CCM, mnajua hatari mnayohubiri kwenye KUUA binadamu?

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,917
SIASA ya nchi yetu imechukua sura mpya sana katika awamu hii ya tano. Tumerejea hatua nyingi nyuma katika kuheshimu misingi ya demokrasia na haki ya kijamii, utawala bora na Uhuru binafsi. Hatuna tofauti na tawala za KIBABE za nyakati za kitambo huko Marekani ya kusini. Tupo sehemu mbaya.

Viongozi wastaafu wapo kimya. Nao wameingiwa na hofu? Hawajui ni hatari sana wao wakiendelea kukaa kimya wakati wana CCM wa sasa wakihubiri kuua, kuteka, kutesa hadharani? Nchi yetu ikiharibika na machafuko hata wao na Ndugu zao wataumia. Wasikae kimya. Wakatae hadharani uovu.

Kuna gharama kubwa sana kuongozwa na chama kilichokataa tamaa, kimepagawa, ni kimefika Mwisho kuzalisha fikra mpya (timamu) na sasa wanafikiria kuwaua watu wengine wanaotofautiana nao fikra, mtazamo na itikadi. CCM wamepagawa. Hawafanyi siasa tena.

CCM sasa sio chama cha siasa. CCM imefilisika hoja na uwezo wa kutengeneza viongozi timamu. Wamebaki wafuasi na walamba nyayo. CCM imejinasibisha na DOLA. wapinzani wa CCM wanapambana na DOLA na mfumo na sio CCM (dead horse). CCM ni kitu mfu sasa. Haipo CCM kuna dola.

Kufikiria kutoa uhai wa mtu mwingine kwa namna yoyote ile ni kiwango/hatua ya Mwisho kabisa kuelekea kufilisika hata uwezo wa ubongo kufanya kazi. Maana yake ubongo umeshindwa kufikiri njia mbadala, umeamua kutoa suluhisho la "kuua". Ubungo uliopooza ( paralyze) ndio haufanyi kazi tena.

Mbunge wa CCM, (ambaye ni mbunge wa kuteuliwa na Rais) Abdallah Bulembo anasimama bungeni,kwa sauti na madoido na kumtuhumu Zitto Kabwe (kwa usaliti?) na anasema Zitto Kabwe hapaswi kurejea nchini, auwawe huko nje ya nchi. Spika wa bunge yupo kimya na wabunge wa CCM wanashangilia.

Kinachotia kinyaa zaidi ni mama anayejiita 'mtumishi wa Mungu' Gertrude Rwakatare (ambaye pia no mbunge wa kuteuliwa na Rais) anapiga makofi pembeni ya Bulembo na kushangilia kauli za kuua binadamu, na baadae atahubiri haki, mshikamano na utulivu kwenye jamii, na ataeleweka, watanzania ni wepesi kuwamudu.

Serikali ya awamu ya tano inajinasibu kufanya maendeleo makubwa ya kiuchumi yenye kugusa watu, kwanini wapambe wa serikali hii, viongozi wake wanakataa kukosolewa? Kwanini wasijitokeze kwa wananchi na kusema maendeleo hayo, wananchi wawashangilie?

Serikali ambayo imejenga SGR, inajenga SGHEP, ikaleta ndege zaidi ya 11, imeleta umeme kila kijiji, imepeleka Maji kila familia nchi nzima, imejenga barabara, imetengeneza Meli, viongozi wake wanaogopa kukosolewa? Hadi hadharani wanasema wanaikosoa serikali yao wanapaswa kuuwawa?

Serikali ambayo imewalipa 'cash' wakulima wa Korosho, ikawalipa 'cash' wakulima wa Pamba, wakulima wa Mbaazi, dengu wanafurahia bei ya bidhaa zao, soko la nje limefunguka, kwenda India kupeleka mazao ni rahisi, inaogpa kukosolewa? Au wanayotupa simulizi ni ya uongo?

Kama huwezi kutetea Hoja zako, huwezi kuitetea serikali yako na umeshindwa kuitetea CCM hadharani (huna hoja) unataka na ambao wanaweza kuikosoa serikali wanyamaze kimya? Wakifanya majukumu yao ya kuikosoa serikali mnakasirika? Mnatamani kuwaua? Mmekuwa watu wa hovyo!

