Tangu tupate Uhuru, mwaka 1961, mpaka leo 2025 tunaongozwa na Serikali ya CCM. Maana yake Chama hiki ni kikongwe, kimezeeka. Kimetutoa huko na kutufikisha hapa tulipo.
Katika kipindi hiki chote Cha utawala wa CCM, yako mazuri lakini pia zipo changamoto zinazotukabili kama Taifa ambapo imefika wakati kelele za wananchi wanaotaka reforms zinazidi kuongezeka.
Wananchi wanatamani kuona raslimali zao zinatumika vizuri zaidi ya ilivyo sasa, wanataka kuwa na maisha bora kuliko ilivyo sasa, wanatamani kuona mdudu rushwa anapungua zaidi livyo Sasa, wanatamani kuona viongozi wanaowachagua hawageuki miungu watu, watu wanaoogopwa badala ya kuheshimwa.
Mabadiriko haya yanapatikana kwenye sanduku la kura. Lakini kwa bahati mbaya sana au kwa makusudi, CCM haitaki kuwepo ushindani linganifu kwa vyama vya Siasa. Malalamiko ni mengi kuhusu Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Kitendo kingine cha uoga wa CCM ni kutengeneza mazingira kwa vyama vya upinzani ambavyo inataka ishindane navyo kwenye Uchaguzi.
Napenda sana mfumo wa CCM kutaka Vijana ndio wagombee nafasi mbalimbali za Uchaguzi na kwamba wapewe kipaumbele.
Lakini kwa vile mfumo wa uongozi wa CCM na falsafa zake umezeeka, hata hao vijana hawatakidhi matamanio na matarajio ya wananchi.
Kwa hiyo, kwa vile tulikubali kuwepo kwa mfumo wa Vyama vingi vya Siasa, na Kwa vile nchi hii ni ya kwetu wote, CCM ikubali kuweka mazingira sawa ya kiushindani ili na wengine tuwapime.