PostGE2025 CCM Lindi wafafanua juu ya taarifa kuhusu wanachama kurudisha pikipiki na baiskeli za chama

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
TAARIFA KWA UMMA​

Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Lindi kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za uzushi na upotoshaji mkubwa zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii zikielezea kuwa baadhi ya Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Liwale wamekamatwa na Jeshi la Polisi Tanzania na kuletwa Lindi Mjini kwa kosa la kurudisha Pikipiki na Baiskeli za CCM. Jambo hili siyo la kweli na limejaa uzushi na upotoshaji wingwi kwenye mitandao ya kijamii, hali ya kisiasa ndani ya Wilaya ya Liwale na Mkoa wa Lindi iko shwari mara baada ya kumaliza mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani, na hakujawahi kutokaea tukio lolote linalohusu Viongozi na Wanachama wa CCM kurudisha vitendea kazi vya Chama Cha Mapinduzi kwenye mamlaka husika.

Aidha Chama kinawapa pole Viongozi, Wananchama na Wananchi waliyo shtushwa na taharuki hiyo. Chama kinawaomba Viongozi, Wanachama na Wananchi waendelee kuwa watulivu sambambamba na kudumisha Amani, Umoja na Mshikamano kwa maslahi ya Taifa letu.

Pia Soma: Tetesi: - Lindi: Wananchi waliorudisha Pikipiki na baiskeli za Samia wamekamatwa na Polisi
​
 
CCM tunakanusha uzushi wa nini tungekaa kimya
 
Hawaaminiki tena hawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…