Mwenyekiti wa UVCCM ni mjumbe wa NEC, mjumbe wa kamati kuu ya CCM Taifa, mjumbe wa mkutano mkuu Taifa. Huyu anawajibu wa kumshauri mwenyekiti wa CCM Taifa kuhusu masuala ya sera za vijana, ajira, uchumi, usalama, Amani na utulivu. Kwa akili hizi, atafanya hayo?

Kheri James anaagiza vijana wake wawashambulie, kuwajeruhina kuwaua viongozi wa upinzani ambao wanatoa maoni yao yenye kupingana na serikali ya CCM. Haya ni Mawazo ya mwenyekiti wa vijana wa CCM Taifa hadharani. Sirini Je? Mnajadiliana kuhusu kuwaua wapinzani wenu kisiasa?

Huyo ambaye mnapanga kumuua, mnadhani hana familia, ukoo, marafiki? Kwamba mnaweza kumuua mtu kwa sababu haipendi CCM na ninyi mkaendelea kuwa salama tu? Hamjui kuna nguvu kubwa katika kulipiza kisasi? Mtamwaga damu zenu nyingi kuliko hao wapinzani. Kaeni kwa kutulia.

Polisi wametulia kimya. Wanasikia yote yanayoendelea. IGP yupo kimya. Hapo anasubiri mwanasiasa wa upinzani asimame, aseme kama huyu Bulembo (wamkamate na kumpa mashtaka ya ugaidi, uchochezi au uhujumu uchumi). Tunaishi kwenye nchi iliyoharibika sana. Imeharibiwa na CCM kwa kiwango KIKUBWA.

Godbless Lema, mwaka 2017 alikamatwa na kuwekwa mahabusu ya gereza la Kisongo, ARUSHA kwa zaidi ya miezi 4 kwa kosa la kutoa simulizi bungeni, yenye kuhusu ndoto ambayo ilimuonesha JPM atafariki. Kosa! Ndoto ikapewa mashtaka ya uchochezi. Maajabu! Awamu hii ya Awafu mwenye nguvu.

Mwaka 2017, ikulu DSM, wakati wa kupokea taarifa ya kamati ya Madini (Tanzanite na Almasi), Rais Magufuli alitoa tuhuma za Usaliti kwa "mtu/watu" na akasisitiza wasaliti wanachofanywa kwa mbinu za kiaskari. Alisema "wamedukua" maongezi ya huyo mtu na Mwanyika na wamegundua usaliti wake.

Usaliti wake ni upi mtu huyo ambaye hakutajwa? (wengine tunajua nani alikuwa akizungumziwa) usaliti wake ni kuomba nyaraka (documents) za mikataba ya BARRICK na Serikali. Huu ndio usaliti? Kwamba mtanzania hapaswi kufahamu yenye kuhusu nchi yake kwenye mikataba? Ni kosa la jinai? Dhambi?

Ok! Siku hiyo, saa chache baadae, Tundu Lissu akitoka bungeni kwenda nyumbani kwake, saa saba mchana, Jua kali, alishambuliwa kwa risasi nyingi na risasi 16 ziliingia katika mwili wake. Waliomshambulia Tundu Lissu kwa risasi hadi sasa hawajawahi kujulikana. Inashangaza.

Sasa tunaona viongozi wa CCM wakisema hadharani bila hofu kuhusu kuwaua wapinzani, wakosoaji wa serikali, wanaharakati wa haki za binadamu. Wakiwapa majina mabaya kwanza, wasaliti. Ili jamii ikubali kwamba wapinzani hao kwa sababu ya wao kukataa kusimama na CCM ni usaliti.

CCM imefilisika. Hawajui kukubali katika kutokubaliana pia ni demokrasia? Sio lazima kila kitu kama taifa wananchi mkubaliane. Ndio maana katika uchaguzi mkuu wa 2015 kuna watanzania zaidi ya milioni 6 hawakumchagua Magufuli aliyekuwa mgombea wa CCM. Hawa watanzania bado wapo. Mnawaua wote?
 
