CCM mna mpango wa kuwaambia nini Watanzania wakati wa kampeni?

CCM mna mpango wa kuwaambia nini Watanzania wakati wa kampeni?

Upekuzi101

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2020
Posts
221
Reaction score
542
Hivi kwa Tanzania ya sasa CCM Ina mpango wa kuwaambia nini wamachinga, mamantilie, wakulima, wafugaji, wachimbaji wadogo, Wafanyabiashara wadogo wanafunzi wa elimu ya juu na day workers nini pale watakapokuja kuomba kura.

Mind you, hili ndo kundi kubwa la wapiga kura na ndio kundi linalokutana na matokeo ya uborongaji wa mama.
 
Hawana tatizo kwani ni wao pekee ndio wanaruhusiwa kufanya kampeni mwaka mzima.
 
We unaishi dunia gani mpaka usione kazi inayofanywa na ccm???
Nyie watu wa viwango vya chini ndio mnaiona, wenzenu wa viwango vya juu huko uingereza yule mdada na waziri wake wa fedha hawakumaliza wiki nje, hizo ndizo nchi zenye watu wa viwango vya juu siyo nyie mnashangilia visima vya miaka ya 40!
 
Hawa ndo wazee wa burudani raundi hii kwaiyo kinachoendelea huku chini haelewi kabisa.
 
Ushaona wapi Tapeli au Dalali anakosa maneno matamu ya kumshawishi mteja aingie kingi!
 
Wapo wanachelewesha mradi wa Nyerere, watauzindua 2025 kuelekea uchaguzi... Watajinadi wameweza kutatua shida ya umeme iliyokuwa inatukabili
 
Back
Top Bottom