Mkuu Wangu Halisi,
I love it, saafi sana, sasa mkuu kuna jamaa yangu amekuona hapo Dodoma, nishitue kama bado upo hapo ili nikupe mikoba zaidi pa kwenda kuchota more dataz,
Tanzania, tumetoka mbali sana kisiasa, kuna ambao hawakuyaona ambayo wengi tuliyapitia huko nyuma ya jinsi tulivyokuwa tumebanwa, mimi Town yaani Dar, zamani niliwahi kuishi na mkali wangu anayeitwa Bob Bayona, yaani wing moja kwenye gorofa moja Down Town, ambalo ndani lina hoteli ya Son-Afrique Hotel, next to Business College,
Bayona, the man alikuwa msomi sana na mtu mweye kichwa hasa, lakini the guy alikuwa mlevi sijawahi kuona, akishalewa alikuwa na tabia ya kusema hovyo sana kuhusu ubovu wa serikali kama tunavyosema hapa JF yaani kukosoa, man! siku moja saa kumi na moja za asubuhi watu tunarudi kutoka mangomani, ilikuwa Jumapili unajua enzi zile mambo yote yalikuwa Msasani Beach kwa JPP na Choggy, tukakuta jengo zima limezingirwa na watu hivi design design, duh tukaambiwa hatuwezi kuingia ndani mpaka wamalize shughuli zao, kuja kushitukia eti jamaa ni maajenti wa Serikali wamekuja kumchukua Bayona kwamba anataka kupindua serikali ya Mchonga, daaamn!
Hata wafagiaji wa lile jengo na Hotel could not believe it, I mean the man was so loved in the building and so harmless kwamba hata watoto wadogo mle jengoni wasingeweza kuamini, halafu jamaa all the time kama hayuko kazini ameutwika ugimbi, sasa atapindua vipi serikali? Tulipaoiifutailia zaidi ile ishu huko kwa wakubwa tukaambiwa, hivi huwa hamumsikii akisema sema hovyo kuhusu serikali, Bayona, na kwamba alikuwa akishirikiana na Ngaiza na wengine kina MCgheee, alipelekwa somewhere kisiwani for the next at least three to four years, siku alipotoka hatukuamini jinsi mkulu aliyekuwa na afya njema na jitu miraba minne halafu unajua jamaa alikuwa lightskinned hivi mweupee ukim-cheki kwa wasi wasi utadhani mtishi, wote tuliomuona tulilia machozi!
Sasa my point ni kwamba ni rahisi kwetu sisi hapa kusema na kudharau, baadhi ya wabunge na wananchi wengine kwa ujumla, kama kina Kubenea, wanaojaribu kwa kila hali kwa kujitoa mhanga, kuikoromea serikali kwa faida ya sisi wananchi, sasa hivi kuna njama kubwa sana inapikwa ya kumtoa Spika, sawa kuna some ishus ambapo wanaonekana kuwa hawako na sisi, lakini wakuu ninaomba kusema kuwa sometimes sisi wananchi tunahitaji ku-appreciate madogo yanayotafutwa na viongozi wetu, regardless ya vyama vyao kinachofanyika sasa hivi bungeni ni hatua kubwa sana, wakuu ukilinganisha na tulikotoka as a nation hasa kwa wale tulioona na kuishi angalau kidogo on zile enzi za noma, leo tuna wabunge ambao wako radhi kufanya anything ili ishu nzito za wananchi zisisemwe kabisa, tena wengine ni vijana kama sisi!
Naomba kutoa Hongera kwa wabunge wetu wote wanaotupigania sisi wananchi bungeni, kwa kazi nzito wanayoifanya huko bungeni, kuna wananchi ambao tuko nyuma yenu, na mtalipwa na Mungu tu!
Mungu Aibariki Tanzania.