Ukitaka kijua hatari ya aina ya siasa za baadhi ya viongozi wa ccm, fuatilia siasa za viongozi wa kisiasa wa Rwanda kuanzia mwaka 92-94 alafu uliza baada ya mbwembwe na siasa za chuki leo wako wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilikua naangali documentary ya holocaust in the then German-occupied Europe, mambo yalianza hivi hivi, tuna kitu cha kujifunza kwenye historia hizi
 
Hahaha mwanadamu anapo muwinda mnyama kwa kitoweo huwa haoni machozi ya mnyama anayemuwinda, yeye ana concentrate kutekeleza hisia zake.

Sasa hao ndio ccm, wao wanajiita ccm mpya.

Hawajali kuua, as long as wao wanabaki madarakani.
 
CCM wamejigeuza na kuwa kikundi cha kigaidi mbaya zaidi wamepanga mauaji ya Zitto Bungeni Mubashara na ushahidi upo.
 
SIASA ya nchi yetu imechukua sura mpya sana katika awamu hii ya tano. Tumerejea hatua nyingi nyuma katika kuheshimu misingi ya demokrasia na haki ya kijamii, utawala bora na Uhuru binafsi. Hatuna tofauti na tawala za KIBABE za nyakati za kitambo huko Marekani ya kusini. Tupo sehemu mbaya.

Viongozi wastaafu wapo kimya. Nao wameingiwa na hofu? Hawajui ni hatari sana wao wakiendelea kukaa kimya wakati wana CCM wa sasa wakihubiri kuua, kuteka, kutesa hadharani? Nchi yetu ikiharibika na machafuko hata wao na Ndugu zao wataumia. Wasikae kimya. Wakatae hadharani uovu.

Kuna gharama kubwa sana kuongozwa na chama kilichokataa tamaa, kimepagawa, ni kimefika Mwisho kuzalisha fikra mpya (timamu) na sasa wanafikiria kuwaua watu wengine wanaotofautiana nao fikra, mtazamo na itikadi. CCM wamepagawa. Hawafanyi siasa tena.

CCM sasa sio chama cha siasa. CCM imefilisika hoja na uwezo wa kutengeneza viongozi timamu. Wamebaki wafuasi na walamba nyayo. CCM imejinasibisha na DOLA. wapinzani wa CCM wanapambana na DOLA na mfumo na sio CCM (dead horse). CCM ni kitu mfu sasa. Haipo CCM kuna dola.

Kufikiria kutoa uhai wa mtu mwingine kwa namna yoyote ile ni kiwango/hatua ya Mwisho kabisa kuelekea kufilisika hata uwezo wa ubongo kufanya kazi. Maana yake ubongo umeshindwa kufikiri njia mbadala, umeamua kutoa suluhisho la "kuua". Ubungo uliopooza ( paralyze) ndio haufanyi kazi tena.

Mbunge wa CCM, (ambaye ni mbunge wa kuteuliwa na Rais) Abdallah Bulembo anasimama bungeni,kwa sauti na madoido na kumtuhumu Zitto Kabwe (kwa usaliti?) na anasema Zitto Kabwe hapaswi kurejea nchini, auwawe huko nje ya nchi. Spika wa bunge yupo kimya na wabunge wa CCM wanashangilia.

Kinachotia kinyaa zaidi ni mama anayejiita 'mtumishi wa Mungu' Gertrude Rwakatare (ambaye pia no mbunge wa kuteuliwa na Rais) anapiga makofi pembeni ya Bulembo na kushangilia kauli za kuua binadamu, na baadae atahubiri haki, mshikamano na utulivu kwenye jamii, na ataeleweka, watanzania ni wepesi kuwamudu.

Serikali ya awamu ya tano inajinasibu kufanya maendeleo makubwa ya kiuchumi yenye kugusa watu, kwanini wapambe wa serikali hii, viongozi wake wanakataa kukosolewa? Kwanini wasijitokeze kwa wananchi na kusema maendeleo hayo, wananchi wawashangilie?

Serikali ambayo imejenga SGR, inajenga SGHEP, ikaleta ndege zaidi ya 11, imeleta umeme kila kijiji, imepeleka Maji kila familia nchi nzima, imejenga barabara, imetengeneza Meli, viongozi wake wanaogopa kukosolewa? Hadi hadharani wanasema wanaikosoa serikali yao wanapaswa kuuwawa?

