GE2025 CCM Moshi: Fomu ya Ubunge ni 500,000 na Udiwani ni 50,000

GE2025 CCM Moshi: Fomu ya Ubunge ni 500,000 na Udiwani ni 50,000

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Moshi Vijijini kimewaita wanaotaka kugombea ubinge,udiwani na viti maalum kujitokeza kuchukua fomu huku wakitaja gharama ni Sh.500,000 na 50,000.

Aidha,kimepiga marufuku wagombea kuambatana na wagombea,shamrashamra za matarumbeta ngoma,misafara ya watu na pikipiki.

"Nanapenda kuwatangazia wanachama wote wa CCM wanaohitaji kugombea nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Vunjo na Moshi Vijijini wenye sifa zilizoainishwa katika kanuni za uteuzi wa wagombea uongozi vyombo vya dola toleo la Machi 2025 kifungu cha 2 (1iix) wana karibishwa kuja kuchukua fomu.

"Fomu zitaanza kutolewa hapa wilayani kwa Katibu wa CCM Wilaya kuanzia siku ya Jumamosi Juni 28, 2025 hadi Julai 2,2025 kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni.

Taarifa hiyo iliyotolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi CCM Wilaya ya Moshi Vijijini, Ramadhani Mahanyu imesema ada ya fomu ni Sh. 500,000 wabunge huku kwa udiwani ambazo zitatolewa kwa makatibu wa CCM katika Ofisi za CCM Kata.

"Mgombea anapokuja kuchukua fomu haruhusiwi kuna na shamrashamra za aina yeyote ile (matarumbeta,ngoma,misafara ya pikipiki,wala misafara ya watu au mbwembwe za aina yeyote ile."
1750931192273.png

chanzo: Nipashe​
 
Fomu ya ubunge ingekuwa 5m udiwani elfu 50
 
Back
Top Bottom