Mmeondolewa na hamna mtakachofanya. Mtabaki kubweka tu mitandoani.Naenda kwenye mada moja kwa moja.
CCM mmefanya uteuzi wa makatibu wakuu nchi nzima, jambo ambalo ni nadra kufanyika au halijawahi kufanyika tangu tumepata uhuru.
Kwamba anaingia mwanachama wa chama CCM kushika wadhifa wa urais.Anashika pia wadhifa wa uenyekiti wa chama
Kisha anaanza kupangua safu yoote ya uongozi kuanzia ngazi ya taifa mpaka wilayani.
Hao watu unaowapangua ndio watendaji wa mashinani wanaokijua chama,kuliko hao vigogo mnaokaa nao huko makao makuu.
Lakini pia hata hao wakubwa wa chama unaowateua huko juu pia hawana uzoefu na siasa za CCM ikiwemo pia kutowajua wajumbe mikoani na jinsi ya ku deal nao.
Tumewaona wakipita wakitoa matamko ya kiserikali zaidi, kuliko ya kichama.
Kwa ufupi tu niseme wazi uamuzi huu meenyekiti hukushauriwa vizuri.
Hili kundi ni kubwa sana na kuliondoa kwa wakati mmoja, ukizingatia wao pia wana mitandao yao mpaka mashinani.
2025 hiyo unayojiandalia mwenyekiti usishangae lolote usiloweza kuamini likitokea, ukizingatia kwamba hata hao wabunge ni wageni wa siasa za majukwaani.
Upinzani wa kweli ndio unaweza kuzaliwa sasa.
Kama umefanya mapinduzi kuondoa mfumo mzima wa JPM, (ingawa hii ni tafsiri isiyo rasmi).
Angalieni tusije kutana wote vijiweni.
Huenda Kwa umefanya haya kwa sababu ambazo wananchi wa kawaida hatuzijui.
Lakini kwa wananchi wengi mashinani huko site wakawa na tafsiri yao tofauti,kama watatokea wa kuwashawishi na kuwaeleza vinginevyo na wakamuamini.
Alamsikh!
True Keyboard warriors🤣🤣