Serikali ambayo imewalipa 'cash' wakulima wa Korosho, ikawalipa 'cash' wakulima wa Pamba, wakulima wa Mbaazi, dengu wanafurahia bei ya bidhaa zao, soko la nje limefunguka, kwenda India kupeleka mazao ni rahisi, inaogpa kukosolewa? Au wanayotupa simulizi ni ya uongo?

Kama huwezi kutetea Hoja zako, huwezi kuitetea serikali yako na umeshindwa kuitetea CCM hadharani (huna hoja) unataka na ambao wanaweza kuikosoa serikali wanyamaze kimya? Wakifanya majukumu yao ya kuikosoa serikali mnakasirika? Mnatamani kuwaua? Mmekuwa watu wa hovyo!

Mwenyekiti wa UVCCM ni mjumbe wa NEC, mjumbe wa kamati kuu ya CCM Taifa, mjumbe wa mkutano mkuu Taifa. Huyu anawajibu wa kumshauri mwenyekiti wa CCM Taifa kuhusu masuala ya sera za vijana, ajira, uchumi, usalama, Amani na utulivu. Kwa akili hizi, atafanya hayo?

Kheri James anaagiza vijana wake wawashambulie, kuwajeruhina kuwaua viongozi wa upinzani ambao wanatoa maoni yao yenye kupingana na serikali ya CCM. Haya ni Mawazo ya mwenyekiti wa vijana wa CCM Taifa hadharani. Sirini Je? Mnajadiliana kuhusu kuwaua wapinzani wenu kisiasa?

Huyo ambaye mnapanga kumuua, mnadhani hana familia, ukoo, marafiki? Kwamba mnaweza kumuua mtu kwa sababu haipendi CCM na ninyi mkaendelea kuwa salama tu? Hamjui kuna nguvu kubwa katika kulipiza kisasi? Mtamwaga damu zenu nyingi kuliko hao wapinzani. Kaeni kwa kutulia.

Polisi wametulia kimya. Wanasikia yote yanayoendelea. IGP yupo kimya. Hapo anasubiri mwanasiasa wa upinzani asimame, aseme kama huyu Bulembo (wamkamate na kumpa mashtaka ya ugaidi, uchochezi au uhujumu uchumi). Tunaishi kwenye nchi iliyoharibika sana. Imeharibiwa na CCM kwa kiwango KIKUBWA.

Godbless Lema, mwaka 2017 alikamatwa na kuwekwa mahabusu ya gereza la Kisongo, ARUSHA kwa zaidi ya miezi 4 kwa kosa la kutoa simulizi bungeni, yenye kuhusu ndoto ambayo ilimuonesha JPM atafariki. Kosa! Ndoto ikapewa mashtaka ya uchochezi. Maajabu! Awamu hii ya Awafu mwenye nguvu.

Mwaka 2017, ikulu DSM, wakati wa kupokea taarifa ya kamati ya Madini (Tanzanite na Almasi), Rais Magufuli alitoa tuhuma za Usaliti kwa "mtu/watu" na akasisitiza wasaliti wanachofanywa kwa mbinu za kiaskari. Alisema "wamedukua" maongezi ya huyo mtu na Mwanyika na wamegundua usaliti wake.

Usaliti wake ni upi mtu huyo ambaye hakutajwa? (wengine tunajua nani alikuwa akizungumziwa) usaliti wake ni kuomba nyaraka (documents) za mikataba ya BARRICK na Serikali. Huu ndio usaliti? Kwamba mtanzania hapaswi kufahamu yenye kuhusu nchi yake kwenye mikataba? Ni kosa la jinai? Dhambi?

Ok! Siku hiyo, saa chache baadae, Tundu Lissu akitoka bungeni kwenda nyumbani kwake, saa saba mchana, Jua kali, alishambuliwa kwa risasi nyingi na risasi 16 ziliingia katika mwili wake. Waliomshambulia Tundu Lissu kwa risasi hadi sasa hawajawahi kujulikana. Inashangaza.

Sasa tunaona viongozi wa CCM wakisema hadharani bila hofu kuhusu kuwaua wapinzani, wakosoaji wa serikali, wanaharakati wa haki za binadamu. Wakiwapa majina mabaya kwanza, wasaliti. Ili jamii ikubali kwamba wapinzani hao kwa sababu ya wao kukataa kusimama na CCM ni usaliti.

