CCM : Matokeo haya ni hazina kwetu

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,137
Reaction score
17,908
Ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni. Kada mmoja maarufu wa CCM ambaye pia ni Mjumbe mpya wa Kamati Kuu ya CCM ametoa mpya. Amesema kuwa matokeo ya Kidato cha Nne,kama yalivyo, ni hazina kubwa kwa Chama cha Mapinduzi. Ni Mjumbe anayetokea mkoa wa Dar es Salaam.

Bila hata ya haya yoyote,na wenzanke kutokumshangaa na badala yake kumshangilia, Mjumbe huyo wa CC ya CCM amesema: ' wale wote waliopata daraja la kwanza hadi la tatu si mali yetu. Hawa watapangwa kwenye Mashule ambayo kwasasa yamejaa upinzani hasa CHADEMA. Hawa wakifika hata Vyuo Vikuu watatusumbua na kutugeuka.'

'Lakini waliopata daraja la nne na sifuri ni hazina yetu. Hawa wakitumiwa vyema wataweza kujengewa utiifu kwa chama na kukipa ushindi hapo mwaka 2014 na 2015 kwenye chaguzi.' aliongeza Mjumbe huyo bila soni yoyote.

' Wa daraja la nne na sifuri watabaki na kazi za ngazi za chini kama ualimu au ukulima ambazo ni tiifu sana kwa chama tawala' alimalizia kusema mchaguliwa mpya huyo wa CC ya CCM.

Ilikuwa ni jana katika kikao cha kawaida cha chama kinachofanyika kila Jumatano Ofisi Ndogo za CCM Lumumba-Dar. Hata baadhi ya wajumbe wa kikao hicho walionesha kuchukia na kusikitishwa na kauli ya m-CC huyo kijana.

Je,tutafika?
VUTA-NKUVUTE wa Lumumba-Dar es Salaam
 
Last edited by a moderator:
Kwanini msifike na CCM yenu yenye mipango ya kuifanya nchi hii kuwa ya mambumbumbu?Kuanzisha shuel za kata wakati vitendea kazi na walimu hakuna mlijua matokeo yake ndio maana sishangai huyo mwanachama akisifia ujinga huu wa kufeli kwa vijana wetu,na utaona kama kuna wa kumchukulia hatua kwa kauli yake mbaya.
 
Ni vigumu kuamini kama kauli ya namna inaweza kutoka kwa binadamu mwenye kuwapenda wenzake kama anavyojipenda mwenyewe. Ila kwa vile mgombea wa Republican Mit Romney alitoa kauli za kuligawa taifa kama hivi naweza kujizuia nisishangae, maana dunia tunayoishi leo ni shughuli.
 
Kumbe kudumaza elimu, ili kuunda taifa la mbumbu na ombaomba na wachuuzi, ilikuwa ni miongoni mwa malengo ya shule za Kata, malengo mengine ni kuzuia ndoa za utotoni. Tanzania eeeee... Nchi yangu eee....
 
Hivi kumbe wanafunzi wanafelishwa kwa lengo la kuikomoa CHADEMA,

Imefikia mahali suala la ELIMU linaendeshwa kisiasa na kumuharibia mtanzania maisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…