Uchaguzi 2020 CCM kwanini msiawaachie Beneficiaries watangaze mafanikio? Kwanini nguvu kubwa kuyatangaza?

Uchaguzi 2020 CCM kwanini msiawaachie Beneficiaries watangaze mafanikio? Kwanini nguvu kubwa kuyatangaza?

Utakuwa hujaona beneficiaries wanaoishi ughaibuni basi😄😄Kuna ka kipengele TBC wameweka wakati wa habari za usiku wamekaita Wabongo Ughaibuni, watu wenyewe hata kiswahili fasaha hawajui wanasifia ma interchange ya ccm.
 
Shida iko hapo, kuna watu hawajui maji safi na salama ta kunywa yakoje, ila kila siku wanatangaziwa Madaraja na Ndege
Ha ha ha wanatumia nguvu kubwa kutangaza ujenzi wa madaraja huku wanaowatangazia wakishindia mlo mmoja kwa siku.

CCM ni wachawi.
 
Mleta mada; muhimu kujua kuwa sisi ni watanzania kwanza kabla ya kuwa wanachama wa chama chochote cha siasa. Hivyo mwanaCCM anapoelezea mazuri yaliyofanyika, asibaguliwa, yeye naye ni mnufaika Kama mtanzania mwingine yeyote yule.
Tunalazimika pia kujitangaza kwani sisi Ni chama cha siasa na tuliahidi kutekeleza. Kama hiyo haitoshi, tunatangaza kwasababu kuna watu wanapotosha ukweli

Tatizo nguvu inayotumika hadi kuzuia magazeti yasiandike habari ya kukosoa hayo anayojisifia ndo tunashangaa wasikilizaji tunataka tusikia na wapinzani wake wanasemaje kuhusu hayo maendeleo makubwa anayoyasema CCM. Kwanini wanazuiwa wasisikike kuna woga kuwa wananchi watafahamu kuwa hakuna makubwa yamefanyika ni kelele ndiyo kubwa.
 
Wale ni wanafiki sasa kama kuna maendeleo si warudi Tanzania? Wanafanya nini nje kama kwa sasa Tanzania ni sawa na Denmark
Utakuwa hujaona beneficiaries wanaoishi ughaibuni basi[emoji1][emoji1]Kuna ka kipengele TBC wameweka wakati wa habari za usiku wamekaita Wabongo Ughaibuni, watu wenyewe hata kiswahili fasaha hawajui wanasifia ma interchange ya ccm.
 
Kiujumla Meko hakuna alichofanya mkuu. Hayo madaraja hayana msaada wowote kwa watanzania wanaoshindia mlo mmoja hasa watumishi wa umma.
Elewa basi, nimekuambia kama hutaki niongee na wewe acha kupotosha kuwa hakuna kilichofanyika au kukebehi. Yaani nyie muwaambie watanzania habari za uongo halafu utake tunyamaze, hiyo tumekataa mchana kweupeee
 
Kiujumla Meko hakuna alichofanya mkuu. Hayo madaraja hayana msaada wowote kwa watanzania wanaoshindia mlo mmoja hasa watumishi wa umma.
Dah kumbe watumishi wa umma wanashindia mlo mmoja, sawa nashukuru kwa taarifa
 
Elewa basi, nimekuambia kama hutaki niongee na wewe acha kupotosha kuwa hakuna kilichofanyika au kukebehi. Yaani nyie muwaambie watanzania habari za uongo halafu utake tunyamaze, hiyo tumekataa mchana kweupeee
Kwn Kuna sehemu nimeandika hakuna kilichofanyika?. Au unajistukia
 
Mleta mada; muhimu kujua kuwa sisi ni watanzania kwanza kabla ya kuwa wanachama wa chama chochote cha siasa. Hivyo mwanaCCM anapoelezea mazuri yaliyofanyika, asibaguliwa, yeye naye ni mnufaika Kama mtanzania mwingine yeyote yule.
Tunalazimika pia kujitangaza kwani sisi Ni chama cha siasa na tuliahidi kutekeleza. Kama hiyo haitoshi, tunatangaza kwasababu kuna watu wanapotosha ukweli

Wanufaika watapotosha vipi ukweli? Labda kama pana tafsiri ngeni ya neno mnufaika?