CCM imefilisika. Hawajui kukubali katika kutokubaliana pia ni demokrasia? Sio lazima kila kitu kama taifa wananchi mkubaliane. Ndio maana katika uchaguzi mkuu wa 2015 kuna watanzania zaidi ya milioni 6 hawakumchagua Magufuli aliyekuwa mgombea wa CCM. Hawa watanzania bado wapo. Mnawaua wote?
Sasa hivi kimekua chama cha kutoa roho wakosoaji wake
IMG_20200204_085031.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Angekua mbunge wa "UPINZANI" ndio ameongea hayo ya kuuliwa mbunge wa CCM, basi angepotezwa na kufunguliwa kesi ya "UHUJUMU UCHUMI, KUKWEPA KODI NA KUTISHIA KUUA". Ila CCM wanajiona wako sawa na wana kinga maalum.

Muda ni rafiki, wana CCM mtaondolewa bungeni na mtapoteza hio kinga yenu, mtarudi mtaani.
 
Mwanahabari Huru,
Huna haja ya kuwakumbusha mkuu acha tukusanye ushahidi kwa ajili ya ICC. Ninasanya clips. Sasa hivi ni za
1. Job Ndugai
2. Abdallah Bulembo
3. Bwana kihongosi wa Iringa

Wote hawa wataungana na akina Musiba.
Tuwashukuru kwa kutupa "leads" za alipo Ben Saanane, Azory Gwanda, Kanguye, waliojaribu kumuua Tundu Lissu, pamoja na wauwaji wa Alfonce Mawazo, Diwani wa Hananasif, na wengine
 
K
SIASA ya nchi yetu imechukua sura mpya sana katika awamu hii ya tano. Tumerejea hatua nyingi nyuma katika kuheshimu misingi ya demokrasia na haki ya kijamii, utawala bora na Uhuru binafsi. Hatuna tofauti na tawala za KIBABE za nyakati za kitambo huko Marekani ya kusini. Tupo sehemu mbaya.

Viongozi wastaafu wapo kimya. Nao wameingiwa na hofu? Hawajui ni hatari sana wao wakiendelea kukaa kimya wakati wana CCM wa sasa wakihubiri kuua, kuteka, kutesa hadharani? Nchi yetu ikiharibika na machafuko hata wao na Ndugu zao wataumia. Wasikae kimya. Wakatae hadharani uovu.

Kuna gharama kubwa sana kuongozwa na chama kilichokataa tamaa, kimepagawa, ni kimefika Mwisho kuzalisha fikra mpya (timamu) na sasa wanafikiria kuwaua watu wengine wanaotofautiana nao fikra, mtazamo na itikadi. CCM wamepagawa. Hawafanyi siasa tena.

CCM sasa sio chama cha siasa. CCM imefilisika hoja na uwezo wa kutengeneza viongozi timamu. Wamebaki wafuasi na walamba nyayo. CCM imejinasibisha na DOLA. wapinzani wa CCM wanapambana na DOLA na mfumo na sio CCM (dead horse). CCM ni kitu mfu sasa. Haipo CCM kuna dola.

Kufikiria kutoa uhai wa mtu mwingine kwa namna yoyote ile ni kiwango/hatua ya Mwisho kabisa kuelekea kufilisika hata uwezo wa ubongo kufanya kazi. Maana yake ubongo umeshindwa kufikiri njia mbadala, umeamua kutoa suluhisho la "kuua". Ubungo uliopooza ( paralyze) ndio haufanyi kazi tena.

Mbunge wa CCM, (ambaye ni mbunge wa kuteuliwa na Rais) Abdallah Bulembo anasimama bungeni,kwa sauti na madoido na kumtuhumu Zitto Kabwe (kwa usaliti?) na anasema Zitto Kabwe hapaswi kurejea nchini, auwawe huko nje ya nchi. Spika wa bunge yupo kimya na wabunge wa CCM wanashangilia.

Kinachotia kinyaa zaidi ni mama anayejiita 'mtumishi wa Mungu' Gertrude Rwakatare (ambaye pia no mbunge wa kuteuliwa na Rais) anapiga makofi pembeni ya Bulembo na kushangilia kauli za kuua binadamu, na baadae atahubiri haki, mshikamano na utulivu kwenye jamii, na ataeleweka, watanzania ni wepesi kuwamudu.

