 80 hapo utamwacha nani uchukue nani? CCCM watakuja na maadili ambayo yatasawazisha kila kitu. Mfano, wale watia kupotia mitandao ya jamii, waliotoa rushwa na wakakamatwa na TAKUKURU, historia zao katika chama. Haway yanawetosha kuwachuja watia nia an kubaki na wale wasiokuwa na makandokando!
 
Back
Top Bottom