Uchaguzi 2020 CCM maji ya shingo Kyela, wapambe wa Mwakyembe waapa kuichagua CHADEMA. Mangula ashindwa kuokoa Jahazi

Uchaguzi 2020 CCM maji ya shingo Kyela, wapambe wa Mwakyembe waapa kuichagua CHADEMA. Mangula ashindwa kuokoa Jahazi

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Huku ikiwa bado Mbeba Maono Tundu Lissu kukanyaga ardhi ya Kyela, tayari CCM imeanza kupukutika yenyewe mithili ya mti wakati wa kiangazi, makovu ya kura za maoni yanaendelea kuitesa baada ya wapambe wa Mwakyembe kujiapiza na kugoma kumnadi wala kumpa kura zao mgombea wa CCM Ally Jumbe ambaye wanadai alikuwa mbeba mafaili wa Mwakyembe aliyesaliti kambi.

Taarifa zinadokeza kwamba mikutano mizito na mikubwa ya Mgombea Ubunge wa CHADEMA Mhe. Alinanuswe Mwalwange na hasa umati uliohudhuria siku ya uzinduzi wa kampeni zake kwenye uwanja wa Tacoshiri kumeisambaratisha zaidi CCM huku wapambe wa Mwakyembe wakichekelea hasa baada ya kampeni za uzinduzi za CCM zilizotangulia kudoda kwenye uwanja wa siasa

FB_IMG_1600524937889.jpg

Juhudi za Mzee Mangula kuokoa jahazi zimegonga mwamba
 
Kwa mara ya kwanza kyela itaongozwa na wapigania HAKI na MAENDELEO yaani CHADEMA. Nilikuja mwezi uliopita ukifika tu hapo njia panda ya Busokelo na Matema unapokelewa na bango kubwa la mgombea ubunge CHADEMA.[emoji851]

#Waliozoeakuishikwauongokamwehawawezikuishikwaukweli
 
We kajamaa unakuwa muongo mpaka unajichanganya kwa hiyo unataka kutuaminisha kwamba bila mpasuko CDM hawashindi .
 
Sidhani CCM ninayoijua ya sasa kama ina upambe na wapambe! Nasema sidhani.
 
Chadema mnapagawa, mtajua 28/10/2010 kama CCM imechokwa na mgombea wenu muongo muongo
 
Back
Top Bottom