Serikali ya awamu ya tano inajinasibu kufanya maendeleo makubwa ya kiuchumi yenye kugusa watu, kwanini wapambe wa serikali hii, viongozi wake wanakataa kukosolewa? Kwanini wasijitokeze kwa wananchi na kusema maendeleo hayo, wananchi wawashangilie?

Serikali ambayo imejenga SGR, inajenga SGHEP, ikaleta ndege zaidi ya 11, imeleta umeme kila kijiji, imepeleka Maji kila familia nchi nzima, imejenga barabara, imetengeneza Meli, viongozi wake wanaogopa kukosolewa? Hadi hadharani wanasema wanaikosoa serikali yao wanapaswa kuuwawa?

Serikali ambayo imewalipa 'cash' wakulima wa Korosho, ikawalipa 'cash' wakulima wa Pamba, wakulima wa Mbaazi, dengu wanafurahia bei ya bidhaa zao, soko la nje limefunguka, kwenda India kupeleka mazao ni rahisi, inaogpa kukosolewa? Au wanayotupa simulizi ni ya uongo?

Kama huwezi kutetea Hoja zako, huwezi kuitetea serikali yako na umeshindwa kuitetea CCM hadharani (huna hoja) unataka na ambao wanaweza kuikosoa serikali wanyamaze kimya? Wakifanya majukumu yao ya kuikosoa serikali mnakasirika? Mnatamani kuwaua? Mmekuwa watu wa hovyo!

Mwenyekiti wa UVCCM ni mjumbe wa NEC, mjumbe wa kamati kuu ya CCM Taifa, mjumbe wa mkutano mkuu Taifa. Huyu anawajibu wa kumshauri mwenyekiti wa CCM Taifa kuhusu masuala ya sera za vijana, ajira, uchumi, usalama, Amani na utulivu. Kwa akili hizi, atafanya hayo?

Kheri James anaagiza vijana wake wawashambulie, kuwajeruhina kuwaua viongozi wa upinzani ambao wanatoa maoni yao yenye kupingana na serikali ya CCM. Haya ni Mawazo ya mwenyekiti wa vijana wa CCM Taifa hadharani. Sirini Je? Mnajadiliana kuhusu kuwaua wapinzani wenu kisiasa?

Huyo ambaye mnapanga kumuua, mnadhani hana familia, ukoo, marafiki? Kwamba mnaweza kumuua mtu kwa sababu haipendi CCM na ninyi mkaendelea kuwa salama tu? Hamjui kuna nguvu kubwa katika kulipiza kisasi? Mtamwaga damu zenu nyingi kuliko hao wapinzani. Kaeni kwa kutulia.

Polisi wametulia kimya. Wanasikia yote yanayoendelea. IGP yupo kimya. Hapo anasubiri mwanasiasa wa upinzani asimame, aseme kama huyu Bulembo (wamkamate na kumpa mashtaka ya ugaidi, uchochezi au uhujumu uchumi). Tunaishi kwenye nchi iliyoharibika sana. Imeharibiwa na CCM kwa kiwango KIKUBWA.

Godbless Lema, mwaka 2017 alikamatwa na kuwekwa mahabusu ya gereza la Kisongo, ARUSHA kwa zaidi ya miezi 4 kwa kosa la kutoa simulizi bungeni, yenye kuhusu ndoto ambayo ilimuonesha JPM atafariki. Kosa! Ndoto ikapewa mashtaka ya uchochezi. Maajabu! Awamu hii ya Awafu mwenye nguvu.

Mwaka 2017, ikulu DSM, wakati wa kupokea taarifa ya kamati ya Madini (Tanzanite na Almasi), Rais Magufuli alitoa tuhuma za Usaliti kwa "mtu/watu" na akasisitiza wasaliti wanachofanywa kwa mbinu za kiaskari. Alisema "wamedukua" maongezi ya huyo mtu na Mwanyika na wamegundua usaliti wake.

Usaliti wake ni upi mtu huyo ambaye hakutajwa? (wengine tunajua nani alikuwa akizungumziwa) usaliti wake ni kuomba nyaraka (documents) za mikataba ya BARRICK na Serikali. Huu ndio usaliti? Kwamba mtanzania hapaswi kufahamu yenye kuhusu nchi yake kwenye mikataba? Ni kosa la jinai? Dhambi?

Ok! Siku hiyo, saa chache baadae, Tundu Lissu akitoka bungeni kwenda nyumbani kwake, saa saba mchana, Jua kali, alishambuliwa kwa risasi nyingi na risasi 16 ziliingia katika mwili wake. Waliomshambulia Tundu Lissu kwa risasi hadi sasa hawajawahi kujulikana. Inashangaza.

Sasa tunaona viongozi wa CCM wakisema hadharani bila hofu kuhusu kuwaua wapinzani, wakosoaji wa serikali, wanaharakati wa haki za binadamu. Wakiwapa majina mabaya kwanza, wasaliti. Ili jamii ikubali kwamba wapinzani hao kwa sababu ya wao kukataa kusimama na CCM ni usaliti.

CCM imefilisika. Hawajui kukubali katika kutokubaliana pia ni demokrasia? Sio lazima kila kitu kama taifa wananchi mkubaliane. Ndio maana katika uchaguzi mkuu wa 2015 kuna watanzania zaidi ya milioni 6 hawakumchagua Magufuli aliyekuwa mgombea wa CCM. Hawa watanzania bado wapo. Mnawaua wote?
Kwa Uzi huu nami naomba uwe mda sheria ya mgombea binfsi ipite ili sisi tusiokua na vyama tusimamishe mgombea wetu na tukamate dola ili vyama vyenu vyote vibaki kua upinzani maana kwa sasa mnatuchanganya hii ndo dawa iliyobaki ili tunusuru taifa kwa nini mnagombana wakati lengo ni moja kwamba nikuleta maendeleo ya taifa na watu wake
Kwa nini hamkai kama vyama mkarekebisha mapungufu yaliyopo badala yake kila chama kinatunisha msuli juu ya kingine
Tanzania kama nchi ni zaidi ya chama chochote vyama vipo kama sehemu ya kupata uwakilishi wa kulitumikia taifa kwa maslai mapana ya wananchi sawa kila mtu ana dini yake ila lengo kuu ni kuuona ufalme wa mungu sasa kama lengo leno ni moja kwa nini mnagombana .kwa nini hasikilizani na kwa nini mnatukanana na kuombeana mabaya
Tafadhali tunaomba sheria ya mgombea binafsi irusiwe nasi tusio na vyama tuwaoneshe makali .
 
Mkitokea mkatupa haki iyo kwanza tutashinda mapema kwa nini nasema
1.sisi watembea kwa nguu,na wengine wengi tusiokua na uwezo wengi hatuna vyama
2.watumishi wa huma na vyombo vyote vya ulinzi wako kwetu maana hawana vyama ila wako kwa mjibu wa sheria
3.watumishi wa mahakama wote wanatimiza wajibu ila hawana vyama
4. Wapo wanachama wenu wengi watatuunga mkono maana wengi wamechoka na kelele na maugomvi yenu yasiokua na tija kwa taifa
NINI TUTAFANYA MKITUPATIA IYO FULSA
Kwanza tutaitaitaji mgombea ambae hajawai jiusisha na siasa hapa tutaitaji mtu yoyote ambaye yupo tiyari kuliongoza taifa bila kujali anatoka tahasisi gani hata kama yupo kazini tutamshauri kazi aache naamanisha hapa kutoka tahasisi yoyote iliyo kisheria hapa tz ila elimu pia lazima izingatiwe
NA IKITOKEA AKAPITA KAMA MTAPITSHA
1Kuhakikisha wateuzi wake wote katika nafasi tofauti wanateuliwa kulingana na uwezo binafsi sio mtu anatoka chama gani
2.nafasi zote zinazo usu uongozi wa chama hazitakuepo maana hatakua anatokana na chama Bali yataundwa mabaraza ya kutaifa bila kujali vyama
3.speaker wa bunge atatoka popote ili mradi tu awe na uwezo ambao wabunge wenzake wameukubali
4. Wakuu wa wilaya na mkoa lazima wapigiwe kura kudhibitishwa kwa chombo mahalum kitakachokua na mamlaka
TAFADHALI RUHUSINI MGOMBEA BINAFSI
 
Back
Top Bottom