SI KWELI PreGE2025 CCM mkoa wa Simiyu wagomea mkutano mkuu kwa njia ya mtandao

SI KWELI PreGE2025 CCM mkoa wa Simiyu wagomea mkutano mkuu kwa njia ya mtandao

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Source #1
View Source #1
Kimenuka

CCMSIMIYU25JUL2025.jpg
 
Tunachokijua
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeitisha mkutano mkuu wa njia ya mtandao Julai 26, 2025 ukiwa na ajenda ya kufanya maboresho ya katiba.

Madai

Kumeibuka taarifa kwa umma yenye utambulisho wa Chama Cha Mapinduzi ikidaiwa kutoka mkoa wa Simiyu ikieleza kuwa chama hicho kwa mkoa wa Simiyu hawatoshiriki katika mkutano ulioitishwa na chama hicho Julai 26, 2025 kwa ajili ya marekebisho ya katiba.

Uhalisia wa Taarifa hiyo

JamiiCheck imefuatilia na kubaini kuwa taarifa hiyo si ya kweli.

Ufuatiliaji umebaini kuwa taarifa hiyo haijatolewa na chama hicho kwa mkoa wa Simiyu kama inavyoonekana bali ni ya kughushi na ina mapungufu kadhaa ikiwemo kukosa Sahihi ya ya mwenyekiti huyo wa mkoa.

JamiiCheck imewasiliana na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu Shemsa Mohamed:

"Hiyo barua sio ya kweli ni fake, mimi au ofisi yangu haijaandika barua ya aina hiyo, kwa sasa nipo NEC, mimi na Wajumbe wote tutashiriki kikao cha kesho na wala hakuna shida ya Mtandao kama ilivyoandikwa, kwanza hiyo barua hata haijasainiwa, hivyo ipuuzeni ni barua fake."
Kama ni kweli,ni waluga luga tu hao............TAA ilizaa,TANU,ikazaa CCM........hivi ni vyama vya watu wa pwani,watoto wa mjini.......harakati za uhuru kuna namna zilianzia pwani regions and coastal zone yote.

Wakina mulikaribishwa tu kwenye harakati,hamuna nguvu yeyote ile,musijisahaulishe
 
Kama ni kweli,ni waluga luga tu hao............TAA ilizaa,TANU,ikazaa CCM........hivi ni vyama vya watu wa pwani,watoto wa mjini.......harakati za uhuru kuna namna zilianzia pwani regions and coastal zone yote.

Wakina mulikaribishwa tu kwenye harakati,hamuna nguvu yeyote ile,musijisahaulishe
Harakati za uhuru zilianzia Arusha, hao wa pwani wakaiga.
Viongozi walio leta uhuru wanatoka kanda ya ziwa.
 
Hapo muhimu ni hilo la kutujuza kuwa KATIBA inabadilishwa, hayo mengine hayana effect yoyote kwa watawala wenu...hawashindwi hata kupiga bomu mkoa mzima mkiendelea na kelele.

Swali la msingi, KATIBA inabidilishwa ili kuwaje? Kuna mambo ya baharini baharini kulainisha njia yao bara au?
 
1. Simiyu
2. Mara
3. Geita
4. Shinyanga
5. Kilimanjaro
6. Arusha
7. Mbeya
8.
9.
 

Attachments

  • IMG-20250725-WA0000.jpg
    IMG-20250725-WA0000.jpg
    88.8 KB · Views: 36
Hapo wanajisumbua tu hakuna mkoa utakao kubali kufanya kikao kwa njia ya mtandao huu ni upumbavu na ulafi na ubinafsi wa wazi kabisa na uvunjifu wa katiba yao wenyewe na sheria za nchi
 
FRIDA KAAYA ADAIWA KUVURUGA UCHAGUZI WA UWT WILAYA YA MOSHI MJINI

Katibu wa CCM Wilaya ya Moshi Mjini Frida Kaaya amedaiwa kutaka kuharibu Uchaguzi wa UWT Wilaya ya Moshi Mjini baada ya kutuhumiwa kujaribu kuiba kura za Mgombea wake ambaye ni katibu wa CCM Kata ya Kiusa Yobineshi Mafie.

Katibu huyo amedaiwa kuchakachua kura wakati wa zoezi la kuhesabu kura ambapo kura zilizoharibika na za wengine alikuwa akimpatia mgombea wake jambo lililopelekea mabishano na wagombea wengine kabla ya Msimamizi wa Uchaguzi huo kuingilia kati.

Inadaiwa katibu huyo aliwaagiza makatibu wote wa CCM kata kwenda eneo la Mkutano na kumuombea kura mgombea wake huku baadhi yao wakihusishwa na vitendo vya rushwa hali iliyopelekea TAKUKURU kuwafukuza katika eneo hilo huku Mgombea udiwani kata ya Mjimpya Rashid Maarufu BABA MZAZI ambaye ni mtu wa karibu sana na Katibu huyo wa wilaya kufukuzwa eneo hilo baada ya kukuta akinunulia wajumbe chai na vinywaji.

Hata hivyo mgombea huyo alishindwa vibaya sana katika uchaguzi huo uliendeshwa kwa uwazi, haki na usawa na wagombea wote kukubari matokeo na kusaini fomu za matokeo kama kanuni zinavyoelekeza.

Katika hali ya kushangaza Katibu huyu wa CCM Wilaya alimshauri na kumsaidia mgombea wake kukata rufaa akidai kuwa hakuridhishwa na mchakato wa Uchaguzi hivyo anaomba uchaguzi urudiwe na huku akijinasibu kuwa atagharamia gharama zote za uchaguzi. Kitendo cha Katibu wa CCM wilaya kutumia nguvu kubwa kumsaidia mgombea wake, kumewavuruga wajumbe na kumshangaa kwa nini yeye ambaye kanuni za Uchaguzi zinamtambua kama mkurugenzi wa Uchaguzi anajiingiza kwenye makundi ya kuwabeba wagombea.

Tunaomba mamlaka zinazohusika kuchukua hatua za haraka kudhibiti vitendo hivi kwani vinaashiria kuwepo kwa mambo ya kihuni katika uchaguzi ujao wa wabunge na madiwani.
 
Back
Top Bottom