VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
Ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni. Kada mmoja maarufu wa CCM ambaye pia ni Mjumbe mpya wa Kamati Kuu ya CCM ametoa mpya. Amesema kuwa matokeo ya Kidato cha Nne,kama yalivyo, ni hazina kubwa kwa Chama cha Mapinduzi. Ni Mjumbe anayetokea mkoa wa Dar es Salaam.
Bila hata ya haya yoyote,na wenzanke kutokumshangaa na badala yake kumshangilia, Mjumbe huyo wa CC ya CCM amesema: ' wale wote waliopata daraja la kwanza hadi la tatu si mali yetu. Hawa watapangwa kwenye Mashule ambayo kwasasa yamejaa upinzani hasa CHADEMA. Hawa wakifika hata Vyuo Vikuu watatusumbua na kutugeuka.'
'Lakini waliopata daraja la nne na sifuri ni hazina yetu. Hawa wakitumiwa vyema wataweza kujengewa utiifu kwa chama na kukipa ushindi hapo mwaka 2014 na 2015 kwenye chaguzi.' aliongeza Mjumbe huyo bila soni yoyote.
' Wa daraja la nne na sifuri watabaki na kazi za ngazi za chini kama ualimu au ukulima ambazo ni tiifu sana kwa chama tawala' alimalizia kusema mchaguliwa mpya huyo wa CC ya CCM.
Ilikuwa ni jana katika kikao cha kawaida cha chama kinachofanyika kila Jumatano Ofisi Ndogo za CCM Lumumba-Dar. Hata baadhi ya wajumbe wa kikao hicho walionesha kuchukia na kusikitishwa na kauli ya m-CC huyo kijana.
Je,tutafika?
VUTA-NKUVUTE wa Lumumba-Dar es Salaam

Last edited by a moderator: