DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
TAARIFA KWA UMMA
Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Lindi kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za uzushi na upotoshaji mkubwa zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii zikielezea kuwa baadhi ya Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Liwale wamekamatwa na Jeshi la Polisi Tanzania na kuletwa Lindi Mjini kwa kosa la kurudisha Pikipiki na Baiskeli za CCM. Jambo hili siyo la kweli na limejaa uzushi na upotoshaji wingwi kwenye mitandao ya kijamii, hali ya kisiasa ndani ya Wilaya ya Liwale na Mkoa wa Lindi iko shwari mara baada ya kumaliza mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani, na hakujawahi kutokaea tukio lolote linalohusu Viongozi na Wanachama wa CCM kurudisha vitendea kazi vya Chama Cha Mapinduzi kwenye mamlaka husika.
Aidha Chama kinawapa pole Viongozi, Wananchama na Wananchi waliyo shtushwa na taharuki hiyo. Chama kinawaomba Viongozi, Wanachama na Wananchi waendelee kuwa watulivu sambambamba na kudumisha Amani, Umoja na Mshikamano kwa maslahi ya Taifa letu.
Pia Soma: Tetesi: - Lindi: Wananchi waliorudisha Pikipiki na baiskeli za Samia wamekamatwa na Polisi