CCM MP has said that ATCL air hostesses are not attractive

CCM MP has said that ATCL air hostesses are not attractive

Teargass

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2018
Posts
20,648
Reaction score
17,772
Mbunge CCM asema wahudumu wa ATCL hawana mvuto kwa wateja

THURSDAY NOVEMBER 7 2019

Mbunge wa Kigoma Kusini nchini Tanzania (CCM)

Mbunge wa Kigoma Kusini nchini Tanzania (CCM) Husna Mwilima

Dodoma. Mbunge wa Kigoma Kusini nchini Tanzania (CCM) Husna Mwilima amesema wahudumu wa ndege wanaoajiriwa na Shirika la Ndege Nchini (ATCL) hawana mvuto kwa wateja.

Mwilima ameyasema hayo leo Alhamisi Novemba 7, 2019 wakati akichangia Mapendekezo ya Mpango wa Taifa wa Maendeleo bungeni jijini Dodoma. Mwilima amempongeza Rais John Magufuli kwa kutimiza ahadi yake ya kuifufua ATCL na kuwataka mawaziri pia kutimiza ahadi zao.

“Mheshimiwa waziri mimi nataka nitanie kidogo hizi ndege zetu zinafanya vizuri sana lakini mle ndani hebu tuangalie tunaowaajiri. Wale maair hostess (wahudumu) hata ukimuita mle ndani akigeuka abiria anaona kweli tuna maair hostess mle ndani,”amesema na kuongeza:

“Sijui mnatumia vigezo gani? Unakuta air hostess mfupi, hana mvuto wa kuifanya ndege zetu zionekane. Leo mimi hapa nimezeeka na miaka 50 na ukiniweka…”amesema kabla ya kukatishwa na utaratibu uliombwa na Mbunge wa Geita Vijijini (CCM), Joseph Musukuma.

Musukuma amesema huo ni ubaguzi na kwamba kuna wengine wanazaa watoto ambao hawana maumbo kama anayoyasema mbunge huyo.


Chanzo: Mwananchi
 
Hehehe watu wa "air hostage" wameongea😂😂
 
Mbunge wa Kigoma Kusini nchini Tanzania (CCM) Husna Mwilima amesema wahudumu wa ndege wanaoajiriwa na Shirika la Ndege Nchini (ATCL) hawana mvuto kwa wateja.

Mwilima ameyasema hayo leo Alhamisi Novemba 7, 2019 wakati akichangia Mapendekezo ya Mpango wa Taifa wa Maendeleo bungeni jijini Dodoma.

Mwilima amempongeza Rais John Magufuli kwa kutimiza ahadi yake ya kuifufua ATCL na kuwataka mawaziri pia kutimiza ahadi zao.

“Mheshimiwa waziri mimi nataka nitanie kidogo hizi ndege zetu zinafanya vizuri sana lakini mle ndani hebu tuangalie tunaowaajiri. Wale maair hostess (wahudumu) hata ukimuita mle ndani akigeuka abiria anaona kweli tuna maair hostess mle ndani,” amesema na kuongeza:

“Sijui mnatumia vigezo gani? Unakuta air hostess mfupi, hana mvuto wa kuifanya ndege zetu zionekane. Leo mimi hapa nimezeeka na miaka 50 na ukiniweka…”amesema kabla ya kukatishwa na utaratibu uliombwa na Mbunge wa Geita Vijijini (CCM), Joseph Musukuma.

Musukuma amesema huo ni ubaguzi na kwamba kuna wengine wanazaa watoto ambao hawana maumbo kama anayoyasema mbunge huyo.

Akiendelea kuchangia Mwilima amesema sifa ya mhudumu wa ndege ni lazima awe mrefu na amenyooka akiwa mwanaume ama mwanamke na kuomba jambo hilo lizingatiwe.


Chanzo: Mwananchi


ATCL YAJIBU, HATUAJIRI WANAWAKE KUONESHA UZURI

Wakati mbunge wa Kigoma Kusini (CCM), Husna Mwilima akisema wahudumu wa ndege za ATCL hawana mvuto kwa wateja, shirika hilo limesema haliwachagui kwa ajili ya kuonyesha sura.3

“Hatuchagui wanawake kwa ajili ya kuwapeleka kuonyesha uzuri kuna vigezo lazima tuwapime uelewa. Lazima kujua wana uwezo upi wa kufuatilia mafunzo watakayopewa ili watoe huduma inayotakiwa kwa wateja wetu na si sura,” alisema Ladislaus Matindi, mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL).





photo_2019-11-07_16-00-36.jpg

Pia soma
 
Haya mambo hayafai kuyasema hadharani
Ni insensitive sana kumuambia air hostess hana mvuto wa kuwa air hostess.
Kuna kipindi walikuwa wakiwakejeli mtandaoni, dah niliona watu hawajali kabisa hisia za watu
Kama ni ushauri unatoa tu kimyakimya kwa wahusika wanaufanyia kazi
 
Biashara ni mvuto. Huyo Msukuma aliemkatisha hana hoja, kama umezaa mfupi si tatizo, ila ajira hiyo inahitaji warefu wenye mvuto, hivyo hatuwezi kulazimisha kuajiri wasio na mvuto.
Kwani ndege zinabeba wanaume tu ili wavutiwe na hao wahudumu wanawake? Ndege Zina wahudumu wanaume pia haya huyo mwilima atueleze vigezo vya mhudumu mrembo wa kiume aweje?
 
Msimlaumu sana pengine yeye anatafsiri tofauti ya maana ya mvuto.
 
Hiyo ni biashara, na kila biashara inahitaji vigezo wanavyovitaka wao. Kama hao ma air nini sijui wanatakiwa warefu labda. basi wafanye hivyoo. Mbona hamsemi mashirika yale ambayo mpaka wakuajiri basi eti uwe na uzoefu wa miaka kadhaa sehemu fulani?

Huo nao si ubaguzi?
 
Wanawake watanzania nashauri ikodiwe ngoma ya wale wapiga ngoma maarufu wa pwani wapiga ngoma za kusuta wanawake hovyo na kwenda na ngoma hiyo kwenda kumsuta bungeni huyo Husna Mwilima huku kila mwanamke akiwa kavaa kanga yenye maandishi ya matusi ya nguoni ya kumporomoshea huyo mbunge Husna Mwilima.

Ikishapatikana Spika ataarifiwe kuwa kuna ngoma inakuja pigwa kwenye viwanja vya bunge
 
Back
Top Bottom