Ni wazi kuwa wanaolalamika hawakupata waliyotarajia. Walitegemea kuwa kiongozi wao mkuu angekuwa:

IMG_20200804_210728_515.jpg
IMG_20200804_210728_515.jpg

Madhara ya kukosa uongozi wenye mlengo huo umeleta maumivu unayoyaona au kuyasikia.

Mbaya zaidi ni kuwa, hata sasa hajatoa hata mwelekeo tu kuwa ana mpango wa kuwa atabadilika ili tumpe angalau nafasi nyingine.

Kipi kimepotoshwa hapo?
 
Kwahiyo hautuoni wanufaika mitaani na mitandaoni tunavyoipongeza serikali ya awamu ya tano?

Mfano jana nimemskia mwananchi wa kawaida akisema...kama ingewezekana tungemchangia Magufuli aende apumzike mahali huku sisi tukimpigia kampeni maana kwa aliyoyafanya kachoka saana.

Maneno ya Adam Mchomvu.
 
Kama kweli umetekeleza na yanaonekana kwa macho ya kawaida kwnn utumie nguvu kuyaelezea?? Acha watu baki ndo wayaelezee ww tulia
Kwani kuna sehem au sheria inawakataza kuyaelezea waliyofanya??? Mnajifanya kulilia demokrasia ila kwa upande wenu tu ikiwa kwa upande mwngne mnaanza kutoa povu
 
Nakumbuka wakati nafanya kwenye NGO moja ni International ilikuwa akija Mgeni yaani wafadhiri wa mradi tulikuwa haturuhusiwi sisi staff kuongelea tulicho kifanya bali wale wanufaika ndo pekee waliruhusiwa kueleza kama wananufaika kweli au la na some time walikuwa wanatuumbua vibaya mno.

Sasa CCM hayo maendeleo kama watu wamenufaika watayatangaza, sasa hizi nguvu zote za kuyatangaza ni ili iweje? Beneficiary wako wapi? Mbona hawatangazi?

Ngugu zinazo tumika kutangaza mafanikio zina walakini kwa sababu kama mafanikio watu wamefanikiwa automatic watatangaza.
Waswahel wanaaema CHEMA CHAJIUZA KIBAYA CHAJITANGAZA
 
Siwezi kutulia watu wakipotosha. Hakuna mtu baki, yote yanatuhusu sisi kama watanzania
Hauwezi kupotosha kitu kinachoonekana, tatizo ni pale anayetaka sifa anaamua kujazia nyama bila kuangalia umbile. Miradi yote inajengwa kwa pesa za watanzania, misaada na mikopo, wewe unatuambia imejengwa kwa pesa za Magufuli! Huo ni uporaji.
 
Kwani kuna sehem au sheria inawakataza kuyaelezea waliyofanya??? Mnajifanya kulilia demokrasia ila kwa upande wenu tu ikiwa kwa upande mwngne mnaanza kutoa povu
Usiseme waliyoyafanya wakati pesa ni za kodi zetu wote, unasema umenunua ndege wapinzani nao watapanda! Mbona kodi zao unazichukua! Ukichukua lazima ulete mrejesho, si hiari.
 
Wanazania Jiwe katoa pesa mfukoni mwake
Usiseme waliyoyafanya wakati pesa ni za kodi zetu wote, unasema umenunua ndege wapinzani nao watapanda! Mbona kodi zao unazichukua! Ukichukua lazima ulete mrejesho, si hiari.
 
Usiseme waliyoyafanya wakati pesa ni za kodi zetu wote, unasema umenunua ndege wapinzani nao watapanda! Mbona kodi zao unazichukua! Ukichukua lazima ulete mrejesho, si hiari.
Aliehusika kufanya hayo yote nani?? Basi hizo hela ziwekwe kwenye kibubu halafu zifanye hayo zenyewe
 
Ujenzi wa nchi haujakamilika! Akili za watu mara nyingi hupenda kilichokamilika tu, ndiyo maana ni lazima kuwakumbusha kilichofanyika hata kama malengo hayajamilika. Kwa mfano kama watu wanataka barabara ya kutoka Dar kwenda Mbeya, lakini serikali imejenga kutoka Dar mpaka milima ya Kitonga tu, bado haijafika Mbeya, watu hawataona kuwa hayo ni mafanikio. Hivyo ni lazima kuwakumbusha kuwa bado hatujakamilisha mnalotaka lakini tumeshafikia hapa.
 
Back
Top Bottom