kwanza,
wagombea wote wa CCM zaid ya 95% ni vijana wasomi, wahitimu wa vyuo vikuu mbalimbali ndani na nje ya nchi. kwahivyo kiwango cha kufanya mistake ni kidogo mno hususani kwenye ujazaji wa fomu, ukilinganisha na upinzani vijana ambao walisusa kujiandikisha, ikalazimu kuwasukumizia wazee wenye uoni hafifu, ambao hata kujaza fomu ilikua tabu,
fomu imefutwafutwa utadhani majibu ya kuibia kwenye mtihani dah!
Jambo la pili,
wamefanya kampeni za majukwaani na zile za nyumba kwa nyumba, kwa ustaarabu wa kiwango cha juu mno, ukilinganisha na vyama vingine.
Jambo la tatu nikimalizia,
mawakala wa wagombea makini mno wa CCM, wengi wamejitolea na ni watu ambao wamejiandikisha kupiga kura, na kwahivyo inatambulika ni wakazi wa eneo hilo,
ukilinganisha na upinzani ambao, mawakala wao wengi hawajajiandikisha na kwahivyo hawatambuliki ikiwa ni wakazi wa eneo hilo.
Hakuna muujiza kwenye mambo haya ndrugo zango. Ni kujipaga tu.
Usisahau kwenda kupiga kura gentleman 🐒